McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 914
- 2,929
Wakuu,
Tundu akiwasili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam ambapo leo kesi ya uhaini inayomkabili itaendelea
Dada wa Mhe. Tundu Lissu akiwasili Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili mdogo ake
====================================================================
Soma Pia:
Jana tuliishia Part 191 so leo tunaendelea na-;
Part 192
Kesi inaanza muda huu Majaji na Mshitakiwa wamefika.
Mawakili wa Serikali pia wapo tayari.
Hali ya hewa ilikuwa ya mvua kwahiyo mahudhurio sio makubwa ya watu hapa Mahakamani.
Tupo hapa kuwaletea updates kama kawaida.
Anasimama Renatus Mkude anasema wanae shahidi mmoja lakini shahidi mwingine anayefuata amefiwa na Mkwe wake kwahiyo leo tunae shahidi mmoja.
Anasimama Lissu anasema kama amepata msiba ni wazi hawezi akaja.
Mimi niko tayari kuendelea na shahidi aliyepo lakini tulikubaliana angalau waje mashahidi watatu kwa siku.
Nasema hayo sio kwasababu sitaki watu waende msibani ila nasema ili tujue ni muhimu tukatumia muda vizuri ili wasio kwenda msibani tubaki nao kufanya kesi.
Anasimama Renatus Mkude anasema hili ni jambo la kibinadamu tunaomba na sisi mawakili wa serikali twende pale kumcomfort mwenzetu.
Jaji Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Tundu Lissu sijawahi kuwa na roho mbaya kiwango hicho kukataza watu wasiende msibani, kama wao wameona kuna umuhimu huo wa kwenda.
Jaji anasema basi tuendelee.
Renatus anasema shahidi tuliyenae ni P7 na ataongozwa na Thawabu Issa Wakili wa Serikali.
Jaji anauliza una miaka mingapi?
26 ninayo.
Dini yako?
Mkristo.
Anaapishwa hapa Shahidi.
Wakili wa Serikali Thawabu Issa anaanza kumuhoji shahidi hapa.
Wakili: unajishughulisha na nini?
Shahidi wa kificho P7 : Dereva bajaji nafanyia kwa Morombo kule Arusha toka 2023 nafanya kazi hiyo.
Wakili: Hapo kwa morombo pakoje?
Shahidi wa kificho : Kuna watu wengi sana. Kuna maduka na watu wanafanya biashara hapo. Ikiwemo maduka ya mahitaji ya nyumbani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kuna nini kilitokea?
Shahidi wa kificho : hiyo tarehe majira ya jioni nilikuwa kijiwe cha kwa morombo Arusha. Tulikuwa hapo kijiweni na tunafanya mazungumzo ya kawaida.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho : Kuna mwenzetu akasema hamjasikia Chadema wamesema watazuia Uchaguzi wa Mwaka huu. Wamesema watakinukisha mbaya. Alikuwa anatuelezea huyo mtu.
Wakili: kingine ni nini?
Shahidi wa kificho : Akasema kuwa Polisi wanaiba kura hata ukienda Mahakamani hautapata haki.
Wakili: Kikaendelea baada ya mtu huyo kusema?
Shahidi wa kificho : Akasema pia Majaji ni vibaraka wa CCM, akasema pia mwaka 2024 tume ya Uchaguzi ilipewa maelekezo ya kukata wajumbe wa Chadema. Tukiwa tunaendelea na hayo mazungumzo nilipata hamasa kupitia hayo maneno niliyosikia akisema yule Bajaji mwenzangu.
Wakili: Sasa weka vizuri, wewe ulifanya nini?
Shahidi wa kificho : Niliingia kwenye mtandao wa youtube na mimi niweze kujionea hayo maneno. Nilitumia simu yangu na kuingia channel inaitwa Jambo. Simu ya janja.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho : Nikafungua channel ya Jambo na kukuta yale maneno kama nilivyoambiwa hapo kijiweni.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho : Baada ya dakika chache kuna watu wakaja wakajitambulisha kama wao ni maaskari na baadae watu walikimbia tukakamatwa mimi na P4.
