Nyufa kuu kumi zinazoiathiri Jamhuri ya Tanganyika

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Jamhuri ya Danganyika ni Jamhuri ambayo kaskazini imepakana na Upepo wa Kisulisuli, Mashariki kuna bahari ya moto, kusini kuna Korosho za mawe na Kaskazini kuna Mlima mkubwa sana wa Volcano ya Umasikini.
Watu wake ni wapole mithili ya kondoo, lakini viongozi wake ni wakali wenye tamaa na uchu mkali!.

Jamhuri hii ilikuwa katika njia njema kidogo yenye matumaini, lakini sasa mambo ni shaghalabaghala, ukilala ukiamka hujui kuna tamko gani.

Kwa uchunguzi wangu Jamhuri hii ina nyufa zifuatazo ambazo ndizo zinaifanya leo Jamhuri hii iwe kituko mbele ya Mataifa ya Galaxy hii ya S-321

1. Ukurupukaji uliokubuhu

Mfalme wa Kudanganyika akiamka akijisikia tu kutoa tamko anatoa tu bila kukaa na kutafakari kwa kina, Social, Economical hata Political impact ya maamuzi yake ya papo kwa papo. Kwa mfano, Mfalme wa Kudanganyika kaamka siku hiyo Katangaza tu kuwa anahamisha serikali kwenda kwenye Mji mkuu wa nchi hiyo, Mji wa Mizabibu!. Miundo mbinu kule haijakaa sawa, Watu hawana ofisi za kutosha, bajeti ya kujenga ofisi hiyo haikuwepo, Yeye mwenyewe bado mpaka leo yupo katika ule mji wa bandari ya Salama anapunga tu upepo wa bahari ya moto!. Athari za jambo hili, Uchumi wa bandari salama unaochangia pato la Taifa hilo kwa zaidi ya asilimia 65 umeyumba na hata makusanyo yake kuyumba.

2. Bunge na Mahakama ya nchi ya Danganyika vimepwaya

Leo hii Mfalme wa kudanganyika anatoa maagizo tu kuwaambia wakuu wa mihimili hii kuwa fanya hiki, fanya kile, Leo hii katika nchi ya Danganyika ukipeleka kesi nzito dhidi ya serikali, Majaji wanakukimbia ili wasiisajili, Wakati mwingine wanaipiga chini fasta kwa visingizio kuwa haikufuata taratibu, Hata Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi hiyo anazuiwa kutoa hotuba kwenye siku ya sheria ya nchi hiyo ili tu wakubwa hawa wa Mfumo wa Mahakama wasimuudhi Mfalme Mwema wa nchi ya Kudanganyika. Infact Mfalme alishajitangazia kuwa Yeye Mhimili wake Umejichimbia parefu sana kwenye Ugiligili wa nchi ya Danganyika.

3.Dalili za kansa ya Udini inayoitafuna nchi ya Danganyika chini kwa chini.

Katika Danganyika Mfalme hufanya teuzi mbalimbali, lakini ukiwa msomi wa Fani ya SOSHOLOJIA ( Elimu ya Jamii) utashangazwa kweli na vigezo vinavyotumika katika kuteua watu wanaohudumu katika nchi hiyo. Kikawaida Misingi ya Sosholojia inasema, Ili nchi iwe na Harmonony basi lazima nguvu zote za kidemografia za watu zizingatiwe katika utumishi wa nchi husika. Lakini cha ajabu mfalme wa Danganyika kila akiteua watu wa kumsaidia kazi , basi utakuta mara zote watu wa Dini moja ndiyo Wengi!.Kiasi kwamba unajiuliza hivi katika watu wa dini nyingine hakuna watu competent na wa kutosha kushika nafasi kwa wingi kama wale wenzao, mbona inaonekana kama vile kuna formula fulani hivi inafuatwa katika teuzi hizi? Hali hii inafahamika vyema, lakini cha ajabu mfalme kaweka pamba masikioni.

4. Kutokuheshimu Katiba na Sheria.

Katika nchi ya Kudanganyika, tamko la mfalme ni kama sheria, akisema hakuna kufanya hiki hata kama ni haki ya mtu ndani ya katiba, basi hilo linabebwa kuwa ni sheria, mfalme akisema hakuna kufanya shughuli fulani ambayo ni rukhsa kikatiba na kisheria, basi tamko lake linakuwa juu ya katiba na hilohilo ndo linatekelezwa!

5. Taasisi dhaifu na one man show.

Katika nchi ya Danganyika, Taasisi za nchi hiyo ni dhaifu, badala ya kuwezesha taasisi ziwe imara, mara kibao mfalme kajikuta akiingilia kati kurekebisha hili au kutoa tamko lile. Taasisi hizi badala ya kufanya kazi kwa weledi, zinafanya kazi kwa kuviziavizia. Kuna rais mmoja katika nchi moja iliyoko katika Milkyway Galaxy katika Solar System, Sayari ya Tatu kutoka kwenye Jua alisema, Nchi za bara moja masikini katika Sayari hiyo hazihitaji Mtu mwenye Nguvu, bali zinahitaji TAASISI zenye nguvu. Bahati mbaya Danganyika ya Leo ina mfalme anayeamini kuwa yeye ndiye nchi na nchi ni yeye, mifimo ya Taasisi za Danganyika ni.midogo sana

6. Serikali ya Danganyika inaamini katika VITU kuliko WATU

Leo hii Danganyika inajenga mabarabara makubwamakubwa katika Jiji lake, inajenga Madaraja ya Juu wao wanayaita Flyovers, Wanajenga barabara inayopita baharini LAKINI wakati huohuo kuna maelfu ya wanafunzi wameshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa uhaba wa madarasa, Kuna wanafunzi wamekosa mkopo kysoma elimu ya juu licha ya ufaulu mzuri, kuna shule zinaendeshwa chini ya Mwembe!

7. Danganyika hailei mbegu ikakomaa hadi kuwa mti wa matunda.

Leo hii katika nchi ya Kudanganyika, mbegu ikichipua tu tayari ufalme wa kudanganyika umeshafika kuzengeazengea, nchi ya Danganyika inatoza kodi kubwa kiasi kwamba Wafanyabiashara biashara zao haziwezi kukua na hatimaye kuwa wafanyabiashara wakubwa, badala ya nchi ya Danganyika kutengeneza walipa kodi wakubwa wa kesho yenyewe inang'ang'ana na wachuuzi wa leo na kuwaua kabisa kibiashara kabla hawajainuka na kuwa wafanyabiashara wakubwa. Leo Wakulima wa Zao la Korosho za Mawe walipojikusanyia tubilioni 200 tuwasaidie kuboresha zao lao kwa kununua pembejeo, utafiti , elimu n.k. Ufalme wa kusadikika ukaitolea mate ile hela, matokeo yake hali ya zao husika mustakbali wake haueleweki!

8. Danganyika haina muendelezo wa mipango.

Leo hii Wadanganyika watasema Kilimo Kwanza, Maika miwili baadae watasema Viwanda, baada ya miaka miwili hawasemi viwanda tena bali wanazungmzia Miundo mbinu kwanza itakayowezesha Viwanda huko mbeleni!. Wadanganyika wataambiwa sasa ni umeme wa gesi, kesho wataambiwa ni umeme wa maji!. Leo watasaini mkataba na nchi ya wachina kujenga reli, Kesho watabadirisha watasaini na mturuki, halafu sasa ni serikali hizohizo za chama kilekile kinachotawala Danganyika!. Muendelezo hakuna!

9. Siasa duni, batili na za kijinga

Katika nchi ya Danganyika, mwanasiasa anaweza kujiuzulu uwakilishi katika jimbo fulani, kisha akamuunga mkono mfalme, na kisha akateuliwa na mamlaka ziliozoteuliwa na mfalme kugombea katika jimbo lilelile, Kodi za wananchi wa Danganyika zikatumika tena, Mgombea akashindishwa na kisha akirudi katika Jengo la uwakilishi anageuka kasuku sasa wa kumwaga sifa juu ya mfalme, kuunga mkono miswada iliyoletwa na mfalme!. Wakati haya yakifanyika, Danganyika inanuka umasikini uliokubuhu!. Badala ya pesa kutumika kujenga shule zinatumika kugharamia chaguzi za waunga juhudi!

