Magufuli aliahidi kuboresha mafao ya Wafanyakazi. Badala yake kavuruga maslahi yao, na ametumia fedha za mafao yao kujipaisha zaidi

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Moja ya simulizi za kusikitisha katika utawala wa awamu ya Tano, ni kisa cha wafanyakazi wa Tanzania. Zipo kada nyingi zilizoumizwa sana na utawala huu, mojawapo nyingine ni wakulima. Hawa wote wametumika kama nyenzo tu ya kufanikisha miradi ya awamu hii, huku wao wenyewe na familia zao wakiachwa kwenye mateso na lindi la ufukara. Nachelea kusema kinachofanyika kinakaribia mfumo wa utumwa haswa.

John Joseph Pombe Magufuli, wakati anajinadi 2015, aliahidi, kati ya ahadi nyingi, kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Na baada ya bajeti yake ya kwanza, alitamka kwamba ataanza kuyaboresha "baada ya mwezi mmoja au miwili", akidai kwamba haiwezekani kuboresha maslahi kabla ya kukamilisha zoezi la kuhakiki WAFANYAKAZI HEWA. Hilo lilionekana ni busara iliyo wazi kabisa. Wafanyakazi wakavuta subira.

Kusema kweli uhakiki ulifanyika, watu walihakikiwa zaidivya mara 4, lakini mishahara haikupanda, ila bei mbalimbali na gharama za maisha, ziliendelea kupanda.

Miezi haigandi, ikasonga mbele, ukawa mwaka, na zaidi. Baada ya kuachana na kisingizio cha uhakiki wa wafanyakazi, Serikali ya JPM ikabuni kibwagizo kingine: maboresho ya wafanyakazi yapo ndani ya maboresho ya maisha ya watanzania wote. Barabara zinazojengwa, ujenzi wa reli ya SGR, mradi mkubwa wa umeme wa Stigler, fly over, ununuzi wa ndege, na mengine mengi.

JPM aliridhishwa sana na hoja hii, kiasi kwamba baada ya hapo, akisikia kilio cha kuboresha maslahi ya wafanyakazi, alikuwa anajibu kwa ukali: kama unaona mshahara hautoshi, nenda kalime! Hapo JPM aliridhika kabisa kwamba ametekeleza ahadi yake ya kuboresha maslahi yavwafanyakazi.

Na kwa kweli, kuna wakati aliahidi kwamba kabla ya kumaliza awamu hii ya miaka 5, atatekeleza ahadi yake. Mpaka hivi sasa keshavunja bunge, kwa hiyo keshawahadaa wafanyakazi kwa mara nyingine.

Inafaa kukumbuka kwamba kama mishahara ya wafanyakazi haiongezwi, basi maana yake vipato vyao vinashuka, kwa sababu gharama za maisha zimepanda sana kipindi cha Magufuli, ili kugharimia miradi mingi aliyoianzisha bila kuzingatia uwiano katika sera za uchumi. Kwa hiyo maana yake ni kwamba kiuhalisia, badala ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi, ameyadunisha kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni pamoja na maisha ya watanzania wote kwa ujumla wao, wamefukarishwa zaidi.

Lakini Magufuli hakuishia hapo katika mradi wake mkubwa wa kufukarisha wafanyakazi. Ameingilia pia Mafao na Pensheni za wafanyakazi wastaafu, na kuzipiga.

Mbali ya kurithi madeni ya serikali, ambapo serikali ilikopa toka mashirika ya hifadhi za jamii, Magufuli badala ya kupunguza madeni hayo, ameyaongeza zaidi na zaidi.

Ili kuficha " uporaji" huu, serikali ya JPM imetumia njia kadhaa, hapa nitaje njia mbili: kwanza kuunganisha mashirika. Hapa kuna manufaa mengi kwa serikali. Kwanza kujipatia muda zaidi kwa kisingizio cha " mchakato", pili "uhakiki", na kuficha udhaifu wa mashirika yaliyokuwa hoi zaidi kutokana na uporaji huo wa serikali.

Pili ni kwa "kurekebisha" vikokotoo.