Wakili: kilichoendelea hapo?
Shahidi wa kificho : Tukapelekwa kituo cha Polisi Murieti. Tulikaa kama Dakika 45 tukapelekwa kituo cha Polisi Central Mjini.
Wakili: baada ya kuwa umepelekwa Central ikawaje?
Shahidi wa kificho : Tukaingizwa Ofisi ya RCO nikaambiwa nashitakiwa kwa kosa la kutaka kufanya fujo, niliandikwa maelezo na kuingizwa Mahabusu na asubuhi yake ndugu zangu walinifuata nikazaminiwa na kupewa tarehe za kuwa naenda kuripoti kwenye hicho kituo cha Polisi.
Wakili: Nini kilifuata?
Shahidi wa kificho : Nikawa naripoti kwa mujibu mpangilio wa hiyo ratiba na ilipofika Tar. 17/04 2025 baada ya kufika kuripoti kama kawaida, nikaambiwa naandikwa maelezo upya.
================
Part 193
Wakili wa Serikali; ikawaje?
Shahidi wa kificho : Nikaandika maelezo haya niliyoyatoa Mahakamani.
Wakili wa Serikali anasema Mheshimiwa Jaji Mwisho wa Mahojiano na Shahidi. Tuko tayari kwa Maswali ya Dodoso.
Anasimama Mhe. Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Unanisikia?
Shahidi wa kificho P7 : Vizuri sana.
Mhe. Lissu: we ni mzaliwa wa kiranyi?
Shahidi wa kificho P7: Ndio
Mhe. Lissu: Unapandia Sakina juu kama unaenda kwa Mzee Disouza Wakili?
Shahidi wa kificho P7: kimya
Mhe. Lissu: Unanisikia shahidi?
Shahidi wa kificho P7 : siwezi kuwa nawajua watu wote
Mhe. Lissu: Ila unapandia Sakina pale?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio
Mhe. Lissu: Sasa sitakufuata huko ila nilivyoona kiranyi nikakumbuka nimefanya kazi na Mzee Disouza huko.
Shahidi wa kificho P7 : Sawa.
Mhe. Lissu: Sina shida na wewe unajua hilo? Sipigi watu.
Shahidi wa kificho P7 : Hata mimi sikuogopi.
Mhe. Lissu: Mbona umejificha huko kwenye kibox kama huniogopi?
Shahidi wa kificho P7: Ndio hivyo sasa
Mhe. Lissu: Sasa tuanze na ushahidi ambao uliandika maelezo kuhusu tuhuma za wewe kufanya kosa la kutaka kufanya fujo?
Shahidi wa kificho P7 : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya kosa hilo yako wapi?
Shahidi wa kificho P7 : maelezo niliyoandika tarehe 03/04 ndio hayo hayo niliandika tarehe 17/04.
Mhe. Lissu: Uliandika au hukuandika tarehe 03/04
Shahidi wa kificho P7 : niliandika kweli
Mhe. Lissu: yako wapi?
Shahidi wa kificho P7 : Waulize maaskari
Mhe. Lissu: Wewe ni mjanja nenda kawaulize hao maaskari wako, Leo nitashinda hapa na wewe.
Tarehe 17/04 ukioneshwa hayo maelezo utayatambua?
Shahidi wa kificho P7 : Nitayatambua.
Mhe. Lissu: Naomba aonyeshwe maelezo yake tafadhali. Wanamtafutia na kumpatia.
Shahidi wa kificho P7 : Ndio haya maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Umeyapata?
Shahidi wa kificho P7 : nayapitia
Mhe. Lissu: Yapitie halafu wambie majaji kama ndio yako?
Shahidi wa kificho P7 : ndio yenyewe.
Mhe. Lissu: Naomba nimsomeee maneno yake na nitamuonesha maeneo ninayotaka kumkanusha na baadae kuomba ayatoe kama ushahidi.
Anaanza kumsomea hapa.
Amemaliza anamuuliza je maelezo haya yako sawa na uliyonayo?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio yako sawa
Mhe. Lissu: Sasa nakuoensha maeneo nitakayokukanusha.
