Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,808
- 11,973
MTAKA AELEZA NAMNA MIKAKATI YA KUKUZA ELIMU SIMIYU ILIVYOZAA MATUNDA
Sekta ya Elimu Mkoani Simiyu imekuwa ikifanya vizuri katika kipindi hiki cha karibuni. Katika matokeo ya darasa la saba Mwaka huu 2020 Mkoa wa Simiyu umetoa shule 8 katika orodha ya shule zilizoongeza ufaulu kwa kiasi kikubwa kitaifa kwa muda wa miaka 3 mfululizo. Hii imepelekea Jamii Forums kufanya mahojiano na Mkuu wa Mkoa huo ili kutambua mikakati iliyotumika kuendeleza Elimu Mkoani hapo.
Akizungumza na Jamii Forums, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka ameeleza mikakati mbalimbli iliyoweza kukuza Sekta ya Elimu Mkoani hapo.
Mtaka ameeleza kuwa ajenda ya kuipa Sekta ya Elimu kipaumbele ndiyo iliyopelekea kukuza ufaulu kwa madarasa yote Mkoani Simiyu. Amesema, Sekta ya Elimu ikiendelezwa itapelekea kukuza Sekta nyingine zote kama Kilimo, Ufugaji, Afya na Viwanda.
Ameeleza mazingira ya Mkoa wa Simiyu kwa Wanafunzi kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Wazazi walio katika hali duni kutamani Watoto wao waache shule ili kuwapunguzia gharama. Hii upelekea Wazazi kuwaonya Watoto wao wakienda kufanya mtihani wa Taifa wahakikishe hawatofaulu.
Ameongeza kuwa Walimu wamekuwa wakifanya kazi tatu. Kazi ya kumjenga Mzazi atoe hamasa kwa Mtoto ili asome, kazi ya kumjenga Mtoto aweze kusoma na kazi ya kuhakikisha Mtoto anasoma na kufaulu.
Amesema, Mkoa wa Simiyu ni tofauti na sehemu nyingine kama Dar es Salaam ambapo Mtoto anapoanza darasa la kwanza anakuwa ameshasoma pre-nursery, ama akienda kuanza kidato cha kwanza anakuwa ameshasoma pre-form one. Hivyo basi kwa Simiyu inahitajika mikakati maalumu ambayo itamsaidia Mtoto kusoma.
Vilevile amesema Walimu walishapoteza matumaini kutokana na mazingira yaliyopo. Muda mwingine kunakuwa na mambo ya kimila ambayo wanakuwa wanafanyiwa Walimu. Hivyo ni lazima haya makundi matatu, Mzazi, Mwalimu na Mwanafunzi yaweze kuletwa pamoja na kushirikiana.
Amesema 2016 Simiyu ilikuwa ya mwisho kwa mitihani ya Taifa darasa la nne na la saba, kidato cha pili, cha nne na cha sita. Hivyo basi waliweka mikakati ya miaka mitano ambayo ingeweza kuwatoa kutoka hapo walipo hadi kufika namba moja.
Aidha Mtaka ameeleza kuwa mkakati wa kwanza ulikuwa ni kuleta motisha kwa Walimu kwani wamekuwa wakifanya kazi ambayo jamii haiwaungi mkono. Amesema Viongozi hawapaswi kuwa sehemu ya jamii hiyo, hivyo ni lazima walete nuru kwa Walimu ili waweze kufanya kazi yao katika mazingira mazuri.
Mkakati mwingine ni kuandaa kambi za kitaaluma ili kuhakikisha Wanafunzi walio katika kipindi cha mitihani kuhakikishiwa wanapata mazingira mazuri ya kusoma. Wanafunzi wamekuwa wakitumia madarasa kuweka kambi hizo baada ya muda wa kawaida wa masomo. Hii imesaidia kuwaepusha Wanafunzi na shughuli mbalimbali za nyumbani zinazowazuia kujisomea kipindi cha mitihani.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa waliweza kufanya utafiti kwa kufuatilia shule binafsi zinazofanya vizuri namna zinavyojiendesha. Na kubaini kuwa Mwanafunzi wa sekondari kabla ya kufanya mtihani wa Taifa anakuwa ameshafanya mitihani ya kujiandaa zaidi ya 50-100, kwa shule ya msingi anakuwa amefanya wastani wa maswali si chini ya 6000. Hii ni tofauti kwa shule za Serikali, ambapo Mwanafunzi anakuwa amefanya mitihani si zaidi ya 7 kabla ya mtihani wa Taifa.
Vilevile ili kuweza kukuza ufaulu kwa Wanafunzi wanaofanya vibaya darasani mkakati mwingine ulikuwa ni kuwaajiri Walimu wazuri kutoka katika shule zinazofanya vizuri, kwa miezi mwili hadi mitatu. Walimu hao ni kwa ajili kuboresha matokeo kwa Wanafunzi.
Aidha ili kuongeza motisha ulianzishwa utaratibu wa kutoa tuzo kwa Walimu na Wanafunzi waliofanya vizuri. Ikipatikana A kwenye somo la kidato cha nne Mwalimu anapata 30,000, ikipatikana B anapata 10,000. Kwa kidato cha sita ikipatikana A Mwalimu anapata 50,000 na Mwanafunzi anapata 100,000.
Aidha Mtaka ametoa shukrani kwa Viongozi wote wa Mkoa Simiyu kwa ushirikiano wanaotoa katika kuendeleza Mkoa huo. Vilevile ametoa wito kwa Viongozi kutoa hamasa kwa Walimu na kuepuka kutoa kauli za kuwakatisha tamaa. Amesema lugha chafu kwa Walimu huwafanya wakate tamaa na kazi yao, na kupelekea kutofanya kwa ufasaha shughuli zao.

Hongera sana RC Simiyu Ndugu Anthony Mtaka, wewe ni kiongozi kweli
Uongozi maana yake kuonesha njia na ku-influence wengine wawe vile utakavyo ama inavyotakiwa wawe. Miongoni mwa mikoa yenye jamii ngumu kuziongoza kuelekea kwenye "peak" ya mapinduzi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ni mikoa ya kanda ya ziwa inayoundwa na Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na...
www.jamiiforums.com