Mbinu za medani: Aida Khenan, Mbunge wa Nkasi ndiyo awe Mwenyekiti wa CHADEMA

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,359
14,633
Habari wanajukwaa,

Kufuatia uchaguzi kuisha na CHADEMA kuambulia Mbunge mmoja huko Nkasi Kaskazini, Aida Khenan aliyeibuka mshindi kwa kumbwaga mbunge machachari wa CCM Ally kesi aliyeliongoza jimbo hilo kwa miaka kumi!

Ikumbukwe Aida Khenan licha ya yeye kuibuka kidedea pia kwenye jimbo lake jumla ya madiwani kumi wa CHADEMA walishinda kwenye kata zao, hivyo kulifanya jimbo la Nkasi kuongoza kwa kuibwaga CCM kwenye ubunge na udiwani!

Ikumbukwe pia, kabla ya uchaguzi vigogo wa CHADEMA waliokuwa wanajimwambafai kuwa wanazijua mbinu za medani za kuishinda CCM ni Mbowe, Mdee ,Lema ,Msigwa ,Heche na Sugu walioishia kubwagwa vibaya sana kwenye majimbo yao!

Kwa muktadha huo kati ya Mbowe na Aida Khenan ni nani anazijua mbinu za medani za kushinda uchaguzi? Bila shaka ni Aida Khenan wa Nkasi Kaskazini na si Lema ,Msigwa wala Mdee!

Je, CHADEMA iko tayari kuongozwa na mwenyekiti asiyejua medani za kushinda uchaguzi? La hasha CHADEMA inatakiwa kuongozwa na Aida Khenan anayejua mbinu za kuishinda CCM bila kuleta visingizio vya tume, polisi wala mawakala.

Anayejua jinsi ya kushawishi wananchi, kusambaza mawakala vituoni ,kudeal na polisi ,kumbana mkurugenzi ndiyo awe mwenyekiti wa CHADEMA.

Si Mbowe ,wala Tundu Lisu aliyefika Nkasi kumuombea kura Aida lakini bado akaibuka kidedea, hivyo anazo sifa zote za kuwa mwenyekiti mpya wa chama.
 
Chadema sijui wanasubiri nini kumfukuza kwenye chama?
Sioni haja ya kumfukuza. Wamwache tu maana waliomuweka hapo wanatafuta gia ya kuishambulia chadema. Wakimfukuza watawapa kiki maana ndo ilikuwa nia yao. Wamuweke halafu afukuzwe wapate chakusema
 
Yeye mwenyewe hajui ameshindaje, alivyosikia matokeo ya Mbowe ile usiku usiku yalivyotoka alikuwa anajua wameshamla kichwa
Nani kakwambia huyo mama anajiamini na aliishamwambia Least tutakutana jimboni akadhani ni kejeli na Sasa kaamini Kenani ni kisiki Cha
Mpingo.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom