Mbio za ubunge Igunga Dkt. Slaa, Zitto kuzindua kampeni; CHADEMA kutumia helikopta Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio za ubunge Igunga Dkt. Slaa, Zitto kuzindua kampeni; CHADEMA kutumia helikopta Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  *CHADEMA kutumia helikopta Igunga
  *Yaanika mikakati ya kushinda jimbo
  *CCM yavuta pumzi, yasubiri CC


  Na Benjamin Masese

  VUGUVUGU la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora linazidi kupanda
  huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitangaza safu ya viongozi wa kitaifa watakaozindua kampeni za chama hicho Septemba 9, mwaka huu.

  Mbali na kuanika majina ya viongozi wake watakaozindua kampeni, chama hicho kina mkakati wa kutumia helikopta ili kufikia maeneo yote ya Jimbo la Igunga.

  "Kama kawaida yetu tayari helikopta imeandaliwa kwa mashambulizi ya kampeni jimbo la Igunga, lakini hatutaanza nayo, tutaanza na vyombo vya ardhini kwanza tukiona kuna ulazima, ndipo tutakaponyanyuka juu kwa juu na kumwaga sumu 'chini'."

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga. Alisema viongozi wa kitaifa watakaohudhuria uzinduzi wa kampeni za chama hicho ni Katibu Mkuu, Dkt. Willbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Bw.Zitto Kabwe.

  Bw. Tumbo alisema kuwa tayari Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana juzi na kupitia majina ya wagombea 16 waliochukua fomu, ambapo kwa kuzingatia sifa na mtu mwenyewe anavyokubalika kwa wananchi wa Igunga, ilimpitisha Bw.Joseph Kashindye, kuwania kiti hicho.

  "Hapa tulipo hatujaanza kampeni, lakini wananchi wameonesha shauku kubwa ya kukiunga mkono chama chetu ili kuwaongoza, kwani wamedai kwamba kwa miaka mingi walikuwa hawajapata kiongozi wa kukaa nao na kujadiliana wanachohitaji," alisema Bw. Tumbo.

  Alisema baada ya uzinduzi huo viongozi wa kitaifa watasambaa maeneo yote ya jimbo hilo kumnadi mgombea Bw. Kashindye, ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoke mikononi wa CCM).

  Alisema utafiti wa awali umeonesha kuwa CHADEMA itaibuka na ushindi kwa zaidi ya asilimia 80, huku vyama vingine vikigawana asilimia zilizobaki.

  Alisema CCM ina hali mbaya kuliko vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo. Alisema dalili zinaonesha kuwa wananchi wamechoka na sera za chama hicho.

  "Hadi sasa tunajua tunashinda na harakati za kumwaandaa mgombea wetu kwenda bungeni zimeanza na tutampeleka kwa maandamano hadi Dodoma na kufanya hafla fupi ya kumkaribisha,"alisema.

  Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, CCM Bw. Nape Nnauye, alisema muda wowote kuanzia sasa Kamati Kuu itakutana kumteua mgombea wa chama hicho na kutangaza siku ya kuanza kampeni.

  Akizungumza na gazeti hili jana,Bw. Nnauye alisema kauli za CHADEMA kujihakikishia ushindi ni mbinu za kuwatisha watu na wagombea wengine, lakini CCM inazichukulia kama kelele ambazo zimezoeleka kwao.

  "Hakuna chama ambacho kinatangaza mikakati yake barabarani,tunatarajia Kamati Kuu itakaa muda wowote kumpitisha mgombea mmoja na kutangaza siku rasmi ya uzinduzi wa kampeni, wao ndio wanasuasua sisi tuko imara na ushindi ni wetu kama kawaida,"alisema.

  Awali alisema CCM ina asilimia 90 za ushindi katika jimbo hilo na kuongeza kwamba kampeni za chini chini za baadhi ya vyama vya siasa zilizoanza Igunga ni mchezo wa watoto wadogo.