10. Elimu duni ya Wadanganyika

Wadanganyika kiukweli wengi wao hawajui nchi yao inakwendaje, badala ya kuhoji ili waongozwe, wao wamekubali kuswagwa!. Badala ya kuhoji matumizi ya kodi zao katik ufalme wao, wao wanasema kwani nikihoji ndo nitaletewa ugali mezani?. Badala ya kuwa ni Citizens wao wamegeuka kuwa Subjects. Watawala wa Danganyika wanalijua vizuri hili suala, na ndiyo sababu huamua kufanya mambo with impunity, watawala wa Danganyika kwa kupendezwa na hii hali ya Jamii iliyolala wameamua kurasimisha hali hii kupitia sheria, Wameunda sheria ya Takwimu ili Umma usiwe huru kupata Data huru na kuchalenge wanachoambiwa. Ili Wadanganyika wasiamshwe kupitia social media imewekwa sheria kali ya mitandao ya kijamii. Ili wasiamshwe kupitia harakati za muziki kuna chombo cha kupitia mashairi ili kama ufalme wa Danganyika umesemwa basi mashairi hayo yazuiwe. Sasa Hii fungakazi ufalme wa Danganyika umeamua kuwa ili umma usije ukainuka na kuutoa madarkani basi viundwe vyama dhaifu vya upinzani ambavyo msajili ambaye ni mteuliwa wa mfalme ataweza kuviingilia na kuvigeuzageuza kama chapati kadri impendezavyo mfalme.

Hii ndo hali halisi ya nchi ya Danganyika!. Kama Danganyika itaendelea kuzilea nyufa hizi basi kamwe haitopiga hatua yoyote ya maendeleo, itaendelea kupiga Marktime tu
 
Hahaaa. Kweli we unajua kuchambua nchi ya waliodanganyika. Ila umesahau kimoja. Mwanzoni wale walioitwa wasiojulikana siku hizi tunawatambua kwa kauli zao dhidi ya yule waliotaka kumuua!
 
Hoja ya 5 ndiyo imebeba sehemu kubwa ya hoja zako. Taasisi Imara ndiyo hufanya nchi iwe na msingi imara kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Hufanya siasa ziwe zinatabirika, Sera kuu za nchi kuwa na mwelekeo na Sheria za nchi kuweza kuheshimiwa.

Hoja ya 6 ni pana sana na ni moja ya jambo ambalo nimekuwa nikilisema humu mara kwa mara. Tunahitaji maendeleo ya watu kwanza: Elimu bora, Huduma bora za afya, Utoaji mzuri wa haki za binadamu, Usawa baina ya mwanamume na mwanamke etc. Treni na Ndege haziwezi kutusaidia nchi kupata hivi vitu moja kwa moja. Lakini upande wa pili, serikali lazima ikubali kwamba haiwezi kuwafanyia watu vitu vyote au kuwa The Nanny Government. Inachotakiwa kufanya ni kuruhusu uhuru wa kifikra, uhuru wa kiuchumi na uhuru wa kisiasa kwasababu sehemu kubwa ya maendeleo huletwa na wananchi wenyewe.

Hoja ya 10 nayo imemeza hoja zako nyingi.
Elimu duni ni changamoto sana kwa watanganyika: Tena ni duni kuanzia kwa watawala hadi watawaliwa. PhD na Masters za Tanganyika hazina umaana wowote ule. Kama mtu mwenye PhD yuko radhi kuvua usomi wake na kufuata kile ambacho kiongozi wake wa dini anakisema au mganga wa kienyeji anakisema huku akijua dhahiri ni kitu kibaya unategemea kwamba hilo ni taifa la wasomi kweli ? AU mtu mwenye PhD kukubali kuendeshwa na mtu aliyefeli kidato cha nne kisa tu ni kiongozi wa chama unadhani kunaleta matokeo chanya kwenye taifa ?

Sasa elimu duni ndiyo imetuletea siasa uchwara na wanasiasa uchwara. Tukiweza kurekebisha elimu hapa Tanzania basi naamini asilimia 50 ya matatizo yeti itakuwa imesuluhishwa. Lakini haiwezi tokea kwasababu ujinga na upumbavu wa watanganyika ni mtaji mkubwa wa kisiasa kwa baadhi ya watu
 
Mfalme wa Danganyika yuko bize kweli kweli anakata tawi la mti alioukalia .

Ila nimemuangalia mfalme, nimemuangalia kuanzia machoni hadi namna ya utembeaji,namna ya gestures anazozifanya, ni tofauti kabisa na Zamani, mfalme anaonekana kuanza kupoteza Mojo na Energy. Ni vyema wadanganyika wakaelezwa ni kitu gani haswa kinamsibu mfalme, Je ni msongo wa mawazo au anaumwa?
 
Danganyika ni kama mtoto yatima asie na mwenyewe.

Wadanganyika wanapigika vibaya sana huku mfalme hana habari kabisa!

Wadanganyika ndani ya miaka 3 au 5 ijayo, wanaweza kuwa wanakosa hata basic needs na huo ndio utakuwa mwanzo wa wao kupingana na watawala wao kama ilivyotokea katika mataifa mengine duniani.
 
Back
Top Bottom