Mbinu za kuangua vifaranga kwa njia ya Kienyeji

mkuu hapo kwenye red, kuku wa hivyo unaweza kum-handle namna gani? halafu,

ratio inayotakiwa hasa kati ya jogoo na tetea ni ipi mkuu? yani kuku jike wangapi wanatakiwa wamilikiwe na jogoo mmoja ili kuokoa vita kati ya majogoo?

asante..

mkuu nisha elezea kama kuku unawafuga nje yaani wana piga misele nje Ratio nzuri ni mitetea watano kwa jogoo mmoja hii ni kwa sababu nje jogoo hutumia nguvu nyingi sana pale anapo kimbiza mtetea, kama ni ndani hata mitetea 10 kwa jogoo mmoja ni sawa, Ila kuna aina nyingine za kuku ambao ni havy mfano Dorep jogoo mmoja anatakiwa mitetea 4 hadi 5 hata kama ni ndani wanafugiwa
 
mkuu asante sana kwa maelezo mazuri,

niko mbioni kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji ambapo minimum nimeamua nianza na kuku 30 majike, hivyo basi kulingana na ushauri wako itanibidi niwe na majogoo kama 6 kwa ajili ya kusimamia uzalishaji.

mkuu, nina kaswali kadogo hapa, hivi huu mtindo wa kuokota mayai mara tu kuku anapotaga na kwenda kuyatunza hauwezi kumuathiri hasa pale anapofikia hatua za mwisho wa utagaji?

inawezekana kweli akaatamia bila kuona mayai? au inakuwaje hapo?
 
haimuathili kuku akisha fikia kuanza kuatamia ataenda ile sehemu yake ya kutagia ataanza kulala pale hata kama hakuna mayai, Na ni vizuri kuokota mayai ili yasipate wadudu au kuvunjika lakini akma banda ni zuri na kuna kiota basi unaweza kumuachia mayai yake pale pale haina haja ya kuyatoa
 
Mtaalam kuna sehemu nimeona umetaja incubator...hizi machine zenye ubora zapatikana wapi.
 
endelezeni wandugu tupate somo kwa faida ya wengi.CHASHA NDUGU YANGU TOA SOMO ZIMA TAFADHALI KAMA UNA MUDA.Hasanten
 
Je kwa Mwanza wapi naweza pata incubator ndogo ya mayai kati ya 60 na 100????????? na kwa bei gani?
 
Njia nyingine ni kumtumia kuku kuangua mara mbili mfululizo,yan anapoangua mara ya kwanza unatoa vifaranga immediately kabla hajaamua kutoka navyo alafu unaweka mayai mengine,lakin angalizo uweke kwnza mayai mabovu ili ayazoee alafu ndio unaweka mazima,kwa njia hii utajikuta unatotolesha vifaranga vingi kwa muda mfupi

unawezezaje kutoa vifaranga ....kwani kuku anakuwa kwenye kiota chake Muda wote
 
Kama kuna mhitaji wa mashine tuwasiliane Ninatengeneza kwa gharama nafuu 0754078015
 
Kwanza napenda kuwapongeza kwa maamuzi mliyochukua ya kujiajiri, Pia napenda na mm niongeezee somo kidogo hapa katika hii mada. Kwanza naanza jinsi ya kulea mayai. Mayai katika mazingira ya joto kama dar yanatakiwa kukaa siku zisizo zidi 10 tangu kutagwa kutokana na mazingira ya joto yaliyopo huko. katika mazingira ya baridi yanaweza kukaa add siku 14-16 kama mikoa ya nyanda za juu kusini. pia mayai yanatakiwa kutunza katika tray ikiwa sehem yenye incha kali kuangalia chini na sehem yenye incha butu, kuangalia juu. maana sehem butu nio kitovu cha kifaranga na ni sehemu anayopumulia na kupata hewa kutokea hapo.

Kutotoresha

Unaweza kutotoresha kwa njia ya mashine ama kwa njia ya asili kama kwa kutumia kuku. pia unaweza tumia moto kwa usiku na jua mchana, au kwa kutumia maji ya moto. Hapa nitaelezea siku nyingine kwa undani zaidi.

