Mbona umekuwa adimu!!!

Mbona umekuwa adimu!!!

Hapa mie nakuwa kama ng'ombe aliyenyimwa ndevu...lol!

pole sana Zinduna?

Sasa wapi panauma zaidi?
 
Last edited by a moderator:
kweli dunia duara
mapenzi si masihara
mtu kuwa taahira
mbele ya hadhira

mabazazi kujifanya maimam
kumrubuni mtu timam
ili tu kukidhi hamu
haya mapenzi mim sina hamu ...

Al jununi fununi.
Ati mahaba kizungumkuti..
Hata mwenye zake akili...
Utadhani kafungwa kizuizui....

Buibui na utando wake.
Yeye ndo kitanda chake..
Zinduna naye ana wake...
Kama Pemba na Chake Chake...

Ila yeye wake ni Kichuna.
Na kimya kimya kapotea..
Katoweka na lote huba...
Mahabuba wake kamwachia....
Maumivu yarabi toba!
 
Al jununi fununi.
Ati mahaba kizungumkuti..
Hata mwenye zake akili...
Utadhani kafungwa kizuizui....

Buibui na utando wake.
Yeye ndo kitanda chake..
Zinduna naye ana wake...
Kama Pemba na Chake Chake...

Ila yeye wake ni Kichuna.
Na kimya kimya kapotea..
Katoweka na lote huba...
Mahabuba wake kamwachia....
Maumivu yarabi toba!


Zinduna amezinduliwa
na moyo ametobolewa
Sasa ana waya waya
mapenzi ameyagwaya

Mapenzi siku hizi tabu
hata ukiwa kibabu
Ni maradhi yasiyo na tabibu
hata ukinywa kikombe cha babu...
 
Zinduna amezinduliwa
na moyo ametobolewa
Sasa ana waya waya
mapenzi ameyagwaya

Mapenzi siku hizi tabu
hata ukiwa kibabu
Ni maradhi yasiyo na tabibu
hata ukinywa kikombe cha babu...

Basi aje kwangu ajimwaye mwaye
Kama yangeyange kwa raha zake
Kama pete na kidole
Mimi na yeye polepole

Utabibu wangu si ngekewa
Ni kipaji toka kwa jaala
Mie sijigambi kuoteshwa
Bali haya ni majaaliwa
 
Basi aje kwangu ajimwaye mwaye
Kama yangeyange kwa raha zake
Kama pete na kidole
Mimi na yeye polepole

Utabibu wangu si ngekewa
Ni kipaji toka kwa jaala
Mie sijigambi kuoteshwa
Bali haya ni majaaliwa


Nahofia asije kanyaga moto
baada ya kuruka majivu
usjejitangaza mganga
kumbe ndo mchawi mkuu

tukampoteza Zinduna wetu
bora sasa alialia kikwetu
kuliko huko aje alie mdomo juu
Kwa kurushwa roho juu juu
bora sasa
 
Humu kuna malenga wa nguvu!
mwaJ mzima wewe?? nilifurahi kukuona jana! MUUMBA JUU ATUPE PUMZI, TUENDELEE KUONANA TENA NA TENA WANGU!
 
Last edited by a moderator:
mwaJ mzima wewe?? nilifurahi kukuona jana! MUUMBA JUU ATUPE PUMZI, TUENDELEE KUONANA TENA NA TENA WANGU!

Sijambo dear. Hunishindi mie, nilifurahi sana sana. Ni kweli sasa tutaweza kuonana tena na tena nje ya JF.
 
Zinduna: Umekuwa adimu kwa yangu mazoea..
Mimi: Mazoea yapi tena hayo mpenzi Zinduna?
Zinduna: Umekuwa mgumu hata kunisalimia.
Mimi: Nisamehe kwa hili zinduna jitajitahidi kujirekebisha la azizi
Zinduna: Umekuwa huna hamu, mimi nawe kuongea.
Mimi: hata kwa hili naomba msamaha kuanzia leo ntaongea nawe kipenzi
Zinduan: Utanipandisha wazimu, kimya kikiendelea
Mimi: basi usipandishe wazimu maana ninakujua patachimbika Mpenzi
Zinduna: Unanipa majukumu nisiyoyatarajia.
Mimi: Naja kwako sahii kukupunguzia majuku mpenzi
Ziduna: Hata Meseji jamani washindwa kunitumia?????
mimi: Mpenzi subiri nijiunge na Tigo ext. ntakutumia
Zinduna: Au umedhamiria roho yangu kuitoa???
mimi: Niitoe niipeleke wapi mpenzi sikujua kuwa nakurusha roho namna hii nimekwishakuomba msahaha natumai umenisamehe na kuanzi sasa utafura jinsi ntakavyo kuhandle

Zinduna: Nakusalimu huko uliko La Azizi wangu ...............
Mimi: Asante kwa salamu nami pia nakusabahi La Azizi
 
Last edited by a moderator:
Umekuwa adimu kwa yangu mazoea..
Umekuwa mgumu hata kunisalimia
Umekuwa huna hamu, mimi nawe kuongea.
Utanipandisha wazimu, kimya kikiendelea
Unanipa majukumu nisiyoyatarajia
Hata Meseji jamani washindwa kunitumia?????
Au umedhamiria roho yangu kuitoa???

Nakusalimu huko uliko La Azizi wangu ...............

Salamu zimfikie, popote alipo lazio
pole zikufikie, kwa hofu akutiayo
ushauri nakupa mie, baki na wako moyo
binadamu simwamini, siku moja takuumbua!

Mimi nimeliamua, tangu mwaka kuingia
moyo sitoufungua, katu katu asilia
machungu sitoyajua, ya kuachwa na kulia
binadamu simwamini, siku moja takuumbua!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom