Mbona Bunge limevurugika?

Mbona Bunge limevurugika?

Wengi waliingia hapo kwa ajili ya JPM ili kufanya kazi maalumu za JPM ..... Sasa si unajua tena Mchungaji akiondoka nini kitatokea kwa Kondoo .........!!
 
Aliyewaweka pale kashaondoka sasa hawajui wafanye nini!
 
Si siri tena, sasa hivi kunaonekana mpasuko mkubwa ndani ya bunge kiasi inakuwa aibu kuangalia na watu inakuwa kama tunaangalia mpira na makelele ya kushangilia.

Ni kwanini bunge letu linakosa heshima na limekaa kiumbea umbea kiudaku udaku kusutana sutana, halipo kiufundi lenye kujielewa, yaani ukisikiliza inafikia wakati hujui ucheke au ulie halina tofauti na mastori ya kijiweni, yaani unajikuta hivi hivi upo na mastori ya kijiweni mmekaa pamoja.

Naanza kuamini kama nchi yetu na watu wake ni wa ajabu ajabu.
Ni kwa vile kuna COVID-19 humo. Nasikia hao wote ni virusi jike!!
 
si tuliambiwaga wapinzani ndo wanavurugu bungeni au
 
Si siri tena, sasa hivi kunaonekana mpasuko mkubwa ndani ya bunge kiasi inakuwa aibu kuangalia na watu inakuwa kama tunaangalia mpira na makelele ya kushangilia.

Ni kwanini bunge letu linakosa heshima na limekaa kiumbea umbea kiudaku udaku kusutana sutana, halipo kiufundi lenye kujielewa, yaani ukisikiliza inafikia wakati hujui ucheke au ulie halina tofauti na mastori ya kijiweni, yaani unajikuta hivi hivi upo na mastori ya kijiweni mmekaa pamoja.

Naanza kuamini kama nchi yetu na watu wake ni wa ajabu ajabu.
Uhovyo wa bunge unatokana na uhovyo wa kiongozi wa bunge
 
Lazima uone hilo maana hata ingia yao humo ilikuwa ya kimashaka tupu!
Hapo umepiga nyoka kichwani. Manaa wameingia bungeni bila malengo, matokeo yake ndio hayo, wapoga kelele badala ya kujenga nchi.
 
Nadhani ni Dr. Slaa alisema siku moja bunge la sawasawa watu huwa wanapigana ngumi. Nakumbuka Kenya kuna mbunge Mmasai siku moja alimshambulia mwenzake kwa rungu. Alipoulizwa kwa nini alisema he was "driving home his point". Wengi hapa hamjaona mabunge mengi yalivyo. Sio Kanisani wala Msikitini kule.

Sasa nina hakika kuna wengi mmekasirika bila hata kujua kuna nini kilitokea. Hivi kimetokea nini? Kama ni kelele basi pale ndiyo kazi yake.

Hata mie nakasirika kwani wale si wawakilishi wa wananchi. Hata Mama mwenyewe alisema mpige kura vyovyote mtakavyo lakini serikali wataunda wao.

Matters must come to a head at some point. Then we will have the courage to demand, not request, for our own constitution. Hii ya kubambikiziwa na wezi na wanyanganyi wa chama kimoja haitatufaa. Ipo siku tutadai kama walivyodai Kenya na tupate katiba yetu. Then, and only then, bunge letu litakuwa na maana. Kwa sasa sio chochote wala lolote, ni sehemu tu ya wanyonyaji wetu wakubwa.
 
Back
Top Bottom