Mbowe afunika Urambo jimboni kwa Mh. Sitta

Mbowe afunika Urambo jimboni kwa Mh. Sitta

laki si pesa hata kinana akifanya mkutano watu wanaoenda hawana kazi?
_je mdee naye alikuwa na chopa? angalia na mkutano wa bunda kama kuna chopa....
::::alafu ID za lumumba zimebaki nne tu jf

posho zimekata selikari imefilisika kwa ufisadi na sasa ivi haipati misaada kwa wahisani mpaka waache ujangiri na ubadhirifu
 
Last edited by a moderator:
Amepata aibu tu watu hawafiki hata idadi ya watu wa kitongoji kimoja.
 
mbona sita akiwaita hawaendi hivyo?na kumbuka hao hawajapelekwa!!bakini kusema wamekwenda kushangaa chopa
 
Cdm pigeni mikutano na vijijini pia! Mfano vijiji vingi vya mkoa wa ruvuma hakuna cdm wala vyama vya upinzani!
 
Sijui wenzangu mmeona aina ya wahudhuriaji wa hii mikutano. CcM wengi wa wanaohudhuria ni wakina mama na wazee na baadhi ya wasichana. CDM wengi ni vijana wa kiume na baadhi ya wababa ambao sio wazee. Kuna kundi ambalo halijalengwa vijana wa kike na watu wa umri wa kati. CdM inabidi kuconnect na wakina mama kama ikitaka kushinda. Vijana si wa kutegemea sana kwani siku ya kupiga kura sometimes hawajitokezi kwa kuwa wana priorities zingine hata kwenda kwenye pombe. But women wakp loyal. Ndio maana ccm inashinda. Vijana wakihamasishwa na wakiamua kukataa kuchaguliwa viongozi na wazee wao tutaona changes

umefatilia mikutano ya Bawacha?...wengi wa wazee unaowaona kwenye mikutano ya ccm ni mabalozi wa nyumba kumi..
 
sitta hivi yupo wapi sijamsikia siku nyingi yupo kweli Kamanda Mbowe endelea na harakati za kuifuta delete kabisa ccm
 
View attachment 200513
View attachment 200514
View attachment 200515
mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), freeman mbowe akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa urambo, katika mkutano wa hadhara wa oparesheni delete ccm, uliofanyika kwenye uwanja wa extended juzi.
View attachment 200514
View attachment 200516mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), freeman mbowe akiwasili kwenye uwanja wa extended mjini urambo, ambako alihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya oparesheni delete ccm
View attachment 200517
siku za mafisadi zina hesabika- futa delete kabisa ccm
futa delete kabisa ccm nchi nzima
 
Viongozi wa CHADEMA wilaya ya Urambo majina yao ni nani tafadhari mwenye nayo ayaweke hapa.

Mi nimechoka kujaza watu kwenye mikutano alafu tunashindwa chaguzi kwa kukosa mizizi (uongozi imara) ngazi za chini.

Kujaza watu kwenye mikutano ni kawaida yetu CHADEMA tangu 2005 Mbowe alipokuwa mwenyekiti. Kilicho adimu kwetu kwa sasa ni USHINDI.

USHINDI USHINDI USHINDI
 
Urambo. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.

Katika mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa Extended mjini hapa takriban mita 100 kutoka nyumbani kwa Sitta aliyeongoza Bunge la Katiba, Mbowe alisema historia ya nchi hii itamhukumu mbunge huyo kwa maovu hayo.

Alisema kutokana na uovu huo wa Sitta ambaye amekuwa akiisifia Katiba Inayopendekezwa kuwa itakuwa nzuri Afrika Mashariki na Kati, vyama vya upinzani vitaendelea kuidai katiba ya wananchi hata kwa miaka 100 ijayo.

Aprili mwaka huu, wabunge wa vyama vya upinzani chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walisusia Bunge la Katiba mjini Dodoma wakilalamikia kuvunjwa kwa kanuni na kutofuatwa kwa mapendekezo ya wananchi yaliyotolewa katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye Operesheni Delete CCM, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema ana uhakika Sitta ataipata hukumu hiyo ya historia kwa kile alichosema kudhulumu haki ya Watanzania milioni 45.

Mbowe anayetumia chopa katika ziara hiyo, alifika katika uwanja huo saa 11.45 na kuhutubia kwa dakika 30.