Kulea Vifaranga

Kuna njia 2 za kulea vifaranga
Njia ya Asili
Njia ya Kisasa

Njia ya Asili- Unaweza tumia mama yake kuvipatia joto kwa usiku na kuviacha vikawa vinatembea nje, kujitafutia vyenyewe chakula. Pia Unaweza tumia box, chungu. au chemli.

Njia ya Kisasa- Unaweza Kuvitunza bandani na kuvipatia chakula, pia kuvipa joto kwa kuviwashia mkaa,ama taa. Au unaweza kuviweka ktika chumba chenye joto ambacho hakiingizi baridi. lakini hii inaweza tumika kwa maeneo kama ya dar. ambayo maximum chumba kinatakiwa kiwe na joto kuanzia 35C. kifaranga kikikosa joto kitapiga kelele sana na joto likizidi kitapiga kelele pia. unatakiwa kukadilia joto ama kuwa na kipima joto kuweza kujua kiac cha joto.

Vifo vya Vifaranga.

Magonjwa na Vifo huviandama vifaranga wa kuanzia wiki moja add mwezi mmoja.
waweza kudhibiti vifo kwa kuwapa chanjo, pia kuwapa dawa inayozuia magonjwa ya kurisi kutoka kwa mama
Aina ya dawa ya kuzuia magonjwa ya kulisi ni ESB3.
Kuzuia magonjwa ya kuambukiza.
Typhod huua sana vifaranga
Unatakiwa kujua kifaranga kinaumwa nn kwa kuangalia manyoya yake ama kinyesi chake.
Kuna kipindi kifaranga kitakunya damu hii nayo huua sana vifaranga.
Vitamin ni nguzo ya mifugo yako.

Pia natoa Huduma ya Kutengeneza Incubator kwa gharama nafuu. kwa swali ama muhitaji tuwasiliane 0754078015
 
namba (2) si kweli. kitaaramu mayai yasizidi siku 14, japo kuku anaweza akatotoa hata mayai 18, aliyo taga mwenyewe. wafugaji wanao fuga kijadi. vijijini, watakubariana na Mimi. kwani huko kuku hutotoa vifaranga vingi tu. nikipata nafasi nitaweka chapisho la kitabu nilicho kitoa (SUA) ili tuelimike ote, nilichelewa kutoa mchango wangu huu kwakuwa nilipigwa BN, asanteni.

Nina kuku wangu anatoka na vifaranga kumi na sita, sasa hii ya siku saba imenipa good time ya kujifunza zaidi.
 
Khasante mkuu BN ni nini na nani wanapga hyo kitu na kwa makosa gani unapigwa BN?,msahada tafadhali
 
unawezezaje kutoa vifaranga ....kwani kuku anakuwa kwenye kiota chake Muda wote

Wala hilo halina shida mkuu. Ni suala la kumuinua tu huyo kuku na kutoa hao vifaranga. Cha msingi hapo ni kwamba unapowatoa hao vifaranga jukumu la kuwalea linakuwa lako na si la mama kuku tena! Vinginevyo watakufa na hasa kutokana na baridi.
 
Nina kuku wangu anatoka na vifaranga kumi na sita, sasa hii ya siku saba imenipa good time ya kujifunza zaidi.

Hongera sana ndugu. Kwako ww ni furaha kwangu ni Maumivu. Mimi nina kuku wangu yy akijitahidi saana anatoka na vifaranga vitano. Kwa upande wa utagaji huwa anataga Mpaka mayai 15
 
Mkuu malila!hongera sana..kuna swali la lishe watu wamelisahau,kuku anayelalia n vyema akajengewa eneo maalum na kupewa chakula cha kutosha ili kufanya asipoteze muda Mwingi kutafuta chakula huku akiacha mayai yakipoa...
 
Jamani nitoeni ushamba katika hili, hivi ni nini huwa kinasababisha kuku asiangue baadhi ya mayai aliyowekewa?? ukiacha suala la yai kutokuwa na mbegu..

Hivi majuzi nilikumbwa..niliwawekea kuki wawili mayai 23. Katika hayo mayai nilipata vifaranga 7 tu..mengine yote viza
 
Swadaktaaaaa..nimepata jibu katika post no. 21 ya Chasha Poultry Farm.. Nitakuwa smart zaidi katika kuandaa mayai na kuku.
 
Last edited by a moderator:
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom