Tanzania Internet Service Providers: Packages | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Internet Service Providers: Packages

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Maxence Melo, Jul 15, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280

  Baada ya kumsoma Kimori nimefikiria ni vema nikatoa mawazo yangu katika mada mpya ambapo sintovuruga mjadala aliouanzisha. Naamini wengine watakuja na mawazo yao tofauti ama yanayoshabihiana na yangu hivyo kutoa mwanga kwa watumiaji wa Internet Tanzania.

  Ninapoongelea speed ya download (uploads wanaohitaji ni wachache sana) namaanisha bila kutumia Download Accelerators.

  VodaComa as an ISP:
  VodaCom kama hauna package maalum basi gharama yake ni kubwa sana, ni zaidi ya Tshs 300/= per MB. Ni vema kama umedhamiria kutumia VodaCom internet (speed yao sijaridhika nayo ingawa nilinunua bundle ya 5GB toka kwao kwa majaribio) basi jaribu kununua bundle ili kupunguza gharama. Devices (modem) za connection kwa VodaCom ni bei nafuu (170,000/=) hivyo unaweza kununua na kutumia kirahisi. Ukiweka bundle ya walau laki 2 unaweza kuitumia mpaka itakapoisha ndani ya kipindi cha miezi mitatu, uzuri wake ni kuwa una-recharge kwa vouchers za kawaida kabisa. Inafaa kwa normal users wasio na downloads wala uploads kubwa. Statistics za downloads na uploads utaziona kwenye software ya modem yako. Download speed yao haizidi 100kb/s pamoja na kuwa unaweza kuwa na modem yenye uwezo wa 7.2MB/s

  Kuna Zantel:
  Hawa nimekuwa nao kwa muda sasa na mimi ni Postpaid Customer wao, hawa nao nalipia bundle ya 10GB kwa mwezi. Nimekuwa nikitumia service yao kwa zaidi ya miezi 6 sasa na naweza kusema pamoja na kuwa nilishakumbana na matatizo nao lakini mara zote wametoa ushirikiano wa karibu. Hawa download speed yao ni nzuri na kuna wakati inafikia 250kb/s. Kwa bundle hii ya 10GB, nanunua 1MB kwa Tshs 26/= na inakuwa ina VAT ndani yake. Haya matangazo wanayoweka barabarani na kudai wana UNLIMITED Internet service ni lugha ya kibiashara ambayo inamaanisha 3GB kwa 90,000/= wakiwa wamewa-target normal users. Kwa mtu kama mimi ambaye per month najikuta nina zaidi ya 20GB siwezi kukubaliwa kuwa na hiyo ya Tshs 90,000/= per month. Hawa ukikumbana na tatizo na service zao naweza hata kukusaidia endapo utakosa msaada wa haraka kwani modem zao nimezitumia karibia zote na kuna device ambayo ukiichukua kwao hata kama una PC 20 ofisini kwako bado unaweza kutumia modem moja kwa PC zote.

  Kuna Benson Online (BoL):
  Hawa achana nao kabisa, nimetumia service yao kwa miezi 6 hivi, kwa mobile zao ambazo walizitangaza kuwa unalipia 180,000/= kwa miezi 3 na unapewa UNLIMITED (uwongo tu kwani wanakubana kwa speed), lakini mobiles zile zikipata joto tu kwishnei! Aidha, connection ya nyumbani kabisa niliyokuwa nayo speed yake ilikuwa inabidi niache nimefungua page nikazunguke wee ili kukuta page imemaliza ku-load. Internet speed yao haizidi 60kb/s (download speed). Hawafai kwa mtu mwenye kuzoea internet ya kasi. Labda wabadilike!

  Kuna hawa Raha.com:
  Nimekuwa mteja wao zaidi ya miaka 2 sasa, kuna kipindi internet yao ilikuwa speed kubwa sana (3months ago) lakini sasa sijui wameelemewa au ni vipi, imekuwa slow SANA kiasi inakatisha tamaa hata kutumia. I do not recommend them to any of my friends. Bahati mbaya zaidi hawana internet ambayo itakuwezesha mtu kuwa mobile. Labda wabadilike!