Matokeo yake, wafanyakazi wengi hivi sasa wanacheleweshewa mafao yao na Pensheni.

Miaka ya hivi karibuni kulikuwa na uboreshaji mkubwa katika utendaji wa mashirika ya hifadhi ya jamii, na kuwezesha wafanyakazi wanaostaafu kulipwa mafao yao mapema. Magufuli badala ya kuboresha zaidi alipoachia Kikwete, ndio amezidi kuvuruga zaidi.

Hapo juu nimetumia neno "UPORAJI" badala ya "UKOPAJI" kwa sababu, mstaafu halipwi pensheni ya kila mwezi, mpaka hapo atakapolipwa mafao yake. Hebu fikiria mtu katumikia miaka yote hiyo, anastaafu, hapati malipo yoyote mwezi baada ya mwezi. Kama atalipwa mafao baada ya miaka 2, maana yake muda wote huu hana kipato chochote. Kwa kuzingatia mstaafu ni mtu mwenye umri mkubwa, ana hatari ya magonjwa nyemelezi kibao, mateso kama haya hayawaachi salama baadhi yao wanafariki bila kupokea malipo yao. Na hata kama hajafariki, atakuwa ameathirika sana, yeye na wategemezi wake, kiasi hata akija kulipwa hayo mafao, kuna athari ambazo hazitawezekana kuponeshwa.
Hapo hakuna uporaji kweli?

Kwa hiyo JPM amewanyima wafanyakazi ile nafuu aliyowaahidi, badala ya kuwapa mkate akawapa UPUPU.

Pia hata kile kidogo kilichohifadhiwa kwa ajili yao wanapostaafu, amekipora pia.

Magufuli hakuishia hapo.
1) kwa mujibu wa sheria, mfanyakazi ana haki ya kupata nyongeza za kila mwaka (increments ) ambazo humwezesha kupanda ngazi za mshahara na madaraja. Miaka yote hii haijawahi kuingiliwa, inaweza kusimama kwa muda tu lakini si kwa kiwango cha wakati wa Magufuli. Katika awamu ya Magufuli, increment imegeuzwa kuwa hisani ya rais, na inatangazwa kwa mbwembwe. Hii ni enzi ya utumwa haswa.

2) Licha ya increments, kuna nyongeza za mishahara za jumla. Hizi Magufuli ndio kabisaaa kafutilia mbali. Hizi zilisaidia sana kuongeza kiwango cha mshahara kinachotumika kukokotoa malipo ya mafao. Ndio kimbilio pekee kwa wale wafanyakazi waliofika kwenye "bar".

3) Kuna kituko au tuseme UMAFIA umefanywa na serikali hii haijawahi kutokea. Mfanyakazi anapata barua ya kupandishwa daraja kwa mujibu wa taratibu. Maana yake mshahara pia unapanda. Tuseme anaambiwa kapandishwa kuanzia tarehe mosi Julai 2017. Baadae analetewa barua mshahara utapanda kuanzia Novemba mosi 2017. Baadae tena anaambiwa atalipwa kuanzia Julai Mosi 2018. Danadana hizo zinaweza kuendelezwa bila kikomo, kuna ambao mpaka leo hawajaonja mshahara mpya, kwa mtindo huo.

Ni wazi Magufuli ameona wafanyakazi ni Mgodi wa kuutumia kutekeleza miradi yake ili kujiletea sifa kubwa, kwa gharama ya wafanyakazi .

Tusisahau kwamba wafanyakazi ni chanzo kikubwa cha makusanyo ta kodi, tena cha uhakika. Serikali inajipigia panga yenyewe bila mjadala wala makadirio.

Tumesikia Rais Magufuli katika ziara hivi karibuni akiwajibu wafanyakazi , kama unaona mshahara hautoshi, nenda kalime. Siku chache Baadae akiongea na walimu, aliwaahidi kulipa mafao yao yote wanaodai, kufikia mwezi wa 8. Swali, hakuwajibu waende kulima. Je, hiyo ni kwa walimu tu? Au wafanyakazi wastaafu wote? Na kama ni walimu tu, kawatenga kwenye kundi la wanaoteswa, ili iweje? UCHAGUZI MKUU 2020?
 
