Mbinu za medani: Aida Khenan, Mbunge wa Nkasi ndiyo awe Mwenyekiti wa CHADEMA

Habari wanajukwaa,

Kufuatia uchaguzi kuisha na CHADEMA kuambulia Mbunge mmoja huko Nkasi Kaskazini, Aida Khenan aliyeibuka mshindi kwa kumbwaga mbunge machachari wa CCM Ally kesi aliyeliongoza jimbo hilo kwa miaka kumi!

Ikumbukwe Aida Khenan licha ya yeye kuibuka kidedea pia kwenye jimbo lake jumla ya madiwani kumi wa CHADEMA walishinda kwenye kata zao, hivyo kulifanya jimbo la Nkasi kuongoza kwa kuibwaga CCM kwenye ubunge na udiwani!

Ikumbukwe pia, kabla ya uchaguzi vigogo wa CHADEMA waliokuwa wanajimwambafai kuwa wanazijua mbinu za medani za kuishinda CCM ni Mbowe, Mdee ,Lema ,Msigwa ,Heche na Sugu walioishia kubwagwa vibaya sana kwenye majimbo yao!

Kwa muktadha huo kati ya Mbowe na Aida Khenan ni nani anazijua mbinu za medani za kushinda uchaguzi? Bila shaka ni Aida Khenan wa Nkasi Kaskazini na si Lema ,Msigwa wala Mdee!

Je, CHADEMA iko tayari kuongozwa na mwenyekiti asiyejua medani za kushinda uchaguzi? La hasha CHADEMA inatakiwa kuongozwa na Aida Khenan anayejua mbinu za kuishinda CCM bila kuleta visingizio vya tume, polisi wala mawakala.

Anayejua jinsi ya kushawishi wananchi, kusambaza mawakala vituoni ,kudeal na polisi ,kumbana mkurugenzi ndiyo awe mwenyekiti wa CHADEMA.

Si Mbowe ,wala Tundu Lisu aliyefika Nkasi kumuombea kura Aida lakini bado akaibuka kidedea, hivyo anazo sifa zote za kuwa mwenyekiti mpya wa chama.
Itapendeza mumeo awe mwenyekiti,halafu mama mkwe wako makamu
 
CHADEMA wanatakiwa wamfute uachama abaki kuwa mbunge wa CCM, mbunge gani anaongea na ana kidharau chama?
Ana haki ya kuidharau chadema maana kaona hawana uwezo wa kushinda ila yeye tuu. Hivyo lazima awadharau.
 
Viongozi wakuu cdm ubinafsi fulani. Kipindi cha uchaguzi serikali za mitaa walipiga mkwara hakuna kushiriki wakati mchakato kwenye chama tayari na fomu zimechukuliwa(wananchi /wanachama walishajiandaa),wakatangaza hawautambui huo uchaguzi. Uchaguzi mkuu uloisha tumeona.... Lazima fulani washinde ndo uchaguzi unakuwa halali
 
Sasa wamfukuze kwa kosa gani? Huyu ni wa kumtenga na kumnyima ushirikiano kuanzia ngazi ya chini hadi juu, lazima ni mtoa Siri na amewekwa hapo kwa kusudi maalum
Sasa wamtenge kwa kosa gani? Na ushirikuano gani ambao mkimnyima atashindwa kwenda bungeni?
Hamueleweki mnataka Nini maana kila siku kumsakama huyu mama.
 
Back
Top Bottom