  Kuna hawa wageni SasaTel:
  Hata kabla ya kutumia service yao niligundua matangazo yao ni tofauti na walicho nacho, bei zao ziko juu ingawa nilitarajia walivyo wageni wameisoma market ya Tanzania hivyo ni rahisi kwao kuja na package za kueleweka. Hawakujipanga vema, lazima ununue devices za kwao kupata services zao, wamekosea labda warekebishe mapema kabisa.

  Kuna SimbaNet:
  Hawa connection yao ya nyumbani (isiyo mobile) ni nzuri, bado niko kwenye majaribio yake. Pia SimbaNet wapo njiani kuja na modem ambazo ni sawa na za Zantel/VodaCom, nina bahati kuwa nimeichukua moja naifanyia majaribio ili baadae niweze kujua kama watafaa kwenye market yetu. Mpaka sasa speed yao ni nzuri, atleast 120kb/s kwa downloads inaweza kufikiwa. Nina wiki 3 tangu niichukue hii connection yao na bado sijaona tatizo kubwa katika kuunganisha, matatizo mawili ambayo nadhani kwa customers wa Tanzania wanaweza kuyaita matatizo ni kulazimika kutumia password, na kutumia username iliyo complicated kitu ambacho ni rahisi kurekebishwa ndani ya dakika chache (labda walifanya makusudi kwa wateja wa kwanza).

  TTCL Broadband:
  Hawa TTCL ni mwisho wa matatizo! Nina wateja karibia 6 hivi (makampuni) ambapo mimi ndiye naangalia internet services za makampuni haya, wengi nilikuta walishakata tamaa tokana na huduma mbovu za ISP wengine na kuwa na suppliers wasiotoa ufumbuzi wa matatizo yao. Tangu nimeingia makubaliano nao niliamua kutumia TTCL na Zantel kama ISP kwa wateja wangu na wote wawili hawa wameonekana kutatua matatizo ya wateja hawa. TTCL Broadband ina packages mbalimbali lakini ukichukua kama 10GB unalipia Tshs 360,000/=. Hii kwa kampuni ya kawaida inatosha kabisa lakini unahitaji kuwa na mtu au kampuni maalum ya kukufanyia hivyo, ukiwaacha TTCL wenyewe wakufanyie kazi basi ukiritimba wake unaweza kuuchukia kabisa kwani service itakuwa haifurahishi na unaweza kujuta hata kuwa nao. Kinachosaidia kwa wateja wangu ni kuwa nimechukua liabilities zote na kuwa na-deal moja kwa moja na TTCL.

  TTCL wana bundles za aina nyingi, 500MB - 50GB per month. Download speed ni kubwa na inafikia hata 256kp/s bila kutumia download accelerators, ukitumia accelerators inakwenda mpaka 2MB/sec. Kinachofurahisha zaidi TTCL wana Upload speed kubwa tu, inafikia hata 516kp/sec.

  Matatizo ya TTCL Broadband ni mengi kidogo:

  1. Hakuna Post Paid service, ikifika mwisho wa mwezi wanakukatia tu! Yani hawakupi hata dakika ili uka-recharge. Kama una mteja ambaye ana service muhimu unaweza kubeba lawama zisizo zako.
  2. Huduma kwa wateja ni very poor, unaweza kupoteza siku nzima na hela yako mkononi bila kupata service ya kueleweka
  3. Baadhi ya maeneo haifanyi kazi (ndani ya Dar) hivyo unaambiwa subiri walau miezi miwili lakini ukweli ni kuwa hata ikiisha hiyo miezi miwili ukirudi unaambiwa miwili tena!
  4. Wakati mwingine unalipia gharama zaidi ya ulivyotumia, statistics zote unaziangalia online hivyo ukishakatikiwa service huwezi kujua mpaka uende kwenye kituo cha TTCL kujua nini kilitokea na kivipi... Wanakatisha tamaa sana!
  TTCL Mobile:
  Nilikuwa natumia service hii lakini niliiweka chini na modem yake kuigawa BURE kwa mtu aliyeonekana kuipenda. Iko slow na haiwezi kuhimili mikikimikiki.

