Mbona voda wahuni?

Mbona voda wahuni?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,260
Nimenunua modem ya voda juzi tu. Tatizo inakula sana. Nimeongea na customer care usiku sana maana muda wa mchana hawapatikani. Jamaa akaniambia kununua bundle niweke elf 10 kisha nitume neno bomba7 kwenda 15300 nitapata net ya wiki nzima regardldess unatumiaje. Nimeweka asubuhi elf 10 ajabu nimetumia kwa saa moja tu! Huu si wizi? Au sikupewa maelezo ya kutosha?
 
hamia airtel ndugu yangu,moderm zao ziko fresh na wanakata kidogo 2.
 
We vp. Ukiweka elfu kumi tuma sms BOMBA7 kwenda no 123. Watakujibu kuwa tayari umenunua bundle. Sasa wewe baada ya hiyo saa moja ikawaje? Kwa hiyo BOMBA7 unatumia unlimited kwa wiki nzima Pia waweza chukua BOMBA30 kwa Elfu 30 kwa mwezi.
 
sasa kuna wazimu mmoja huko customer care aliniambia nitune BOMBA7 kwenda 1530. kumbe ni 123? nashukuru ndugu hapo juu
 
Hamia tigo,hakuna longo longo kabsa.
 
Hizo namba zote zinatumika kupata bundles na unlimited,inawezekana kuna kosa la kimaandishi wakati wa kutuma ndio likatokea hilo tatizo.Hata mimi kuna wakati niliomba huduma ya bomba7,kabla sijathibitishiwa nikaanza kutumia net,ndani ya saa 1 pesa ikaisha.
 
sasa kuna wazimu mmoja huko customer care aliniambia nitune BOMBA7 kwenda 1530. kumbe ni 123? nashukuru ndugu hapo juu

Zote ziko applicable mkuu,na co 1530 ni 15300. Baada ya muda hyo code ya 123 itafutwa na itatumika hyo nyingne.
 
Nimenunua modem ya voda juzi tu. Tatizo inakula sana. Nimeongea na customer care usiku sana maana muda wa mchana hawapatikani. Jamaa akaniambia kununua bundle niweke elf 10 kisha nitume neno bomba7 kwenda 15300 nitapata net ya wiki nzima regardldess unatumiaje. Nimeweka asubuhi elf 10 ajabu nimetumia kwa saa moja tu! Huu si wizi? Au sikupewa maelezo ya kutosha?

Si kweli mkuu unaponunua unatumia siku 7,pale unapewa zaidi ya 1GB. Sasa inakuwaje bundle hyo iishe kwa saa moja tu.
 
Nadhani ni wale jamaa wa customer care walini mislead, pamoja na ugeni wa kutumia hii huduma. kwa sasa ninachofanya nimeweka line yangu ya kawaida kwenye modem na ilikuwa na elf 10. nilichofanya nilitoa line niliyopewa ambayo niliweka hela kimakosa. inafanya kazi fresh tu. haiwezi kuleta madhara kwenye hii laptop?
 
Ni kuhama, airtel ndio mambo iko huko, japo najua nawafanyia promo lakini majamaa wako fit, voda watu tulishakimbia siku nyingi, hawafai
 
Ni kuhama, airtel ndio mambo iko huko, japo najua nawafanyia promo lakini majamaa wako fit, voda watu tulishakimbia siku nyingi, hawafai
tutacheki na gharama zao mkuu, ila isije ikawa kama katika tangazo lao la kuhamia airtel
 
Kwa maoni yangu, tatizo siyo MODEM wala VODA. Nakushauri u-disable automatic update zote ambazo huwa zinaji update kwenye background bila mtumiaji kujuwa na kumbuka file zake ni kubwa. Hivyo nakushauri u-disable updates kuanzia operating system ya PC yako na application programmes zote ulizowahi ku-down load ljj
 
but remember this is unlimited service for the whole week, so it doesnt matter if there is automatic update or downdate
 
Kwa maoni yangu, tatizo siyo MODEM wala VODA. Nakushauri u-disable automatic update zote ambazo huwa zinaji update kwenye background bila mtumiaji kujuwa na kumbuka file zake ni kubwa. Hivyo nakushauri u-disable updates kuanzia operating system ya PC yako na application programmes zote ulizowahi ku-down load ljj
ohooo, unlimited service
 
nop! kuna kitu ulikosea, likely ulianza kutumia internet kabla ya kupata confirmation ya bundle uliyonunua (SUBIRA). I can tell Vodacom is the best, ukiacha mambo ya promotion za hapa na pale za washindani.
 
There is nothing called Unlimited access! Kuna given amount ya Bytes ambazo zikifika ata baada ya lisaa limoja hiyo Bomba inakwisha. All providers the same apply.
Ukweli ni kuwa Voda,Tigo na wengineo they buy too from Internet service Providers and every bit count,mjini akuna cha bure.
 
Mpilili, Bado maoni yangu kuhusu PC kuji-update programs zake kwenye background bila ya mtumiaji kujuwa ndiyo tatizo kubwa hela kutumika kwa muda mfupi sana regardless ya socalled bundles/unlimited hizo ni gimicky za biashara,.
 
akuna unlimited hapo wizi mtupu unauziwa mb or gb kadhaa ila tgo nawakubali wanayo unlimited yaukweli 45000 kwa mwezi na ipofasta
 
nimejisajili kwenye hiyo bomba saba toka jana saa moja jioni. nimetumia mtandao hadi saa 6 usiku na kufungua mafile makubwa tu na bado muda huu natumia ila naona iko poa tu. hope italast kwa hiyo week
 
kwa maoni yangu, tatizo siyo modem wala voda. Nakushauri u-disable automatic update zote ambazo huwa zinaji update kwenye background bila mtumiaji kujuwa na kumbuka file zake ni kubwa. Hivyo nakushauri u-disable updates kuanzia operating system ya pc yako na application programmes zote ulizowahi ku-down load ljj

hapa kaka ndo uko sahihi!
 
Back
Top Bottom