MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Matendo ya Saed Kubenea ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo yako mbioni kuwaingiza wananchi katika gharama ya uchaguzi mwingine wa kumtafuta Mbunge mpya wa Jimbo la Ubungo.
Wataalam wa mambo ya kisiasa wanatuambia demokrasia ni gharama hata hivyo gharama za demokrasia ambazo hazina mpango(justification) ni kama wizi wa mali ya umma. Matokeo ya matendo ya Saed Kubenea yako mbioni kuakisi wizi wa mali za umma(unjustifiable expenditure).
Ikumbukwe kuwa, Mbunge huyu wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kwa tiketi ya CHADEMA kwa sasa ana kesi mahakamani ambayo matokeo yake yanaweza kutengua kikatiba Ubunge wake wa Jimbo la Ubungo.
Saed Kubenea anadaiwa mahakamani kama ilivyonukuliwa na Gazeti la Majira kutenda kosa Desemba 14, 2015, katika Kiwanda cha Nguo cha Took Garment Com Ltd, kilichopo Mabibo External kwa kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya, Makonda akisema ni kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo alichonacho ni cha kupewa hali ambayo iliashiria uvunjifu wa amani na utulivu.
Katika macho ya kanuni za adhabu nchini, kosa la Kubenea linakaribisha kifungo gerezani cha kuanzia miezi sitta.
Katika sheria ya Kanuni za adhabu Sura ya Sita, kifungu cha 89(1)(a-b) kinasema;
89(1) Mtu ye yote ambaye:-
(a) atatumia maneno ya kinyaa, ya matusi au ya usafihi kwa mtu mwingine yeyote kwa namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani; au
(b) atazozana au kwa namna nyingine yeyote ataleta fujo kwa namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani. Mtu huyo amekosa kosa dogo na atakapoonekana na hatia atapasiwa kifungo cha miezi sita.
Katiba yetu ya mwaka 1977 kwenye kifungu cha 67(2)(c) inasema;
67(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Wananchi wa Ubungo kuingia kwenye Uchaguzi mwingine ambao sababu zake zingeweza kuzuilika kiutaratibu na kisheria liwe funzo kwa taifa!
Ni vizuri Mamlaka zinazowasimamia wawakilishi ambazo ni Tume ya Uchaguzi, Bunge na vyama vya siasa ziangalie utaratibu wa kuanzisha semina elekezi mapema iwezekanavyo baada ya uchaguzi ili wawakilishi wa aina ya Saed Kubenea waweze kupata darasa litakalo wawezesha kuelewa umuhimu wao katika taifa.
Wawakilishi wa aina ya Saed Kubenea lazima waelewe neno MHESHIMIWA kama kianzishi cha Jina kwa wabunge halikuwekwa kama pambio bali limewekwa kuonyesha umuhimu wa Mbunge katika jamii na taifa.
Huyu MHESHIMIWA tokea atangazwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, he keeps hitting the headlines for all the wrong reasons. Hawezi hata kujifunza kutoka kwa wabunge wa aina ya John Mnyika ambao wamefanikiwa katika ubunge siyo kwa sababu ya wrong reasons and character bali kwa sababu ya kuibua hoja za kitaifa na kuzisimamia kwa nguvu za hoja. Mnyika has always been exceptionally good at his job, he never puts a foot wrong.
Wananchi wanaingia gharama kubwa kumpata Mbunge lakini vile vile inatakiwa watu wa aina ya Saed Kubenea wawekewe chujio imara ili wasiweze kupenya na kuwa wabunge kwa sababu matendo yao hayaakisi/hayaendani na gharama za kumpata Mbunge kutoka kwa wananchi ambao ni walipa gharama za uchaguzi.
Waingereza wanasema, justice is blind, hii ina maana kuwa sheria hazina siasa na kwa maana hiyo, ni vizuri wananchi wa Jimbo la Ubungo wakaanza kujiandaa mapema kuingia kwenye Uchaguzi mwingine wa kupata Mbunge Mpya.