Mbinu ya kivita ninayoitumia kujizuia kutongoza wasichana barabarani

mpasta

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
917
1,997
Wanajamvi wenzangu mie hapa Jijini DSM nilihamishiwa kikazi nikitokea mkoani. Siku za mwanzoni nilikuwa napata shida barabarani. Kila msichana ninayekutana nae namuona mrembo, haswa nikifika maeneo ya Posta Mpya kule.

Basi Asubuhi kabla sijatoka Home nikawa ninatumia dakika takribani 5 za kumuomba MUNGU aniepushe na vishawishi huko njiani nisiwe na tamaa na wake za Watu na mabinti wa watu. Basi Shetani alivyo mshenzi, ukipanda tu Daladala muda huo huo umetoka kusali analeta bonge la PISI kali akae na wewe kwenye siti moja, afu anakusalimia kwa sauti ya huba.....

Sasa baada ya kuwaza mpango mkakati wa namna ya kujinasua na kutamani vidosho, nikakumbukia tukio la mwanachuo mwenzetu mmoja enzi tupo Chuo KIKUU la kuachwa na mpenzi wake dakika za majeruhi kabla hatujamaliza Chuo. Jamaa alichanganyikiwa nusra ajitoe uhai. Yule dada aliyemtosa mwenzetu akaenda kuolewa na jamaa mwingine ambaye hakukaa nae sana, dada alifariki kwa uzazi.

Hivyo jamaa aliyetoswa huzuni ikaondoka akaanza kuwaza huenda angemuoa yeye sasa nae angekuwa ni Mgane aliyefiwa na mkewe. Hivyo tukawa tukikutana nae jamaa kauli yake, anasema "Unaweza kupenda jambo kumbe lina Shari na wewe na unaweza kuchukia jambo kumbe lina heri na wewe, Mungu ndio mjuzi wa yote".

Sasa hiyo mbinu nikaanza kuitumia, nikikutana na demu mkaliii barabarani naanza kumuwazia mabaya nafsini mwangu. Naweza kuanza kujisemea "Ooh huenda ana U.T.I sugu huyu demu anatafuta wa kumuambukiza", au naweza kusema huyu huenda ni kikojozi kitandani, au huenda ana mikosi ya urithi huyu,ukitembea nae tu nitajivika mabalaa kwenye maisha yangu yote...

Nashukuru Mungu huu mbinu ya kivita imenisaidia sana, sasa nina mwaka wa 6 DSM hii licha ya kujazana warembo kila kona nipo njia kuu sichepuki. Nikitoka Job mazoezi nikitoka mazoezi Home na Issue zangu binafsi...

Nyie wenzangu mnatumia mbinu gani za kivita?? karibuni kuchangia mada....
 
st,small,845x845-pad,1000x1000,f8f8f8.jpg
 
Wanajamvi wenzangu mie hapa Jijini DSM nilihamishiwa kikazi nikitokea mkoani. Siku za mwanzoni nilikuwa napata shida barabarani. Kila msichana ninayekutana nae namuona mrembo, haswa nikifika maeneo ya Posta Mpya kule. Basi Asubuhi
Kufanya mazoezi kila siku na kuzingatia muda,muda ndo kila kitu.
 
Kuna jamaa yangu aliwahi kuniambia kuwa..."Glenn ukikutana na mrembo sana na akataka kuvuta hisia...jisemee moyoni mwako; " chui huyoo" ili usianze kumuwazia" haha
 
Sema Ukweli tuu Bro.Hela huna sasa hivi....Hii vita Tutaona rangi zote miaka hii.
Ukweli sina pesa, ila mie mchakarikaji sana kitaa, nakopa kwa kutumia Salary yangu nafanya mambo, licha ya mikopo lakini bado Salary yangu inasoma digit 8, sio masihara kwa serikalini kuwa na mikopo au bado unasoma digit 8
Hivyo za kuhonga ndogo ndogo haziwezi kunishinda labda hiyo ya kununuliana magari kama HARMONIZE ndio siwezi
Screenshot_20220621-144918.jpg
 
Ukweli sina pesa, ila mie mchakarikaji sana kitaa, nakopa kwa kutumia Salary yangu nafanya mambo, licha ya mikopo lakini bado Salary yangu inasoma digit 8, sio masihara kwa serikalini kuwa na mikopo au bado unasoma digit 8
Hivyo za kuhonga ndogo ndogo haziwezi kunishinda labda hiyo ya kununuliana magari kama HARMONIZE ndio siweziView attachment 2267679
Daaah.. Mkuu unakula maisha..
 
Naona unafanya kazi wizara ya fedha mkuu, hongera
 
Ukweli sina pesa, ila mie mchakarikaji sana kitaa, nakopa kwa kutumia Salary yangu nafanya mambo, licha ya mikopo lakini bado Salary yangu inasoma digit 8, sio masihara kwa serikalini kuwa na mikopo au bado unasoma digit 8
Hivyo za kuhonga ndogo ndogo haziwezi kunishinda labda hiyo ya kununuliana magari kama HARMONIZE ndio siweziView attachment 2267679
Hivi kumbe Tayari,Hongera mkuu ngoja niende Bank
 
Wanajamvi wenzangu mie hapa Jijini DSM nilihamishiwa kikazi nikitokea mkoani. Siku za mwanzoni nilikuwa napata shida barabarani. Kila msichana ninayekutana nae namuona mrembo

Hapa ni ushamba tu ndio lilikuwa tatizo
 
Ukweli sina pesa, ila mie mchakarikaji sana kitaa, nakopa kwa kutumia Salary yangu nafanya mambo, licha ya mikopo lakini bado Salary yangu inasoma digit 8, sio masihara kwa serikalini kuwa na mikopo au bado unasoma digit 8
Hivyo za kuhonga ndogo ndogo haziwezi kunishinda labda hiyo ya kununuliana magari kama HARMONIZE ndio siweziView attachment 2267679
Duh! PAYE laki tano!!? Kweli watu wana mishahara mizito

Anyways ni 7 digits mzazi siyo 8 digits
 
Back
Top Bottom