Mkuu hapa utaambiwa umetumwa na mabeberu au ni wivu tu wa majirani zetu kenya.Ila hii nchi kuna muda inatia huruma sana yaani nikimuangalia mzazi wangu ni mfanyakazi wa serikali lkn maisha yake aisee unawezalia
 
Kingine kibaya zaidi,wakati hawajaboresha masilahi ya wafanyakazi,kaongeza makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asimilia 8 mpaka 15 huku akijua mishahara ni duni kabisa alafu majukwaani wanajitapa hii ni serikali ya wanyone!!

Ndio maana watu wengine huishiwa uvumilivu na kutumia lugha zisizofaa kuelezea machungu waliyonayo.
 
Akisemaga yeye ni mtetezi wa wanyonge wafanyakazi wanabadilisha Tv/radio fasta tu.

Wao wako kwny ma V8 na wanapiga mijengo ya hatari huku wakizuga bla bla bla za uzalendo uchwara huku wafanyakazi wanaumizwa,mafao mizinguo mitupu.

Na J2 utamuona Church akisema tumuombee.

Ajabu sana.
 
Mtu ukiamua kuacha kazi ufanye mambo yako, unaambiwa huwezi kuchukua mafao yako hadi ufikishe miaka 60. Yaani serikali inafunga ndoa ya lazima na watumishi.....kwa nini wasitoe ajira za mkataba angalau wa miaka 5, ili mtu aamue kuacha au kuendelea na utumishi baada ya miaka 5 na aruhusiwe kuchukua chake...
 
Kingine kibaya zaidi,wakati hawajaboresha masilahi ya wafanyakazi,kaongeza makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asimilia 8 mpaka 15 huku akijua mishahara ni duni kabisa alafu majukwaani wanajitapa hii ni serikali ya wanyone!!

Ndio maana watu wengine huishiwa uvumilivu na kutumia lugha zisizofaa kuelezea machungu waliyonayo.
Kusema kweli kama walioumizwa na serikali hii wangetoa ya moyoni....
 
Nawashangaa sana wanaomsifia MTU FURANI kwa kuleta maendeleo ya vitu,Sasa mtu amefukuza wafanyakazi anaowaita feki na kuwadhulumu mafao yao yote , mtu ambaye amezuia watu wasipate mafao pindi wakiacha kazi mpaka wafike miaka 50 , mtu ambaye hajawahi kupandisha mishahara hata sent 5 ya mjerumani unataka tumpongeze? Hivi unajua miradi mikubwa waliyoifanya WAKOLONI enzi za mwalimu? Miradi ya wakoloni hata 1/10 MTU FURANI haifikii na bado WAKOLONI tuliona hawafai.
 
Moja ya simulizi za kusikitisha katika utawala wa awamu ya Tano, ni kisa cha wafanyakazi wa Tanzania. Zipo kada nyingi zilizoumizwa sana na utawala huu, mojawapo nyingine ni wakulima. Hawa wote wametumika kama nyenzo tu ya kufanikisha miradi ya awamu hii, huku wao wenyewe na familia zao wakiachwa kwenye mateso na lindi la ufukara. Nachelea kusema kinachofanyika kinakaribia mfumo wa utumwa haswa.

John Joseph Pombe Magufuli, wakati anajinadi 2015, aliahidi, kati ya ahadi nyingi, kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Na baada ya bajeti yake ya kwanza, alitamka kwamba ataanza kuyaboresha "baada ya mwezi mmoja au miwili", akidai kwamba haiwezekani kuboresha maslahi kabla ya kukamilisha zoezi la kuhakiki WAFANYAKAZI HEWA. Hilo lilionekana ni busara iliyo wazi kabisa. Wafanyakazi wakavuta subira.

Kusema kweli uhakiki ulifanyika, watu walihakikiwa zaidivya mara 4, lakini mishahara haikupanda, ila bei mbalimbali na gharama za maisha, ziliendelea kupanda.

