Mbio za 29 za mwenge wa Uhuru kumaliza siku 150 na wilaya 150 kesho Wilayani Chato | Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,450
799

Mwenge wanusa harufu ya rushwa na ufisadi kwenye miradi 49 kati ya miradi 1,097 yenye thamani ya 1.2trilioni iliyozinduliwa | TZS 65b zahofiwa kutafunwa na mchwa,​


" Chato tunasema Asante "​


Mtakumbuka Mwenge wetu wa Uhuru uliwashwa rasmi tarehe 17|05|2021 Makunduchi Zanzibar na leo tarehe 14|10|2021 Mwenge wa Uhuru Umefikia kilele chake Mkoani Geita ikiwa ni baada ya kumalizika kwa siku 150 za matembezi yake bara na Visiwani katika Wilaya za kiutawala 150,mikoa 31 sawa na jumla ya kilometa 21,480 hakika ni jambo la kupongezwa na hii ndio tofauti ya CCM na vyama vingine vinavyoupinga,

Mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ( Chief Hagaya ) aliyeambana na DP Dk Philip Mpango,Rais wa Zanzibar na Mkt wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwingi,Waziri Mkuu wa JMT Mhe Khasim Majaliwa Majaliwa,Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma,Mawaziri,wabunge,wakuu wa wilaya na mikoa pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa vyama na Serikali,Kilele hicho asubuhi kilitanguliwa na Misa Takatifu ya kuwaombea Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa hili ambae leo ndio siku yake kitaifa,Hayati Julius Kambarage Nyerere alifariki 14|10|1999 lakini pia alikumbukwa na kuombewa Rais wa awamu ya Tano Hayati Dk John John Joseph Pombe Magufuli na baadae shughuli iliendelea katika Uwanja wa Magufuli Chato.

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru kabla ya kuhitimisha kilele chake umezindua Jumla ya miradi mikubwa 52 mkoani Geita,Kiongozi wa mbio hizi za Mwenge wa Uhuru Kitaifa alikuwa mwanamama Lt Josephine Mwambashi akisaidiwa CPL.Hafidhi Shaban, CPL. Mohamed Mbegu, CPL. Rehema Haji,Pte. Dismas Mvula na Lt Jofrey Juma Vijana hawa wanastahili pongezi kubwa na kwahakika tumeuona Uzalendo wao kwa Taifa lao walikuwa wakali kama nyuki Pindi wanapokuta miradi ya maendeleo ya Serikali haiko sawa hakika wanastahili,

Katika hali isiyoyakawaida Kiongozi wa mbio za Mwenge Lt Josephine Mwambashi alitoa ripoti ya mwenye iliyoonesha kuna harufu ya Rushwa na Ufisadi kwenye Jumla ya miradi 49 yenye thamani ya Tshs 65.34BL kati ya miradi 1,097 yenye thamani ya Tshs 1.2trilioni iliyozinduliwa nchi nzima katika Wilaya 38 ambazo Lt Mwambashi ameomba iundwe tume huru kwaajili ya Uchunguzi zaidi huku akimkabidhi Rais ripoti ya awali ya Takukuru huku Mhe Rais Samia Suluhu Hassan akiahidi kulifanyia kazi,

Hitimisho hili limetanguliwa na siku nane ( 8 ) za kongamano la Vijana na hapa kipekee kabisa naomba niwapongeze sana Mhe Jenistha Muhagama Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Pamoja na Mhe Patrobas Katambi|Ummy Nderiananga manaibu wake Pamoja na Waziri wa michezo wa Zanzibar kwa kulifanya kongamano la vijana na shughuli nzima ya maandalizi ya mwenge kuwa yenye tija kwa Geita na Taifa kwa Ujumla wake,Miongoni mwaviongozi Mawaziri wakujivunia kama Taifa ni hawa watu watatu may The almighty God bless them wanajituma sana watu wa Geita watakubaliana na Mimi 100%

Kama Taifa tuendelee kuwaombea pumziko la milele na kufuata nyayo zao viongozi hawa Hayati Dk John Pombe Magufuli,Hayati Dk Benjamin Mkapa na Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere-Amina

 
Mwenge ni "mungu" wa CCM.
Mwenge ni laana.
Mwenge ni chanzo cha "umasikini" wa kujitakia.
 
Tanzania ndio maana imebarikiwa na inabarikiwa kila siku kwa sana,

Kitendo cha kuwaenzi hawa viongozi kunaiongezea baraka nchi yetu,

Huu ndio uzalendo unaotakiwa ,

Nakupongeza sana Rais Samia kwa hili,

R. I. P MAGUFULI
R. I. P MKAPA
R. I. P NYERERE
 
Mimi namuenzi mzee wa Uwazi na Ukweli Benjamin Mkapa,

Kazini kwangu mimi ni mkuu wa idara napenda sana mfanyakazi muwazi na mkweli,

Tukijenga Seikali ya uwazi tutapunguza rushwa kwa kiwango kikubwa sana
 
Amen,
 
Katambi kweli yuko vizuri dogo ni mtiifu sana Chadema alituumiza sana dogo,
 
Mama Samia karibu Chato,
Tunakupenda sana sana

endelea kutukumbuka mama yetu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…