Mbinu kuu ya TeamLowassa hii hapa

Mbinu kuu ya TeamLowassa hii hapa

Lowassa ni mwanasiasa mbobezi. Ni mwanasiasa aliyelelewa,kuiva na kujiimarisha ndani ya CCM. Ni kati ya wanasiasa ambao wamefanikiwa kuunda mfumo kupitia wafuasi na wanaowaunga mkono. Kama Mwenyekiti Mstaafu Kikwete alivyokiri,Lowassa si wa kubezwa.

Ingawa Lowassa anahusishwa na wizi na ufisadi,wapo wanaoamini ni msafi,mwema,imara na mwenye uwezo wa kuongoza. Wanamuunga mkono wapo vyama vyote. Ndiyo mfumo wenyewe alioujenga. Binafsi,nambeza kwa tahadhari kubwa. Simtenganishi na ufisadi hasa wa Richmond. Lakini,ana nguvu ya kimfumo.

TeamLowassa sasa ina mbinu ya ukimya. Kimyakimya. Hawajitaji kimahitaji na kuvuliwa taji. Wako kimya. TeamLowassa wamejipenyeza kwenye teuzi mbalimbali serikalini kimyakimya.

Kwa ilivyotapakaa TeamLowassa, isingewezekana teuzi ziwaruke wote viunzi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hata wakiwepo hawanayo mikia, wameishakatika wote.
 
Kaka nisamehe mie "Msukuma naandika kama tnavyoongeaga kwa herufi kubwa"....

Mungu akinijaalia lafudhi yangu ikibadilika na mie nitabadilika.....Ungekuwapo karibu nami navyotypekwenye keyboard utadhani naigonga kwa nyundo....Full nguvu na shibe...Hapakazi na kasi tuu.
Wamwise acha vituko.. Mtazamo wako kwa asilimia kubwa ni uhalisia, naamini hata Mkulu analijua hilo, isipokuwa hana jinsi. Hajawajua wanasiasa, ndiyo maana juzi akikabidhiwa "wadhifa" ameingia kichwakichwa na kutengeneza Msemo mgumu sana kisiasa. Impact ya huo msemo atakumbana nayo kila siku ktk maisha yake ya Ukulu.......ni mtazamo tuuu.
 
Back
Top Bottom