  "Pale Igunga, CHADEMA haina kitu hata kama wameanza kampeni za chini chini...ule ni mchezo wa watoto na kawaida ikifika saa sita usiku lazima watoto walale na ndipo tutakaposhinda. Pia tathmini tulishafanya na tumebaini zaidi ya asilimia 90 tunashinda ndio maana hatuna wasiwasi,"alisema.

  Naye Rachel Balama anaripoti kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajia kutangaza ratiba na mikakati mingine leo.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius Mtatiro, alisema;

  "Nipo Igunga kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, lakini kesho nitatoa taarifa zote kuhusu kampeni za CUF."

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha National Reconstruction Alliance(NRA) Bw. Rashid Mtuta, alisema kuwa chama chake kina nia ya kusimamisha mgombea na kinasubiri timu iliyotumwa Igunga kuangalia mazingira ya kukubalika kwake jimboni humo.

  Alisema tayari timu hiyo ya watu watano ipo kwa wiki moja sasa na inatarajia kurudi wakati wowote kuanzia leo.

  "Tunapozungumza tayari timu ya watu watano ipo Igunga kuangalia mazingira na tutatoa tamko," alisema Bw. Mtuta.

  Alisema kuwa timu hiyo inaonngozwa na Kaimu Katibu Mkuu Taifa Bw. Hassan Kisabya.
   
 2. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hivi nape atakanyaga igunga? naskia amepigwa marufuku asitie pua. viva chademaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
 3. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kawaida ya CCM huwa ni wagumu kuelewa kwani ni watu wa kuchukulia mambo kimzaa mzaa na badae ujikuta wakiumbuka lakini nawahasa wananchi wa igunga wasichague chama wachague sera.
   
 4. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "
  "

  Wajameni , CHADEMA nao wana mbwembwe!
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145

  Hizo ni mbinu za kivita.
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  VITA VYA DR SLAA NA CHADEMA KUFUNGIA NDANI GWIJI LA UFISADI NCHI PALE IGUNGA NI SAWA TU NA JINSI PEOPLE'S POWER ILIVYOMFUNGIA NDANI DIKTETA GADDAFI KULE TRIPOLI NCHINI LIBYA

  Dokta wa Ukweli, kazi ya Igunga tunaomba iwe ni FULL-TIME kusudi tukifanikiwa KUNG'OA KIZIKI CHA UFISADI nchini kilichojichimbia kwenye ardhi yenye rutuba nyingi pale Igunga na basi baada ya hapo vita vikasambaa kote nchini hapo ndipo Mtanzania wa hali ya chini atakapoweza kupata ahueni.

  Makamanda wooote CHADEMA vita mbeeele kwambele Igunga mpaka kielewke lakini kwa kushirikiana kambi zima ya upinzani nchini. Kifo Cha CCM kitatangaziwa rasmi pale Igunga hata kabla ya mawaziri kibao na makada wa CCM wasioridhika na utawala wa sasa kuamua kujiengua mmoja baada ya mwingine!!!!!!!!!!!!

  Na endapo kukifanyika kosa lolote la NEC-Jaji Makame kufanya yale madudu ya mwaka jana kule Igunga basi hapo ndipo nako watakua wamerahishisha PEOPLE'S POWER kuingia mitaaani na kukatisha uhai wa hii serikali fisadi na dhalimu tuliyo nayo hivi sasa.

  Chaguo ni lao NEC pamoja CCM chenyewe hapa; ama kunyoa au kusuka!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. U

  UNMAFISADI New Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  ni kweli mkubwa, hawa watu huwa hawaelewi. itakuwa ni kama mkwala wa gaddafi na hatma itafikaaaa, PEEEEPOOZ POWEEEERRRR!..
   
 8. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tambo ni nyingi sana,ngoja tuone.
   