  Zain as an ISP:
  Zain inafaa katika Blackberry (Tshs 35,000/=) tu. Ninayo Blackberry 9000 Bold na service ni nzuri kwa kiasi chake! Lakini, services nyingine hawana tofauti na VodaCom. Ukitumia Blackberry kwa VodaCom hutotamani kurudia isipokuwa Zain. Kwa Blackberry hapo Zain wamefanikisha!

  ISP wengine kama CATS-Net, iWay Africa n.k nitatoa feedback baadae kwani ndio bado natafuta connections zao ili niweze kutoa comment.

  NB: Haya ni mawazo yangu kwani wengine yawezekana wanapata service tofauti na ninavyoipata. Nimekwishajaribu ISP hao juu na naweza kuwa na mawazo tofauti nikiwarudia mmoja baada ya mwingine kuangalia kama kuna mabadiliko yoyote.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimekubali......una experience na hawa providers....data ulizomwaga hapa zinadhihirisha hilo!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Mimi nina BB ya voda..naiona iko bomba sana sana inafungua kila attachment,ina speed kubwa sana ya internet.....sijui wenzetu wana pata tatizo gani labda....
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bravo!
  Maxence we ni mtaalamu wa hizi mambo
  Sasa mtu na ajihukumu mwenyewe!.
  Tunashukuru kwa ufafanuzi wa kina mkuu.
   
 5. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kimoja ambacho nadhani wengi hawajakishtukia.

  Ukijaribu hizi services zao inakubidi ukae locations tofauti. Ukiingia Youtube inawaumbua wengi kwani video hazi-load kabisa na wengine unakuta service inaji-restart (modem).

  Ukitaka kujua speed ya connection husika unaweza kutembelea Speedtest.net - The Global Broadband Speed Test uone.

  Aidha, matangazo ya uwongo na lugha za kibiashara kwa wateja vina-mislead watu sana.

  Binafsi nalazimika kujaribu connections nyingi kuweza ku-recommend kwa wana JF wengi wanaotoka abroad kwani wengi wamezoea services zenye speed nzuri na wakija nyumbani hawajui wapi waende.

  Nimewapeleka wengi Zantel japo hata hawajui kama tunawasaidia kuongeza wateja.

  Mkuu Next Level, kama unahitaji connection mojawapo (wireless) ili uifanyie test (nimeshailipia mwezi mzima) naweza kukupa na kukuruhusu u-download kitu chenye ukubwa wa 1GB uone kasi yake itakuwaje. Free of charge kwani mwisho wa mwezi nitalipia bill yake. Am in Dar and you have my cell #
   
 6. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Ninayo Blackberry 9000 Bold ya VodaCom na naweza kukupa number yangu katika PM for confirmation lakini nikuhakikishie kama umeiona hiyo nzuri basi jaribu kutumia Zain (simply ondoa line ya Voda na weka Tshs 35,000 za Zain maana line ya Zain unaipata kwa Tshs 500/= tu) kisha jaribu kuona difference utakubaliana nami kuwa Zain kwa Tshs 35,000 per month tena UNLIMITED (hawajashtukia sijui?) ni bomba zaidi ya hiyo VodaCom.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu jaribu kuwafuatilia na hawa CTV natumia mimi napewa 2GB kwa siku 30 gharama yake ni $42 wapo Samora pale Harbour View Hotel.
   
 8. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ni kweli unajua mambo
   
 9. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Nitainunua this week, tuonane basi mkuu mbona kimya sana wewe?

  Halafu kama ni $42 kwa 2GB basi hao ndio watakuwa Cheapest ISP in Tanzania kwa sasa mkuu....
   
 10. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BUNDLE PLAN ZA VODA

  TSHS | MB | RATES/MB
  2,000 | 10 | 200
  3,700 | 20 | 185
  15,000 | 100 | 150
  25,000 | 250 | 100
  40,000 | 500 | 80
  72,000 | 1,024 | 70
  108,000 | 2,048 | 53


  Brochure moja nimeona ina hizi rated za bundle;
  Naona lengo la voda ni kuwahamasisha wateja wao kuwa ktk Plan za bundle; pia nimeona kuhusu speed binafsi huwa naingia ktk forums kwa kutumia N series phone; mitandao mingine nilishindwa kabisa labda kwa sasa; ila nahisi pia inategemea mteje uko wapi na je ni peak hours kiasi cha kushare bandwidth ile ile na hii hutokea kote kote
   
 11. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Mkuu Malunde-malundi,

  Vema ume-edit post na kusema ni bundles za VodaCom.

