Mbinu ya kuangusha dola ya mamba

Mbinu ya kuangusha dola ya mamba

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
745
Reaction score
1,504
Na. Robert Heriel.

Kupambana na mamba ni jambo gumu sana. Mamba ni miongoni mwa wanyama jamii ya mijusi wakubwa anaishi Majini. Mamba ni moja ya Wanyama hatari tena wajeuri wanaoongoza kwa kuua watu duniani.

Kama utaambiwa utaje viumbe wenye muonekano wa kutisha basi huwezi kosa kumtaja Mamba. Mama ni moja ya Wanyama wenye meno yasiyo na simile. Ni mnyama anayeishi kwa sababu ya uwepo wa wanyama wengine. Ili yeye aishi basi wengine wanapaswa wafe. Ni mnyama mla nyama za wanyama wengine.

Mamba ni Mfalme wa majini. Yeye ndiye Kibopa na Taikon wa Majini. Sura yake imezingizwa na magamba yenye misumari sumari. Hakika Mamba anasura ya kibedui.

Licha ya mamba kuishi majini lakini Yeye hutagia mayai yake nchi kavu. Hahaha! Mamba bhana mjanja sana. Anataga mayai yake karibu na makazi yake yaliyo iwe ni mtoni au ziwani. Hapa ndipo wajanja wanapotupia Macho yao katika kumuangamiza Mamba.

Utawala wa Mama ni utawala wa kibabe na Kiimla. Utawala wa kinyama. Utawala usio na huruma. Unajua mimi nafuatilia sana wanyama na ndege bila kuwasahu samaki. Lakini moja ya wanyama nilionaa karibu kuwafuatilia ni pamoja na huyu bandidu.

Mamba hupata mlo wake kwa shida za wengine. Ili mamba apate mlo basi sharti Kiumbe mwengine awe na shida kama vile Kiu au kutaka kuvuka mto au ziwa. Hapa ndipo utagundua ubandidu wa Mamba. Muda wa huruma hajawahi kuupata.

Nisikuchoshe embu tuone Mbinu kabambe za kuangusha Dola ya Mamba kama ifuatavyo;~.

1. PASUA MAYAI USIHANGAIKE KUMUUA MAMBA.
Kama nilivyosema mamba hutaga mayai yake nchi kavu. Hii ni habari njema kwa adui za Mamba. Ukitaka kuangamiza dola la mamba basi fanya msako wa kutafuta ni wapi alipotagia mayai yake. Ukiyaona mayai yake yapasue bila huruma.

Ikiwa hujayaona maana naye ni mjanja basi tumia njia hii. Nenda porini huko kachukue Kenge wengi alafu kawamwage eneo alilopo huyo mamba. Hahaha! Hapa mamba atakukodolea macho akiwa majini. Kenge ni Askari doria mwenye Degree ya heshima ya msako wa mayai ya adui mamba. Nakuhakikishia hao kenge uliowaleta watamaliza mayai ya huyo mamba.

Ili kumaliza mchezo mzima. Rudi Porini kawinde Tai na Mwewe kisha wamwage wa kutosha eneo hilo. Kama kenge hatabahatika kuyaona hayo mayai mpaka yakaanguliwa basi Tai watadili na vimamba vidogo vitakavyoanguliwa.

Lengo la mbinu hii ni kudhibiti ongezeko la dola la mamba. Ni suala la muda tuu dola la mamba litaanguka rasmi.

Mbinu hii hutumiwa na watu wenye weledi na akili mingi. Hutumiwa katika kumpunguza nguvu adui hapo mbeleni. Kwani hakuna kiumbe kisichozeeka na kuisha nguvu.

Watu wenye akili hupigana na kesho ya adui zao na wala sio leo yao. Huathiri vizazi vya adui zao ili wakijakushtuka hawana nguzo tena.
2. TENGENEZA BWAWA JINGINE PEMBENI LAKINI PAWE MBALI KIDOGO NA MAKAZI YA DOLA LA MAMBA.
Hahaha! Kama namuona mamba atakavyokutumbulia macho. Unajua mamba kwa sehemu kubwa anategemea zaidi nchi kavu ingawa anaishi majini. Kutoka nchi kavu anapata chakula na anaota jua.

