Mbinu za kuangua vifaranga kwa njia ya Kienyeji

Chasha ulisema inqubeta bora kuagiza china za hapa bongo utendaji kazi wake ni hafifu, je unashaurije katika hili?
 
Mkuu kwa kawaida yai likitagwa inatakiwa ndani ya siku liwe tiarayi limewekwa kwa mashine au kuku kaanza kulalai, baada ya siku saba hatch bility inanza kushuka, ingawa unaweza kuta hata la siku 10 lina totolewa ila mara nyingi hatchibility inakuwa kubwa kwa mayai yenye only 7 day baada ya kutagwa. Na hata kuku mara nyingi yale mayai aliyo taga ya kwanza huwa hayatotolewa, ukikuta kuku katotoa vifaranga kadhaa za kaacha baadhi ya mayai mara nyingi huwa ni yale ya mwanzo kutagwa.

Ni vizuri yale mayai ya mwisho kutagwa ndo awekewe kuku na yale ya mwanzo unaweza kula au kuuza,
Kuku wangu anataga mayai 16 na huwa anatotoa yote, unalizungumziaje hili
 
namba (2) si kweli. kitaaramu mayai yasizidi siku 14, japo kuku anaweza akatotoa hata mayai 18, aliyo taga mwenyewe. wafugaji wanao fuga kijadi. vijijini, watakubariana na Mimi. kwani huko kuku hutotoa vifaranga vingi tu. nikipata nafasi nitaweka chapisho la kitabu nilicho kitoa (SUA) ili tuelimike ote, nilichelewa kutoa mchango wangu huu kwakuwa nilipigwa BN, asanteni.
Kwanini walikupiga ban mkuu?
 
Mkuu Chasha. Mm nna kuku wanatetea sana lkn coni matokeo kwa maana ya kutaga. Kipindi cha nyuma mmoja alikuwa anatetea badae kaacha na saivi tena wanatetea tu japo wanakula vzuri na jogoo wangu ni mzuri. Mkuu ivi hii ni nn? Naomba uzoefu na ushauri...
Kama hujawafungia yawezekana wanataga sehemu
 
Nakuomba uweke hapa kontact zake hapa ili kila mtu mwenye kuhitaji anufaike

HABARI,
Huyu mwenzetu anaulizia njia ya kienyeji naomba muelewe swali lake hizo mashine za kutengenezwa hazina tofauti na za kisasa na hata bei bado ni juu,Ila si mbaya kama utampatia hao jamaa anaweza kupata mwanga zaidi au msaada pia.

LUMUMBA
 
Njia bora na nzuri ya kutotolesha kwa haraka na kupata vifaranga wengi ndani ya muda mfupi, fanya yafuatayo
1. baada ya kuku kutotoa vifaranga wake muache kwa siku 3 kabla hajainuka ktk kiota chake, hamisha vifaranga vyote alivyoangua, na kisha mpe mayai visa ili umuangalie kama ataendelea kuatamia, viza yakae kwa siku3, kisha ondoa viza weka mayai mazuri kwa kuku kuendelea kuatamia, kwa kutumia mbinu hii kuku mmoja anaweza kutotoa vifaranga 60. nakaribisha maswali.
 
Huu na unyanyasaji sana kwa kuku. Hivi unajua kwamba muda ambao kuku anatamia huwa anapungua sana uzito? Angekuwa mtu ningesema anaconda sana kwasasbb huwa mlo wake ni mmoja tuu. Nawaza ukweli kuku huyo huyo apewe kiota alalie zaidi ya siku 40. Kweli huyu kuku anatendewa haki?

Tuache unyanyasaji wa aina hii kwa mifugo yetu.

Yaan sisi binadamu ni viumbe katili sana tena tusio kuwa na huruma
 
HABARI,
Huyu mwenzetu anaulizia njia ya kienyeji naomba muelewe swali lake hizo mashine za kutengenezwa hazina tofauti na za kisasa na hata bei bado ni juu,Ila si mbaya kama utampatia hao jamaa anaweza kupata mwanga zaidi au msaada pia.

LUMUMBA
Yaan sasa hapa kienyej mtu anaambiwa ampe kuku mayai mara mbili mfululizo ayatamie. Jaman kweli tunaitendea haki mifugo yetu hasa huyu kuku?

Kutaga na kuatamia ni kazi kama ilivyo kubeba mimba na kuzaa afu napata hisia baada ya kuzaa ukaambiwa tena urudi leba baada ya siku tatu ukaanze tena kupush?

Tuache ukatili kwa viumbe wengine. Bora aende akatotoleshe kwa mwenye mashine tray ni elf13 tuu
 
Ninakuunga mkono kwa 100% kwani hata mimi nilishafanya hivyo na kugundua ni mateso sana kwa kuku.

Tena mimi nilikuwa namuwekea na chakula kabisa na maji karibu lakini bado alikuwa anakonda sana na kuwa mwepesi.

Hii mbinu si nzuri na ni mateso kwa kuku.
 
Huu na unyanyasaji sana kwa kuku. Hivi unajua kwamba muda ambao kuku anatamia huwa anapungua sana uzito? Angekuwa mtu ningesema anaconda sana kwasasbb huwa mlo wake ni mmoja tuu. Nawaza ukweli kuku huyo huyo apewe kiota alalie zaidi ya siku 40. Kweli huyu kuku anatendewa haki?

Tuache unyanyasaji wa aina hii kwa mifugo yetu.

Yaan sisi binadamu ni viumbe katili sana tena tusio kuwa na huruma
Unapo mwekea mayai ya kuendelea kuatamia ni vyema, ukaweka na chakula na maji, mle mle bandani.
Mbinu hii ilinisaidia sana kupata kuku wengi ndani ya muda mfupi, nilianza na makoo sita na jogoo mmoja wa kuazima, baada ya muda mfupi nikawa na kuku zaidi ya 500.
 
Back
Top Bottom