Vijana wa dot com ndio hawajui umuhimu wa mwenge...
Mwenge sio tu lile litaa linalowaka...think big...
Mwenge ni zaidi ya hapo...rudi kwenye dhana yenyewe ya mwenge kuwa ni uhuru, ni taa ya matumaini na inachoma maadui zetu...
Mwenge hauna tofauti na ziara za Lowassa anazopanga kufanya nchi nzima...lengo lake ni kuhamasisha wafuasi wake kwa lengo fulani pamoja na kukijenga chama chake...
Vivyohivyo Mwenge lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu kuongeza jitihada katika mapambano dhidi ya UKIMWI, vita dhidi ya rushwa na ufisadi, vita dhidi ya dawa za kulevya na umuhimu wa kuitunza amani tulionayo...
Ndugu zangu...wanasiasa wanatuaminisha mambo mengi ya hovyo hasa wale wenye elimu ya hapa na pale ili wajinufaishe binafsi bila kuueleza ukweli...
Nimekuwa nikiona wananchi wanahamasika pale Mwenge wa uhuru unapokaribia kufika maeneo yao kwa kuchangia na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili izinduliwe na Mwenge...nimekuwa nikiona miradi kama zahanati, barabara na vituo vya afya ikikamilishwa haraka ili izinduliwe na Mwenge. Miradi hio unakuta isingekamilishwa kwa wakati na Halmashauri ila kama wanakuwa hawana miradi mizuri itakayozinduliwa au kuwekewa mawe ya msingi hupewa alama mbovu na hutakiwa baadae kujieleza...
Kupitia mbio za mwenge wa uhuru wanachi wananufaika sana...
Pia maendeleo ni gharama na Mwenge hugharimiwa kukimbizwa lakini gharama hizo sio kuuubwa kama tunavyoaminishwa kiaso cha kuona ni anasa...wananchi wenyewe huchangia kwa kuweka utaratibu wa namna ya kukimbiza mwenge katika maeneo yao...wakimbiza mwenge kitaifa hugharamiwa chakula na mafuta kwenye halmashauri husika wanapokabidhiwa...sio kwamba kuna mabilioni hutengwa na serikali kuu...hapana...