Lengo la kutengeneza Bwawa litapunguza idadi ya Wanyama watakao enda kunywa maji anapoishi Mamba. Jambo hili litamfanya Mamba akose chakula na akikosa chakula ni wazi nguvu zitamuisha. Atapambana pambana kula visamaki vya majini lakini kitambo kidogo visamaki vitaisha na hapo ndipo utawala wake utatetereka na kuangamia kabisa.

Huku njaa kule mayai yake umeyapasua au yameliwa na kenge. Vitoto vyake vikianguliwa vinaliwa na Tai au mwewe. Hiyo huitwa ukiinama nchale ukiinuka nchale.

3. INGIA MAJINI UMKAMATE MAMBA.
Hakikisha mamba ananjaa ya kutosha iliyomlegeza hata asiwe na nguvu kabisa. Hapa lazima akukimbie ingawa zamani angekufanya kitoweo. Ukimkaribia unapaswa uzingatie sana. Dili zaidi na mdomo wake maana mamba huringia meno yake. Ingependeza zaidi ukibeba na mti ambao akipanua mdomo unamuwekea. Hahhaha! Mamba kwisha habari yake. Au uchukue kamba umfunge mdomo wake.

Ukifanikiwa jambo hili utaweza mfanya Mamba kuwa Mamba wa maonyesho, unaweza kumuua kisha ngozi yake ukatengenezea mikanda. Mwisho nyongo yake utaiuza kwa watu wenye roho mbaya wakafanye mauaji.

Kufikia hapo Dola ya Mamba itakuwa imedondoka. Kumbuka usitukane mamba ikiwa hujavuka mto. Hiyo ndiyo kanuni kuu ya kupambana na Dola ya Mamba.

Mamba anaweza kuwa mtu yeyote yule ambaye ni adui. Mtu yeyote ambaye hataki unywe maji unapopatwa na Kiu. Mtu yeyote anayeishi kwa kutegemea wewe uumie. Mtu yeyote ambaye hataki uvuke ng'ambo ya mto kimafabikio. Hataki upige hatua yoyote kimaisha.

Mtu yeyote ambaye ukienda kunywa maji unakunywa kwa hofu ukimuogopa huyo ni mamba.

Utawala wa mamba upo kila mahali. Upo katika kila ngazi ya maisha yako. Mamba sharti awe na meno makali mwenye kuogopesha awapo majini au kwenye utawala wake au ofisi yake. Mamba ukifika mahali anapofanyia kazi hupanua mdomo wake ili uogope meno yake.

Sasa nimekupa mbinu za kumkabili ili asikuzuie kuvuka ng'ambo ya mto. Asikuzuie kupiga hatua ya kimaisha.

Kumbuka Hakikisha ukipambana na mamba asijue kama unapambana naye asije kukuzuia kunywa maji ukafa kwa Kiu. Nenda naye kwa akili sana.

Siku utakayomshtukiza ajikute ameachama tuu mdomo alafu wewe uweke Kipande cha Mbao au mti mdomoni mwake. Au mfunge kamba mdomoni.

Usipambane na mamba kama Hujazingatia wala hujachukua tahadhari.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300
 
Kwa hiyo mkuu, unawapa watu mbinu ya kupambana na jiwe? Wewe utakuwa beberu, sio mzalendo na mpiga dili. Yaani unawashauri watu wamshughulikie Daudi Albert, Msiba na wengineo?
 
Mkuu soma alafu uelewe,
 
Scientific observation depicting current political situation,

Lakini mamba hulinda kiota chake na huwa anawahi kwenyekiota siku mayai yanapo anguliwa na kuvihifadhi vifaranga vyake mdomoni mara tu vinapo anguliwa na Kisha kuvipeleka majini

Tai wataambulia vile vilivo chelewa kuanguliwa.