  Lakini nikukumbushe kitu: Endapo unatumia N-97 (Naitumia kwa sasa kujaribu VodaCom ikoje katika simu hii kwani ni mpya kwenye market) au N96 ku-browse kwa kutumia VodaCom basi hakikisha una-disable ku-display images kwenye browser. Ila kama umelipia kwa bundle madam bei naona wamepunguza sana basi haina tatizo ku-display images.

  Raha ya surfing uone kila kitu including images. Hizi bei wamezitoa last week? Manake ni mpya kwangu, 2GB kwa 108,000/=? Nakumbuka last time ilikuwa ni laki 2 hivi.

  Halafu, hata hivyo bei hiizi ukiangalia hiyo 2GB bado wanakukamua Tshs 53 per MB! Zantel wanacharge Tshs 26/= incl VAT. You can compare...

  Halafu angalia kwa user anayetumia simu kawaida bila kununua bundle anachajiwa kiasi gani... 200Tshs per MB na hapo uangalie vema wameweka nyota (*) wakimaanisha hakuna VAT hivyo nayo utakamuliwa baadae.

  Kama kuna ambaye amejaribu kuangalia, ukitumia internet ya VodaCom bila ku-subscribe kwa bundle mwisho wa mwezi unakuta umetumia hela kubwa sana kuliko hata ile ya kupiga simu.
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Voda 2Gb ni 95,000/= ndo natumia sasa hivi.

  Bei kamili ni hizi zipo kwenye website yao.

  Vodacom Internet Prepaid bundles* Standard Volume/MB Monthly Subscription To purchase, SMS this keyword to 123. MyMeg 10 10MB
   
  Last edited: Jul 15, 2009
 13. ocade

  ocade Member

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 26, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka mbona umeatenga zain,

  mbona hujadiscus zain nao data card za zikoje,

  sab mimi nikizitumia maeneoi ya sinza napata speed mpata 365kbps, na maeneo ya kijitonyamana napata mpaka speed ya 7.2Mbps
   
 14. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  YES,

  VodaCom hiyo 2GB ni 95,000/= kweli currently. That means bei hiyo ni sawa na Tshs 46.4/= per MB. Still expensive!

  Zain nimeandika kitu mkuu, Speed ya 7.2Mbps ni ya modem mkuu, huwezi kuipata kwa Bongo yetu hii hata uwe umekaa ndani ya ofisi za Zain pale K'nyama!

  Blackberry (BB) ya Zain nimekiri kuwa ni service murua kabisa na inakidhi mahitaji ya mtumiaji. Kuna email 4 nimetumiwa na wote nimewajibu.

  Kwa wale wenye BB na wanataka kutumia internet ya Zain unatuma ujumbe BB kwenda 15344 lakini hakikisha simu yako ina walau Tshs 35,000/= ili uweze kupata huduma hiyo kwani kama salio halitoshi hutopata huduma yao.
   
 15. Kivuko

  Kivuko Member

  #15
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  so,
  who is a true unlimited ISP provider in TZ?one that charges in terms of Speed like 512kb/s and not size-like(2GB etc).
  if i were to use internet i would prefer speed over size.
  Also do we have any LAN providers yet?
   
 16. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #16
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Nothing UNLIMITED! Ni lugha za kibiashara mkuu.

  Halafu kama una kampuni unajua unataka kuwa hustle free unaweza kununua 20GB ya TTCL kwa Tshs 450,000/= kwa mwezi na speed nakuhakikishia ni ya kueleweka. Tatizo ni kama nilivyosema awali, usi-deal na TTCL moja kwa moja, kama unaweza kupata mtaalam ambaye ni mwaminifu akakusaidia ku-deal nao basi inakurahisishia mambo na kukusahaulisha kero za internet.

