Mbinu za kuangua vifaranga kwa njia ya Kienyeji

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,655
Habari wapendwa.
Kutokana na kutafuta njia za kijikim na kupata kujiajiri mwenyewe,Nimefikia wakati ambapo nahitaji kuongeza nguvu na juhudi za kuweza kufanya uzalishaji uongezeke haraka kwa kipindi kifupi.

Kutokana na hayo ningependa kujua kama kuna uwezekano wa kutumia. njia ya kienyeji katika kuangua vifaranga wa kuku.

Mashine kwa sasa ziko juu zaidi.
Hivyo kama unaijua njia ya kienyeji ambayo itakua rahisi karibuni kwa Michango yenu.

Wenu katika Ujasiriamali.
 
Njia za kienyeji ni za kutumia kuku, na zaidi ya kutumia kuku ni kutumia mashine, kuhusu mashine ni kweli ni ghari sana ila unaweza jipanga ukanunua hata ya mayai 45 au mayai 60 ambazo hazizidi laki 30000.
 
Njia za kienyeji ni za kutumia kuku, na zaidi ya kutumia kuku ni kutumia mashine, kuhusu mashine ni kweli ni ghari sana ila unaweza jipanga ukanunua hata ya mayai 45 au mayai 60 ambazo hazizidi laki
30000.

Sijakuelewa hapo mkuu Chasha
Una maana ya elf 30 au?
Na kama ni hizo mashine nikiweza kununua je itakaa na umeme muda gan pindi umeme ukatikapo.
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa hapo mkuu Chasha
Una maana ya elf 30 au?
Na kama ni hizo mashine nikiweza kununua je itakaa na umeme muda gan pindi umeme ukatikapo.
Mkuu ni laki 3 sio elfu 30. Mashine unatakiwa uwe na jenireta au solar, mashine zenye uwezo wa kutunza joto kwa muda mrefu ni zile kubwa ambazo nyingi hutunza kati ya masaa 4 hadi 6.
 
Njia za kienyeji ni za kutumia kuku, na zaidi ya kutumia kuku ni kutumia mashine, kuhusu mashine ni kweli ni ghari sana ila unaweza jipanga ukanunua hata ya mayai 45 au mayai 60 ambazo hazizidi laki 30000.

laki 30000 ndo shilingi ngapi mkuu
 
Mkuu ni laki 3 sio elfu 30. Mashine unatakiwa uwe na jenireta au solar, mashine zenye uwezo wa kutunza joto kwa muda mrefu ni zile kubwa ambazo nyingi hutunza kati ya masaa 4 hadi 6.

naomba kujua hii mashine inapatikana wapi kwa sh ngapi?
 
Njia nyingine ni kumtumia kuku kuangua mara mbili mfululizo,yan anapoangua mara ya kwanza unatoa vifaranga immediately kabla hajaamua kutoka navyo alafu unaweka mayai mengine,lakin angalizo uweke kwnza mayai mabovu ili ayazoee alafu ndio unaweka mazima,kwa njia hii utajikuta unatotolesha vifaranga vingi kwa muda mfupi
 
Kuku akishasikia sauti ya kifaranga baada ya siku mbili hutoka kwa maana anajua ameshaangua hivyo unaweza kuharibu mayai.
 
kuna njia ya kuangua vifaranga kwa njia ya kutumia pumba, majivu.......... ukiweka kwenye ndoo either pumba au majivu yenye joto na ukaweka mayai yako juu kwa siku zile zile 21 unaweza kupata vifaranga, ila usifunike ndoo ili mayai yapate hewa na kiasi cha mwanga, hata hivyo inahihaji uangalizi mkubwa sana katika kuyageuza mayai na kubadilisha majivu au pumba yako ........
 
kuna njia ya kuangua vifaranga kwa njia ya kutumia pumba, majivu.......... Ukiweka kwenye ndoo either pumba au majivu yenye joto na ukaweka mayai yako juu kwa siku zile zile 21 unaweza kupata vifaranga, ila usifunike ndoo ili mayai yapate hewa na kiasi cha mwanga, hata hivyo inahihaji uangalizi mkubwa sana katika kuyageuza mayai na kubadilisha majivu au pumba yako ........

hii ni njia ya hatari sana na haijawah pendekezwa kwa sababu ni pata potea,
 
kuna njia ya kuangua vifaranga kwa njia ya kutumia pumba, majivu.......... ukiweka kwenye ndoo either pumba au majivu yenye joto na ukaweka mayai yako juu kwa siku zile zile 21 unaweza kupata vifaranga, ila usifunike ndoo ili mayai yapate hewa na kiasi cha mwanga, hata hivyo inahihaji uangalizi mkubwa sana katika kuyageuza mayai na kubadilisha majivu au pumba yako ........

Toa maelezo ya kutosha ili kama tunaweza kujaribu tuone matokeo yake
 
hii njia tatizo lake ina higher risk more than return so inahitaji uangalizi wa karibu sana wa mtaalamu, pamoja na kuwa na uangalizi lakini matokeo hayako vizuri, its better to use machine than this analogue methods kuangua vifaranga
 
mkuu@chasha kuku wangu aliatamia mayai 12 lakini cha kushangazaza alitotoa kifaranga 1 tu je ni makosa gani yaliyofanyika hapo? au ni kawaida kutokea ivyo?
 
Kupata mashine za kutotolesha vifaranga (incubators) wasiliana na: Kapalata engineering LTD kwa simu 0786603325 au 0713846725 . Nadhani utapata ufumbuzi huko.
 
mkuu@chasha kuku wangu aliatamia mayai 12 lakini cha kushangazaza alitotoa kifaranga 1 tu je ni makosa gani yaliyofanyika hapo? au ni kawaida kutokea ivyo?

Mr unajogoo kulingana na idadi ya majike ulionayo?
Fuatilia kwavyovyote hilo ndio tatizo
 
Back
Top Bottom