Halafu mamba anaishi vizazi vitano vya mwanadamu, miaka miatatu na kuendelea
 
Chief miaka 300 sio sahihi mzee maana kwa mantiki iyo duniani wangekuwa wamejaa mamba wengi mno tofauti na hali ilivyo sasa!
 
Na. Robert Heriel.

Kupambana na mamba ni jambo gumu sana. Mamba ni miongoni mwa wanyama jamii ya mijusi wakubwa anaishi Majini. Mamba ni moja ya Wanyama hatari tena wajeuri wanaoongoza kwa kuua watu duniani.

Kama utaambiwa utaje viumbe wenye muonekano wa kutisha basi huwezi kosa kumtaja Mamba. Mama ni moja ya Wanyama wenye meno yasiyo na simile. Ni mnyama anayeishi kwa sababu ya uwepo wa wanyama wengine. Ili yeye aishi basi wengine wanapaswa wafe. Ni mnyama mla nyama za wanyama wengine.

Mamba ni Mfalme wa majini. Yeye ndiye Kibopa na Taikon wa Majini. Sura yake imezingizwa na magamba yenye misumari sumari. Hakika Mamba anasura ya kibedui.

Licha ya mamba kuishi majini lakini Yeye hutagia mayai yake nchi kavu. Hahaha! Mamba bhana mjanja sana. Anataga mayai yake karibu na makazi yake yaliyo iwe ni mtoni au ziwani. Hapa ndipo wajanja wanapotupia Macho yao katika kumuangamiza Mamba.

Utawala wa Mama ni utawala wa kibabe na Kiimla. Utawala wa kinyama. Utawala usio na huruma. Unajua mimi nafuatilia sana wanyama na ndege bila kuwasahu samaki. Lakini moja ya wanyama nilionaa karibu kuwafuatilia ni pamoja na huyu bandidu.

Mamba hupata mlo wake kwa shida za wengine. Ili mamba apate mlo basi sharti Kiumbe mwengine awe na shida kama vile Kiu au kutaka kuvuka mto au ziwa. Hapa ndipo utagundua ubandidu wa Mamba. Muda wa huruma hajawahi kuupata.

Nisikuchoshe embu tuone Mbinu kabambe za kuangusha Dola ya Mamba kama ifuatavyo;~.

1. PASUA MAYAI USIHANGAIKE KUMUUA MAMBA.
Kama nilivyosema mamba hutaga mayai yake nchi kavu. Hii ni habari njema kwa adui za Mamba. Ukitaka kuangamiza dola la mamba basi fanya msako wa kutafuta ni wapi alipotagia mayai yake. Ukiyaona mayai yake yapasue bila huruma.

Ikiwa hujayaona maana naye ni mjanja basi tumia njia hii. Nenda porini huko kachukue Kenge wengi alafu kawamwage eneo alilopo huyo mamba. Hahaha! Hapa mamba atakukodolea macho akiwa majini. Kenge ni Askari doria mwenye Degree ya heshima ya msako wa mayai ya adui mamba. Nakuhakikishia hao kenge uliowaleta watamaliza mayai ya huyo mamba.

Ili kumaliza mchezo mzima. Rudi Porini kawinde Tai na Mwewe kisha wamwage wa kutosha eneo hilo. Kama kenge hatabahatika kuyaona hayo mayai mpaka yakaanguliwa basi Tai watadili na vimamba vidogo vitakavyoanguliwa.

Lengo la mbinu hii ni kudhibiti ongezeko la dola la mamba. Ni suala la muda tuu dola la mamba litaanguka rasmi.

Mbinu hii hutumiwa na watu wenye weledi na akili mingi. Hutumiwa katika kumpunguza nguvu adui hapo mbeleni. Kwani hakuna kiumbe kisichozeeka na kuisha nguvu.