Miezi haigandi, ikasonga mbele, ukawa mwaka, na zaidi. Baada ya kuachana na kisingizio cha uhakiki wa wafanyakazi, Serikali ya JPM ikabuni kibwagizo kingine: maboresho ya wafanyakazi yapo ndani ya maboresho ya maisha ya watanzania wote. Barabara zinazojengwa, ujenzi wa reli ya SGR, mradi mkubwa wa umeme wa Stigler, fly over, ununuzi wa ndege, na mengine mengi.

JPM aliridhishwa sana na hoja hii, kiasi kwamba baada ya hapo, akisikia kilio cha kuboresha maslahi ya wafanyakazi, alikuwa anajibu kwa ukali: kama unaona mshahara hautoshi, nenda kalime! Hapo JPM aliridhika kabisa kwamba ametekeleza ahadi yake ya kuboresha maslahi yavwafanyakazi.

Na kwa kweli, kuna wakati aliahidi kwamba kabla ya kumaliza awamu hii ya miaka 5, atatekeleza ahadi yake. Mpaka hivi sasa keshavunja bunge, kwa hiyo keshawahadaa wafanyakazi kwa mara nyingine.

Inafaa kukumbuka kwamba kama mishahara ya wafanyakazi haiongezwi, basi maana yake vipato vyao vinashuka, kwa sababu gharama za maisha zimepanda sana kipindi cha Magufuli, ili kugharimia miradi mingi aliyoianzisha bila kuzingatia uwiano katika sera za uchumi. Kwa hiyo maana yake ni kwamba kiuhalisia, badala ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi, ameyadunisha kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni pamoja na maisha ya watanzania wote kwa ujumla wao, wamefukarishwa zaidi.

Lakini Magufuli hakuishia hapo katika mradi wake mkubwa wa kufukarisha wafanyakazi. Ameingilia pia Mafao na Pensheni za wafanyakazi wastaafu, na kuzipiga.

Mbali ya kurithi madeni ya serikali, ambapo serikali ilikopa toka mashirika ya hifadhi za jamii, Magufuli badala ya kupunguza madeni hayo, ameyaongeza zaidi na zaidi.

Ili kuficha " uporaji" huu, serikali ya JPM imetumia njia kadhaa, hapa nitaje njia mbili: kwanza kuunganisha mashirika. Hapa kuna manufaa mengi kwa serikali. Kwanza kujipatia muda zaidi kwa kisingizio cha " mchakato", pili "uhakiki", na kuficha udhaifu wa mashirika yaliyokuwa hoi zaidi kutokana na uporaji huo wa serikali.

Pili ni kwa "kurekebisha" vikokotoo.

Matokeo yake, wafanyakazi wengi hivi sasa wanacheleweshewa mafao yao na Pensheni.

Miaka ya hivi karibuni kulikuwa na uboreshaji mkubwa katika utendaji wa mashirika ya hifadhi ya jamii, na kuwezesha wafanyakazi wanaostaafu kulipwa mafao yao mapema. Magufuli badala ya kuboresha zaidi alipoachia Kikwete, ndio amezidi kuvuruga zaidi.

Hapo juu nimetumia neno "UPORAJI" badala ya "UKOPAJI" kwa sababu, mstaafu halipwi pensheni ya kila mwezi, mpaka hapo atakapolipwa mafao yake. Hebu fikiria mtu katumikia miaka yote hiyo, anastaafu, hapati malipo yoyote mwezi baada ya mwezi. Kama atalipwa mafao baada ya miaka 2, maana yake muda wote huu hana kipato chochote. Kwa kuzingatia mstaafu ni mtu mwenye umri mkubwa, ana hatari ya magonjwa nyemelezi kibao, mateso kama haya hayawaachi salama baadhi yao wanafariki bila kupokea malipo yao. Na hata kama hajafariki, atakuwa ameathirika sana, yeye na wategemezi wake, kiasi hata akija kulipwa hayo mafao, kuna athari ambazo hazitawezekana kuponeshwa.
Hapo hakuna uporaji kweli?

