Je? Maagizo ya kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2024 yamepuuzwa?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,292
7,863
Wiki tatu zilizo pita Kiongozi wa Mwenge kitaifa alitoa maagizo kuwa; Mabasi yote yanayo pakia na kushusha abiria nje ya Stendi ya Magufuli watoke huko na warudi ndani ya stendi.

Kumekuwa na utitiri wa vituo vya mabasi ya abiria maeneo mbalimbali ya jiji la Dsm haswa maeneo ya Shekilango hadi Urafiki. Mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo hayo.

Kiongozi wa mbio za mwenge amesema kitendo hicho kinaikosesha mapato serikali, hivyo ameziagiza Mamlaka kuhakikisha kuwa Mabasi yote yanapakia na kushusha abiria katika kituo cha Magufuli.

Cha kushangaza hadi sasa bado mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo ambayo sio rasmi, jambo hilo sio tu linaikosesha Serikali mapato bali pia usalama wa abiria ni mdogo sana

LATRA chukueni hatua haraka, ondoeni mabasi hayo kwenye maeneo hayo.
 
Si mlishasema kuwa mwenge hauna tija, sasa mnataka tutii maelekezo ya kiongozi asiye na tija?
 
Wiki tatu zilizo pita Kiongozi wa Mwenge kitaifa alitoa maagizo kuwa; Mabasi yote yanayo pakia na kushusha abiria nje ya Stendi ya Magufuli watoke huko na warudi ndani ya stendi.

Kumekuwa na utitiri wa vituo vya mabasi ya abiria maeneo mbalimbali ya jiji la Dsm haswa maeneo ya Shekilango hadi Urafiki. Mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo hayo.

Kiongozi wa mbio za mwenge amesema kitendo hicho kinaikosesha mapato serikali, hivyo ameziagiza Mamlaka kuhakikisha kuwa Mabasi yote yanapakia na kushusha abiria katika kituo cha Magufuli.

Cha kushangaza hadi sasa bado mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo ambayo sio rasmi, jambo hilo sio tu linaikosesha Serikali mapato bali pia usalama wa abiria ni mdogo sana

LATRA chukueni hatua haraka, ondoeni mabasi hayo kwenye maeneo hayo.
Agizo la kipuuzi. Kwa hiyo nikiwa natoka mkoa naishi sinza na gari linaelekea sinza nishuke magufuli badala ya shekilango. Hayo mabasi yanaingia stand wanaoshuka wanaoshuka na wanaopanda wanapanda. Gari nyingine zinaanzia mbagara wa mbagara wanapata ahueni ya usafiri badala ya kukimbizana mpaka wafike magufuli.
Acha lipuuzwe maana hata bungeni lilishazunguzwa na likaonekana halina tija nakumbuka aliyeongoza mjadara alikuwa shabiby akasema wao kama wamiliki kama hawaoni shida kuwapeleka abiria wanakoenda pasipo kuongeza nauli shida iko wapi.
 
Kiongozi wa mbio za mwenge ni mtu mdogo sana maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, afadhali mkuu wa wilaya kama mamlaka husika haiwezi kuchukua hatua. Anyway, jiji la dar ni kubwa kiasi cha kuwa taabu na shida kurundika mabasi sehemu moja ili tu kukusanya mapato. Ni bora kila kampuni iwe na vituo vyao jiji zima ili iwe rahisi kuvifikia
 
Kuna jeuri inaendelea.
inakuwaje maagizo ya mamlka kupuuzwa?!!
 
Kwasababu Uchaguzi ni Mwakani hawataguswa ili waipe kure CCM kwa kuonekana kuwa serikali inawajali...subiri uchaguzi uishe mwakani...ndio utaona ukali wa migambo na virungu vya polisi
 
Hapo umekosea.
Utawala wa awamu ya 6 ni utawala wa kufuata na kutii sheria.

Mabasi yote yanayo pakia na kushusha abiria nje ya stendi ya magufuli lazima yazuiwe haraka sana.

LATRA wanao wajibu wa kulisimamia agizo hilo.
 
Wiki tatu zilizo pita Kiongozi wa Mwenge kitaifa alitoa maagizo kuwa; Mabasi yote yanayo pakia na kushusha abiria nje ya Stendi ya Magufuli watoke huko na warudi ndani ya stendi.

Kumekuwa na utitiri wa vituo vya mabasi ya abiria maeneo mbalimbali ya jiji la Dsm haswa maeneo ya Shekilango hadi Urafiki. Mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo hayo.

Kiongozi wa mbio za mwenge amesema kitendo hicho kinaikosesha mapato serikali, hivyo ameziagiza Mamlaka kuhakikisha kuwa Mabasi yote yanapakia na kushusha abiria katika kituo cha Magufuli.

Cha kushangaza hadi sasa bado mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo ambayo sio rasmi, jambo hilo sio tu linaikosesha Serikali mapato bali pia usalama wa abiria ni mdogo sana

LATRA chukueni hatua haraka, ondoeni mabasi hayo kwenye maeneo hayo.
Mwambie atulie bibi anatuletea mikopo
 
Huu ni upuuzi sana kulazimisha mabasi kupita stand.

Kwa mfano magari yanapita Dodoma kutokea Arusha/moshi kwenda Iringa, Mbeya Njombe unayataka yaende 88 stand, ni kupoteza muda kwa abiria na gharama kwa wamiliki wa magari.

Unapoteza karibia saa zima kuzunguka na kuongeza foleni katika ya mji.
 
Back
Top Bottom