Watu wenye akili hupigana na kesho ya adui zao na wala sio leo yao. Huathiri vizazi vya adui zao ili wakijakushtuka hawana nguzo tena.
2. TENGENEZA BWAWA JINGINE PEMBENI LAKINI PAWE MBALI KIDOGO NA MAKAZI YA DOLA LA MAMBA.
Hahaha! Kama namuona mamba atakavyokutumbulia macho. Unajua mamba kwa sehemu kubwa anategemea zaidi nchi kavu ingawa anaishi majini. Kutoka nchi kavu anapata chakula na anaota jua.

Lengo la kutengeneza Bwawa litapunguza idadi ya Wanyama watakao enda kunywa maji anapoishi Mamba. Jambo hili litamfanya Mamba akose chakula na akikosa chakula ni wazi nguvu zitamuisha. Atapambana pambana kula visamaki vya majini lakini kitambo kidogo visamaki vitaisha na hapo ndipo utawala wake utatetereka na kuangamia kabisa.

Huku njaa kule mayai yake umeyapasua au yameliwa na kenge. Vitoto vyake vikianguliwa vinaliwa na Tai au mwewe. Hiyo huitwa ukiinama nchale ukiinuka nchale.

3. INGIA MAJINI UMKAMATE MAMBA.
Hakikisha mamba ananjaa ya kutosha iliyomlegeza hata asiwe na nguvu kabisa. Hapa lazima akukimbie ingawa zamani angekufanya kitoweo. Ukimkaribia unapaswa uzingatie sana. Dili zaidi na mdomo wake maana mamba huringia meno yake. Ingependeza zaidi ukibeba na mti ambao akipanua mdomo unamuwekea. Hahhaha! Mamba kwisha habari yake. Au uchukue kamba umfunge mdomo wake.

Ukifanikiwa jambo hili utaweza mfanya Mamba kuwa Mamba wa maonyesho, unaweza kumuua kisha ngozi yake ukatengenezea mikanda. Mwisho nyongo yake utaiuza kwa watu wenye roho mbaya wakafanye mauaji.

Kufikia hapo Dola ya Mamba itakuwa imedondoka. Kumbuka usitukane mamba ikiwa hujavuka mto. Hiyo ndiyo kanuni kuu ya kupambana na Dola ya Mamba.

Mamba anaweza kuwa mtu yeyote yule ambaye ni adui. Mtu yeyote ambaye hataki unywe maji unapopatwa na Kiu. Mtu yeyote anayeishi kwa kutegemea wewe uumie. Mtu yeyote ambaye hataki uvuke ng'ambo ya mto kimafabikio. Hataki upige hatua yoyote kimaisha.

Mtu yeyote ambaye ukienda kunywa maji unakunywa kwa hofu ukimuogopa huyo ni mamba.

Utawala wa mamba upo kila mahali. Upo katika kila ngazi ya maisha yako. Mamba sharti awe na meno makali mwenye kuogopesha awapo majini au kwenye utawala wake au ofisi yake. Mamba ukifika mahali anapofanyia kazi hupanua mdomo wake ili uogope meno yake.

Sasa nimekupa mbinu za kumkabili ili asikuzuie kuvuka ng'ambo ya mto. Asikuzuie kupiga hatua ya kimaisha.

Kumbuka Hakikisha ukipambana na mamba asijue kama unapambana naye asije kukuzuia kunywa maji ukafa kwa Kiu. Nenda naye kwa akili sana.

Siku utakayomshtukiza ajikute ameachama tuu mdomo alafu wewe uweke Kipande cha Mbao au mti mdomoni mwake. Au mfunge kamba mdomoni.

Usipambane na mamba kama Hujazingatia wala hujachukua tahadhari.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300
Inaelekea Wazee wastaafu mnaelekea kufanikiwa naona mmekuja na mbinu za kijasusi
 
Hivi Mamba huwezi kumzoea kama vile watu wanavyocheza na Simba au Nyoka...?
 
Back
Top Bottom