  Kuna jamaa nilimfungia TTCL lakini baada ya kupata speed nzuri alijikuta kawa addicted kuangalia Google Videos kitu kilichopelekea kuwa anatumia internet ya zaidi ya 20GB per month. Ni tatizo lake yeye na wafanyakazi wake!

  Tatizo la TTCL katika packages hizi ni kuwa kama umeshanunua mojawapo ili ku-upgrade inabidi kuandika barua upya ukieleza kwanini uwe upgraded na ikapitishwe na wakubwa (kwa maelezo yao) ndipo uweze kuwa upgraded na haiwezekani katikati ya mwezi!

  Satellite connections unaweza kuchukua kwa SATCOM lakini bei zao utakoma kuringa.

  Ni heri kuchukua 50GB ya TTCL kwa 1,000,000/=
   
 17. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ya lakini nadhani ndo cheapest GSM option au sio? Zain mpaka uwe na modem ya CDMA, mimi natumia sana kwenye simu yenyewe na ninaiunga kwenye laptop pia.
   
 18. Kivuko

  Kivuko Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh,i can imagine of how much i am accustomed to use now,as i use everything from TV,movies to RADIO on the internet.am sure in 2 days ntamaliza monthly package!

  as you put it.ni ukiritimba tu.competition is needed here.wata-upgrade even overnight!

  satelite ni expensive in nature of it's technology ndio maana haishikiki.ndio iliyotufikisha hapa tulipo sasa.kwenye bei ghali
  this looks promising if it didn't cost an arm and a leg!

  our way to development is really really long.tuombe mungu tufike siku moja
   
 19. Kivuko

  Kivuko Member

  #19
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa sasa hivi,i am sure you will never break 1mp/s limit in a cellphone,especially in TANZANIA,may be later.

  kuna vitu kama latency,QoS vinavyo-worsen network perfomance,na hata aina ya simu utumiayo.

  if you go to Speedtest.net - World Results

  highest speed download speed a Tanzanian ISP can offer ni 0.74mb/s that is around 800kb/s (nadhani TTCL) most wako well below 0.5mb/s sort of 512kb/s

  test for yourself don't let advertisers fool you.
   
 20. BrainPower

  BrainPower Senior Member

  #20
  Jul 16, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thanks for the info Mkuu,

  Kama uko Bongo ninge shauri ufanye speedtest speedtest kupitia mirror yao iliyopo TIX. If your ISP is connected with TIX then Itakupa more realistic results.

  Link ya Speedtest in Tanzania
  http://stats.tix.or.tz/speedtest/

  Kama mkuu alivyosema hapo juu. 7.2Mbps is not your internet speed. Hiyo ni connection kati ya data card yako na Cell tower base station. Ni kama ukiconnect lan cable (ethernet) kwenye laptop/pc. "Windows inasema local area connection is now connected -100mbps". Well that doesn't mean your internet speed is 100mbps but your local connection (from PC to switch/router is 100mbps).

  Kuongezea , kwasababu nimefanya kazi na 3G technology ninajua kwamba speed ya 3G datacard can be affected by small things like
  A rooftop made from lead, Network Congestion etc..etc. Nilivyokuwa chuoni nilikuwa nashangaa kwanini siwezi kupata 3G internet wakati wa peak times (early morning , break time , evening). Kumbe wakati huo watumiaji wa simu za mkononi wa mtandao yangu walikuwa wengi. Na hilo mjue !

  Well i use a WiA Dedicated connection. And i download 2GB per day. I don't pay for the download sizes but you must be willing to pay for the dedicated connection. If you are a heavy user look for isps who offer dedicated services, most of them charge you on the speed you selected and not the quota.

  Please Come again..? - i didn't fully understand what you meant by LAN providers. Do you mean LAN isps like CTV and Hotspot (i know its a computer term but - do believe me its also an isp in Dar).

  Reality check:
  Wajamini na speed hizi tumeachwa mbali na nchi nyingine duniani.

  Lakini Tutafika tuu. Tuko mbali ila tutafika tuu. Inabidi tufike. Kwani ni muhimu lazima tufike - (B.P 2009)


  BrainPower
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...