1. Kuhusu kwa Morombo kuwa na watu wengi
2. Tar. 03/04 kuna mtu mmoja alianza
kusema habari za Lissu na Chadema.
3. Watakinukisha Mbaya
4. Polisi wanaiba kura hata ukienda
Mahakamani hutapata haki.
5. Kuhusu wewe kupata hamasa.
6. Uliingia kwa kutumia simu.
Anamsomea hayo maeneo mengi kidogo atakayomuhoji.
Mhe. Lissu: Je ungependa maelezo yako yapokelewe kama kielelezo cha ushahidi?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio.
Jaji upande wa Mashitaka mnasemaje?
Wakili Renatus: Hatuna pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi kitakuwa kielelezo D10 kwa Upande wa Mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Naomba sasa shahidi apatiwe kielelezo D10.
Mhe. Lissu: Umeieleza Mahakama kuwa pale kijiweni kuna watu wengi ikiwemo madereva bajaji na wenye maduka ya vitu vya nyumbani
Shahidi wa kificho P7 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa tuoneshe kwenye hicho kielelezo hayo maneno yapo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: tar. 03/04 mlikuwa mnazungumza mazungumzo ya kawaida na kuna mtu akaibua mazungumzo mengine kuhusu Chadema kuzuia Uchaguzi.
Shahidi wa kificho P7 : ndio
Mhe. Lissu: haya nioneshe yapo wapi?
Shahidi wa kificho P7 : hapa imesema alianzisha lakini mtu yani
Mhe. Lissu: Maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Tena watakinukisha mbaya. Yapo au hayapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P7 : Watakinukisha.
Mhe. Lissu: swali langu umesema hayo maneno yalisemwa na mtu mmoja?
Shahidi wa kificho P7 : Hapana.
Mhe. Lissu: Ahsante. Sasa umesema pia huyo mtu mmoja akasema Polisi wanaiba kura hata ukienda mahakamani majaji ni vibaraka wa CCM.
=============
Part 194
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination P7 ambae ni shahidi wa kificho.
Shahidi wa kificho P7 : Ni kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama hayo maneno kuhusu majaji yapo?
Shahidi wa kificho P7 : hayapo.
Mhe. Lissu: Je kwenye maelezo yako polisi uliandika kuhusu polisi nao kuiba kura
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Je umetaja tume ya uchaguzi hata mara moja kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi wa kificho P7 : Sijataja.
Mhe. Lissu: Je kwenye maelezo yako umetaja uchaguzi wa mwaka 2024 hata mara moja?
Shahidi wa kificho P7 : Hamna.
Mhe. Lissu: Ulisahau ulichoandika polisi?
Shahidi wa kificho P7 : Nilikuwa naandika maelezo sio kitabu.
Mhe. Lissu: Umesema tukiwa tunaendelea na mabishano nilipata hamasa sasa hayo maneno kuwa ulipata hamasa kama yapo kwenye maelezo yako Polisi.
Shahidi wa kificho P7 : hayapo.
Mhe. Lissu: Unasema uliingia youtube kwa kutumia simu janja. Yako wapi kwenye maelezo yako ya polisi hayo nayo?
Shahidi wa kificho P7 : Niliingia youtube maana yake nilikuwa na simu
Mhe. Lissu: huwezi kuingia kwa kutumia Computer?
Shahidi wa kificho P7 : Mimi sina Computer
Mhe. Lissu: Sasa ndio ujibu swali langu kuwa ulisema uliingia kwa kutumia simu?
Shahidi wa kificho P7 : Sijataja.
Mhe. Lissu: Umesema uliingia kupitia Channel ya Jambo sasa tuoneshe hayo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: unasema ulishitakiwa kwa kufanya fujo. Tuoneshe hilo nalo kama lipo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Umesema ulipata dhamana asubuhi.
Shahidi wa kificho P7 : Naomba nirudie.
Mhe. Lissu: Hiyo kurudia utarudia ukiwa unasimulia ndugu zako wa Kiranyi.