Kwa hiyo JPM amewanyima wafanyakazi ile nafuu aliyowaahidi, badala ya kuwapa mkate akawapa UPUPU.

Pia hata kile kidogo kilichohifadhiwa kwa ajili yao wanapostaafu, amekipora pia.

Magufuli hakuishia hapo.
1) kwa mujibu wa sheria, mfanyakazi ana haki ya kupata nyongeza za kila mwaka (increments ) ambazo humwezesha kupanda ngazi za mshahara na madaraja. Miaka yote hii haijawahi kuingiliwa, inaweza kusimama kwa muda tu lakini si kwa kiwango cha wakati wa Magufuli. Katika awamu ya Magufuli, increment imegeuzwa kuwa hisani ya rais, na inatangazwa kwa mbwembwe. Hii ni enzi ya utumwa haswa.

2) Licha ya increments, kuna nyongeza za mishahara za jumla. Hizi Magufuli ndio kabisaaa kafutilia mbali. Hizi zilisaidia sana kuongeza kiwango cha mshahara kinachotumika kukokotoa malipo ya mafao. Ndio kimbilio pekee kwa wale wafanyakazi waliofika kwenye "bar".

3) Kuna kituko au tuseme UMAFIA umefanywa na serikali hii haijawahi kutokea. Mfanyakazi anapata barua ya kupandishwa daraja kwa mujibu wa taratibu. Maana yake mshahara pia unapanda. Tuseme anaambiwa kapandishwa kuanzia tarehe mosi Julai 2017. Baadae analetewa barua mshahara utapanda kuanzia Novemba mosi 2017. Baadae tena anaambiwa atalipwa kuanzia Julai Mosi 2018. Danadana hizo zinaweza kuendelezwa bila kikomo, kuna ambao mpaka leo hawajaonja mshahara mpya, kwa mtindo huo.

Ni wazi Magufuli ameona wafanyakazi ni Mgodi wa kuutumia kutekeleza miradi yake ili kujiletea sifa kubwa, kwa gharama ya wafanyakazi .

Tusisahau kwamba wafanyakazi ni chanzo kikubwa cha makusanyo ta kodi, tena cha uhakika. Serikali inajipigia panga yenyewe bila mjadala wala makadirio.

Tumesikia Rais Magufuli katika ziara hivi karibuni akiwajibu wafanyakazi , kama unaona mshahara hautoshi, nenda kalime. Siku chache Baadae akiongea na walimu, aliwaahidi kulipa mafao yao yote wanaodai, kufikia mwezi wa 8. Swali, hakuwajibu waende kulima. Je, hiyo ni kwa walimu tu? Au wafanyakazi wastaafu wote? Na kama ni walimu tu, kawatenga kwenye kundi la wanaoteswa, ili iweje? UCHAGUZI MKUU 2020?

Update:
Kuna ubunifu mwingine. Kuna Sekula imetoka hivi karibuni. Mwanzoni mfanyakazi alitakiwa awe amechangia kwa miaka kumi katika shirika la Bima ya Afya (NHIF) ili apatiwe kadi ya kudumu yeye na mkewe baada ya kustaafu.

Sasa Sekula inasema kwamba ili apatiwe kadi ya bima yeye na mkewe, anatakiwa awe amechangia miaka 15! Maana yake kama mtu anastaafu na amechangia kwa miaja 10, anatakiwa kulipa fedha taslimu kufidia miaka 5. Hapo unaongelea karibu sh. Milioni 10.

Huu ni ubunifu mzuri sana kwa sababu serikali itapunguza sana kiwango cha kumlipa mafao mfanyakazi. Serikali itakuwa imepiga panga la sh. Milioni 10.

Angalau wangeongeza miaka2. Miaka 5 inaongezwa kwa mpigo? Huyo ndio rais wa kutengeneza wanyonge waongezeke zaidi na zaidi
Hii habari ya sekula mpya bora ungeianzishia mada yake ya kujitegemea maana hili ni jambo kubwa na jipya na wengine ndio kwanza tunalisikia kupitia kwako.
 
Back
Top Bottom