Hivi karibuni akiwa nyumbani kwao Chato alisema kuna mtu anapokea mishahara 17 na akaahidi kufyeka mishahara ya namna hiyo. Imenichukua muda kufikiria suala hili na kiukweli nimekosa majibu.
Kwanza watanzania na dunia nzima wanajua kwamba kabla ya mwezi October mwaka jana Magufuli alikuwa anapokea mshahara wa ubunge na uwaziri kwa pamoja. Na kiukweli hakuna kumbukumbu yoyote kwamba aliwahi kukemea popote matumizi hayo mabaya ya fedha za umma na hajazirudisha mpaka leo.
Lakini pia hata leo mawaziri wake wanapokea mishahara ya ubunge na uwaziri. Anapotwambia anabana matumizi simuelewi kabisa. Unalaumje watu wanaopokea mishahara mingi wakati inaanzia kwenye serikali yako? Wale wanaosema maigizo hawana hoja?