Mbona Bunge limevurugika?

Mbona Bunge limevurugika?

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,179
Si siri tena, sasa hivi kunaonekana mpasuko mkubwa ndani ya bunge kiasi inakuwa aibu kuangalia na watu inakuwa kama tunaangalia mpira na makelele ya kushangilia.

Ni kwanini bunge letu linakosa heshima na limekaa kiumbea umbea kiudaku udaku kusutana sutana, halipo kiufundi lenye kujielewa, yaani ukisikiliza inafikia wakati hujui ucheke au ulie halina tofauti na mastori ya kijiweni, yaani unajikuta hivi hivi upo na mastori ya kijiweni mmekaa pamoja.

Naanza kuamini kama nchi yetu na watu wake ni wa ajabu ajabu.
 
"Atake asitake alazimishweeeeeee "
JamiiForums-470442358.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
😅😅😅


Mumetaka kusikia live.. munapewa munalalamika.. tunahitaji maombi ya nchi nzima.. kuombea banapenda kulalama..

..kazi iendeleeeeeee
 
Si siri tena ,sasa hivi kunaonekana mpasuko mkubwa ndani ya bunge kiasi inakuwa aibu kuangalia na watu inakuwa kama tunaangalia mpira na makelele ya kushangilia.
Ni kwanini bunge letu linakosa heshima na limekaa kiumbea umbea kiudaku udaku kusutana sutana,, halipo kiufundi lenye kujielewa,yaani ukisikiliza inafikia wakati hujui ucheke au ulie halina tofauti na mastori ya kijiweni ,yaani unajikuta hivi hivi upo na mastori ya kijiweni mmekaa pamoja. Naanza kuamini kama nchi yetu na watu wake ni wa ajabu ajabu.
Hilo ndilo Bunge aliloliteua marehemu. Wote waliomo humo ni kwa matakwa ya marehemu. Hakuna anayeweza kusimama kwa ujasiri na kusema kuwa amepelekwa huko bungeni na wapiga kura.
 
Back
Top Bottom