CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,789
- 8,915
mkuu hapo kwenye red, kuku wa hivyo unaweza kum-handle namna gani? halafu,
ratio inayotakiwa hasa kati ya jogoo na tetea ni ipi mkuu? yani kuku jike wangapi wanatakiwa wamilikiwe na jogoo mmoja ili kuokoa vita kati ya majogoo?
asante..
mkuu nisha elezea kama kuku unawafuga nje yaani wana piga misele nje Ratio nzuri ni mitetea watano kwa jogoo mmoja hii ni kwa sababu nje jogoo hutumia nguvu nyingi sana pale anapo kimbiza mtetea, kama ni ndani hata mitetea 10 kwa jogoo mmoja ni sawa, Ila kuna aina nyingine za kuku ambao ni havy mfano Dorep jogoo mmoja anatakiwa mitetea 4 hadi 5 hata kama ni ndani wanafugiwa
mkuu asante sana kwa maelezo mazuri,
niko mbioni kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji ambapo minimum nimeamua nianza na kuku 30 majike, hivyo basi kulingana na ushauri wako itanibidi niwe na majogoo kama 6 kwa ajili ya kusimamia uzalishaji.
mkuu, nina kaswali kadogo hapa, hivi huu mtindo wa kuokota mayai mara tu kuku anapotaga na kwenda kuyatunza hauwezi kumuathiri hasa pale anapofikia hatua za mwisho wa utagaji?
inawezekana kweli akaatamia bila kuona mayai? au inakuwaje hapo?
haimuathili kuku akisha fikia kuanza kuatamia ataenda ile sehemu yake ya kutagia ataanza kulala pale hata kama hakuna mayai, Na ni vizuri kuokota mayai ili yasipate wadudu au kuvunjika lakini akma banda ni zuri na kuna kiota basi unaweza kumuachia mayai yake pale pale haina haja ya kuyatoa
Mtaalam kuna sehemu nimeona umetaja incubator...hizi machine zenye ubora zapatikana wapi.
Njia nyingine ni kumtumia kuku kuangua mara mbili mfululizo,yan anapoangua mara ya kwanza unatoa vifaranga immediately kabla hajaamua kutoka navyo alafu unaweka mayai mengine,lakin angalizo uweke kwnza mayai mabovu ili ayazoee alafu ndio unaweka mazima,kwa njia hii utajikuta unatotolesha vifaranga vingi kwa muda mfupi
namba (2) si kweli. kitaaramu mayai yasizidi siku 14, japo kuku anaweza akatotoa hata mayai 18, aliyo taga mwenyewe. wafugaji wanao fuga kijadi. vijijini, watakubariana na Mimi. kwani huko kuku hutotoa vifaranga vingi tu. nikipata nafasi nitaweka chapisho la kitabu nilicho kitoa (SUA) ili tuelimike ote, nilichelewa kutoa mchango wangu huu kwakuwa nilipigwa BN, asanteni.
namba (2) si kweli. kitaaramu mayai yasizidi siku 14, japo kuku anaweza akatotoa hata mayai 18, aliyo taga mwenyewe. wafugaji wanao fuga kijadi. vijijini, watakubariana na Mimi. kwani huko kuku hutotoa vifaranga vingi tu. nikipata nafasi nitaweka chapisho la kitabu nilicho kitoa (SUA) ili tuelimike ote, nilichelewa kutoa mchango wangu huu kwakuwa nilipigwa BN, asanteni.
unawezezaje kutoa vifaranga ....kwani kuku anakuwa kwenye kiota chake Muda wote
Nina kuku wangu anatoka na vifaranga kumi na sita, sasa hii ya siku saba imenipa good time ya kujifunza zaidi.
Jamani nitoeni ushamba katika hili, hivi ni nini huwa kinasababisha kuku asiangue baadhi ya mayai aliyowekewa?? ukiacha suala la yai kutokuwa na mbegu..
Hivi majuzi nilikumbwa..niliwawekea kuki wawili mayai 23. Katika hayo mayai nilipata vifaranga 7 tu..mengine yote viza
naomba kujua hii mashine inapatikana wapi kwa sh ngapi?