 9. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Kilalakheri CHADEMA, tupo pamoja nanyi katika mabadiliko ya kweli
   
 10. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Nawatakieni kila la heri katika kufanikisha juhudi za kulikomboa jimbo la IGUNGA. Tuko pamoja waungwana
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  matokeo atayasubiria dar. Chadema...... vema
   
 12. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nape Acha longolongo, njoo igunga tuchuane
   
 13. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Safi makamanda tupo nyumayenu
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mimi ng mwanachama wa CDM na naomba chama changu kishinde Igunga. Hata ivo nachelea kujiuliza maswali ambayo viongozi wangu wana majibu. Is J. Kashindye the best contesant and shall make the best MP for Igunga? Je, tunakumbuka kwamba majority ya majimbo tuliyopoteza mwaka jana ni kwa sababu hatukuwa na wagombea wenye uwezo? To what extent have we ensured kwamba uchaguzi wowote ujao tunakuwa na best wagombea? Ni ukwel ulio waz kuwa CDM imeweza kuwavutia wapiga kura wengi, lakini sio wapigiwa kura wengi. Kwa tulio huku mtaani tunajua kwamba wagombea wengi wa Cdm mwaka jana walipewa hiyo chance kwa sababu ndio waliojitokeza, na katika majimbo kadhaa hakutokea mtu ndo maana hatukuwa na wagombea. wapiga kura wanashawishiwa lakin wagombea bora wanakuwa groomed, mbowe, slaa, zito mnajua hilo. Tujiulize kama Mwl Kashindye na Dr Kafumu wangekuwa wote CDM, je bado mgombea wetu angekuwa Kashindye? Kam
   
 15. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Hapa watapasuka vichwa tu. Peaplesss....... powerrrrrrr........
   
 16. only83

  only83 JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ..................Wafuatao wameambiwa hawatakiwi Igunga kamwe............na wakitia pua zao ni halali kwa wakazi wa Igunga.........nao ni:

  1. Nape Nnauye
  2. Kapteni chiligati
  Hawa wakionekana kule watakiona chamoto......................haaaa maskini katibu mwenezi Napeeeeeeeee
   
 17. p

  politiki JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  pointi yako ni ngumu kuielewa kwa maana unasema wagombea hawakuwa wazuri, je kama hao ndio waliojitokeza kugombea ni lazima wapewe nafasi na hao wazuri unaowajua hawakujitokeza kwahiyo uzuri wao hauwezi kutusaidia kitu. kuhusu kafumu na kashindye obvious the answer ni kashindye kwa record yake kabambe ya kupigania maslahi ya waalimu na uzuri wa mwakilishi siyo elimu tu bali ni ukaribu wake na wananchi, uadilifu na record yake ya utumishi. DR.Kafumu anajua uchafu, uovu na wizi wa CCM ameamua kukaa kimya hatujawahi kumsikia hata siku moja akikemea kwa sababu ya kuweka maslahi yake mbele na si ya nchi na wala sijawahi kusikia record yake yeyote ya kuwatetea wananchi kokote kule pamoja na wananchi wa igunga kuwa matatizo chungu mzima. sasa hivi ndio anajiahandaa kupita vijijini kuanza kuwaaidi watu kuwa atawatetea na kutatua matatizo ingawa matatizo hayo yapo miaka yote na yeye anayajua lakini alichagua kula raha dsm. kashindye yuko karibu na wananchi kwani yeye ni mkazi wa igunga watoto wake na familia wake wamekulia igunga mpaka leo hii. jiulizeni watoto wa Dr. Kafumu wanasoma au walisoma wapi ?? yeye mwenyewe akiumwa huwa anatibiwa wapi ?? kama majibu siyo Igunga basi siyo mwenzenu huyo anataka ubunge tu. ukaribu wake na wananchi, record yake ya kutetea maslahi ya waalimu na elimu yake ya chuo kikuu ni sifa tosha chadema walifanya homework yao.
   
 18. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huko tunaoitakia mema nchi hii tunatamani na tuna hamu watu wa Igunga waifundishe adabu CCM kwa kuipiga chini kwa kishindo warudi kama walivyorudi Tarime usiku kwa helcopta yao.
  Peoplllllllllllllllleeeeeeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzzz Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerz
   
 19. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama hakuna uchakachuaji, hapana shaka ushindi mnono ni kwa CDM.
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  natamani kuwa igunga kushiliki ukombozi wajimbo hilo..
   
Loading...