Shahidi wa kificho P7 : Sawa
Mhe. Lissu: Swali langu waeleze Majaji kama hayo maneno ulidhaminiwa asubuhi yapo kwenye karatasi yako ya maelezo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako ya Polisi uliandika kuwa una account ya Youtube?
Shahidi wa kificho P7 : Sikusema.
Mhe. Lissu: Umesema mlisisitiziana kuunga mkono maneno ya Lissu.
Shahidi wa kificho P7 : Kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama kusisitiziana kuunga mkono kauli za Lissu ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi.
Shahidi wa kificho P7 : mimi sijui kwasababu sio mwanasheria.
Mhe. Lissu: Mnasisitiziana kuunga mkono kauli zangu za kuzuia uchaguzi. Nauliza kufanya hivyo ni kosa?
Shahidi wa kificho P7 : Ni kosa ndio maana tukakamatwa.
Mhe. Lissu: Je ulipelekwa Mahakamani kwa lile kosa na kufanya fujo?
Shahidi wa kificho P7 : Hapana.
Mhe. Lissu: Baada ya kukuchukua maelezo tarehe 03/04 je walihangaika tena na wewe kwa hilo kosa la kufanya fujo.
Shahidi wa kificho P7 : walisema niwe naripoti
Mhe. Lissu: Walikuwa wanakwambia nini?
Shahidi wa kificho P7 : Nafyagia nje nasign halafu naondoka.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hawakukwambia lolote zaidi ya kukufanyisha kazi?
Shahidi wa kificho P7 : ndio maana nimefika hapa. Wewe ndio umenisababishia.
Mhe. Lissu: Tar. 17/04 tukaambiwa tusubiri kwani tunatakiwa tuhojiwe tena.
Shahidi wa kificho P7 : Kweli.
Mhe. Lissu: Kwanini walikwambia wakuhoji mara nyingine tena?
Shahidi wa kificho P7 : Sijui
Mhe. Lissu: Walikwambia wanakuhoji kwa ajili ya kesi hii ya kwangu?
Shahidi wa kificho P7 : Hapana hawakuniambia.
Mhe. Lissu: Kwahiyo maelezo yako yalitokana na mahojiano na Polisi?
Shahidi wa kificho P7 : Ndio.
Mhe. Lissu: Umekujaje Mahakamani leo?
Shahidi wa kificho P7 : kwa miguu
Mhe. Lissu: Toka kiranyi?
Shahidi wa kificho P7 : Kwa Basi.
Mhe. Lissu: Nani alikupa nauli?
Shahidi wa kificho P7 : Mwanamke wangu.
Mhe. Lissu: Nani anayekuweka mjini hapa?
Shahidi wa kificho P7 : Mwanamke wangu.
Mhe. Lissu: Je tangu walipoandika maelezo yako Polisi tarehe 17/04 mmekuwa mnawasiliana na Mapolisi
Shahidi wa kificho P7 : Hatujawahi kuwasiliana tena.
======================
Part 195
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi
Mhe. Lissu: Kwanini umepewa Jina la P7?
Shahidi wa kificho P7 : Kwasababu ya usalama wangu.
Mhe. Lissu: Si umesema hakuna aliyekutishia.
Shahidi wa kificho P7 : Ndio hivyo sasa.
Mhe. Lissu: Sina Maswali mengine.
Jaji: Karibu upande wa Serikali kwa Re Examination.
Wakili wa Serikali: Hatuna maswali kwa shahidi huyu.
Upande wa Serikali walisema wana shahidi mmoja tu kwahiyo kesi itaendelea kesho saa tatu asubuhi bila shaka.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Wakili wa Serikali: Renatus Mkude anasimama anasema kama tulivyosema asubuhi naomba tuahirishe hadi kesho asubuhi.
Jaji: Tafadhali tukutane hiyo Kesho Tarehe 19 saa tatu asubuhi.
Inapigwa high court
Watu wote tunasimama,
Majaji wanaondoka,
Watu wanaanza kutawanyika.
Tundu akiwasili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam ambapo leo kesi ya uhaini inayomkabili itaendelea
====================================================================
Leo February 18, 2026Jana tuliishia Part 191 so leo tunaendelea na-;