"Mzee Sitta najua upo nyumbani hapo na unanisikia, kama hunisikii basi mke wako Mama Margreth Sitta atakuwa ananisikia, lakini kama naye hayupo basi kutakuwa na wahudumu watanisikia na watakuja kukueleza," alisema huku akiwaonyesha wafuasi wa chama hicho nyumba ya Sitta iliyopo jirani na uwanja huo.

Alisema Sitta alipuuza maoni ya wananchi waliyotoa katika mchakato wa Katiba Mpya na ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba badala yake akaweka maoni ya chama chake cha CCM.

"Tunasema kwamba historia ya nchi hii itamhukumu kwa maovu aliyoyafanya kukataa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya chama chake," alisema.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, alisema baada ya maoni ya wananchi kuchakachuliwa... "Sasa tutaidai Katiba Mpya hata kwa miaka 100 ijayo."

Alisema wabunge wa vyama vya upinzani walimwamini Sitta kwa kumpigia debe na baadaye walimpa kura iliyomfanya awe Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kutokana na rekodi yake alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Tulifanya hivyo kwa kumwamini kutokana na rekodi zake akiwa spika, tunajuta kumchagua hatukufahamu kwamba atatusaliti na kudhulumu haki za Watanzania," alisema Mbowe.

Hivi karibuni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi alilieleza gazetin hili katika mahojiano maalumu kuwa Sitta aliwageuka wapinzani baada ya kuwaomba wamchague kuwa mwenyekiti akiahidi kupigania serikali tatu, lakini baada ya kupata nafasi hiyo akapigania serikali mbili, madai ambayo Sitta aliyapuuza akisema Sugu hakuwa saizi yake.

Mbowe alisema Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alidiriki kuwatukana hata viongozi wa dini waliomshauri kuhusu umuhimu wa maoni ya wananchi katika Katiba.

Wakati wa Bunge la Katiba linakaribia ukingoni Septemba mwaka huu, Sitta alitumia maneno makali kuwajibu viongozi wa dini waliotoa waraka kukosoa mwenendo wa Bunge hilo, akisema waraka huo ulikuwa wa kipuuzi na haukuwa na utukufu wa Mungu.

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobazi Katambi alisema kwa heshima ya wananchi wa Mkoa wa Tabora, Sitta (72), anatakiwa kupumzishwa katika nafasi zake zote za uongozi kutokana na umri wake.

"Ni kweli mzigo mzito anatakiwa kubebeshwa Mnyamwezi lakini kwa umri alionao Sitta ni kama tunamkosea adabu kwani huu ni muda wake wa kupumzika, tusimchague tena," alisema huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Ufisadi bomba la gesi

Mbowe alitumia mkutano huo kuitaka Serikali kuitisha wakaguzi wa kimataifa ili wachunguze mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambao alidai kuna ufisadi wa Sh1.2 trilioni, vinginevyo atawaeleza wananchi ili waamue.

Juzi, Mbowe aliwatuhumu vigogo wa Serikali kuwa waliongeza fedha katika mradi huo ambazo waligawana kwa masilahi yao binafsi lakini mkopo huo kutoka China utalipwa na Watanzania wote.

Alisema mradi huo ulikuwa wa Sh1.2 trilioni lakini vigogo hao waliongeza kiasi kama hicho na kugharimu Sh2.4 trilioni.

Alisema ukaguzi unatakiwa kufanyika ili kufahamu thamani ya fedha halisi zinazotakiwa kujenga bomba hilo na fedha zilizotolewa na Serikali.

"Hili nitalisema popote bila woga na niko tayari kukamatwa lakini sitakaa kimya nikishuhudia Watanzania wakilipa deni la fedha walizogawana vigogo hao," alisema Mbowe.

Alisema ikiwa Serikali ina nia ya dhati kupambana na ufisadi, iweke hadharani mkataba wa ujenzi wa bomba hilo... "Ndiyo maana mikataba hii imekuwa siri, inafichwa ili wananchi wasiione lakini tunasema Chadema tutaendelea kuipata na mafisadi watajulikana."


Chanzo: Mwananchi

 
gud! huu ufisadi wa bomba la gesi bado haujapewa msukumo mkubwa na attention kubwa katika media ili tuweze kuuelewa vizuri, ilikuwaje, nani kahusika na kwa nini?
 
Wekeni picha sioo mnalopoka tu wakati nilikuwepoo hakuna watu zaidi ya viongoz wote wa mkoa wa tabora aaaaaaaaaaaa ccm haitishiki na mitandaooo
 
Back
Top Bottom