Mbezi Mwisho palivyonitoa ushamba

Mbezi Mwisho palivyonitoa ushamba

Hamna kitu mkuu, pale wanatumia uzoefu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni barabara ambayo karibia kila siku ya kazi, napita, ukitokea kibamba kabla ya kona ya kwenda standy kibao kipo upande wako wa kushoto, na kila penye mkanyiko kibao kipo, ila madereva hatusomi alama za barabatani tu.
 
Halafu polisi wamefanya mtaji, ukikosea ukaingia stand ya daladala wanakukamata
Kama wanafanya hivyo wanakosea, wanatakiwa kukuelekeza tu, maana wakikuchukua pesa hawezi kukuelekeza tena, wanachukulia umefanya makusudi.
 
Nikiwa na safari ya Mbezi lazima nitumie dereva.
Sitaki sitiresi mie.
Hapana kutoendrsha gari mwenyewe, kutakufanya uendelee, kutojua hizo njia, nimeona baadhi ya madereva wenye magari yao huko kibaha, wanaogopa kwenda na gari zao mjini.
 
Well binansi nna tabia ya kuendesha kwa mazoea bila kusoma maelekezo mapya.

Kuna siku nilikuwa namuwahisha mtu stendi ya Magufuli awahi basi la kuondoka saa moja 12 alfajiri. Niko ndani ya muda vizuri tuu nilikuwa natokea Ubungo.

Hapo sijapita maeneo hayo kama miezi 2, niliacha ukitoka Ubungo kwenda stendi ya Magufuli unaweza kuchepuka kushoto ukaingia round about halafu unavuka barabara kisha ukate kushoto kuelekea stendi.

Ila ikiwa mida ambayo sio busy unaweza ukakunjia pale pale kona uingie upande kama unaenda Goba ukitokea Ubungo kitu ambayo ni makosa.

Kwakuwa ilikuwa alfajiri magari si mengi nikajisemea wacha nikatishe nisiende kwenye round about weeehh.....picha likaanzia hapo.... kufika pale pamezibwa nikiwa nashangaa shangaa gari ya nyuma ikanistua kwa honi ikabidi niende mbele....

Sasa nikaanza kupaniki ili niingie stendi upande wa pili navukaje hapo sasa hata maandishi ya kwenye vibao vinavyofuata sioni nikiangalia saa naona muda unakimbia dabodabo, abiria nae anayesafiri akazidi kunipanikisha ntaachwa na gari.....aahahhaaa sitasahau.

Nilienda mbele hadi nakaribia sijui mataa ya wapi kule nshavuka na daraja la mbele huko la waenda kwa miguu yaani sioni pa kugeuzia nikitaka kukata kushoto barabara hairudi yaani sina hamuuu.

Nilipogeuga sasa narudi nna hasiraaa wangu wangu kidogo nikamatwe na askari kwa kupita taa nyekundu....

Ndo kukatisha kushoto kabla ya stendi na kupita round about 2 sijui 3 ndo kukuta basi dereva keshakaa anataka kuamsha safari ianze.

Uzuri msafiri hakuwa na mizigo ya kuweka kwenye buti. Hatukupata hata wasaa wa stori za kuagana... kikubwa kawahi usafiri mie huyooo nikajirudia zangu Mbagala, sina hamuuu....

Pole mtoa mada.... umenikumbusha yaliyonisibu.
Pale ukikosea kama unatoka mjini, unaenda mpaka kwa Yusufu, unakunja kushoto raund about, inakunja kushoto, utaifuata barabara ya juu, mpaka upande wa pili, hatimae magufuri.
 
Mbezi Pana round about 12 . Ukikosea kidogo umeenda Gonna au Mpiji
 
KWANINI WANAKAWIA KUWEKA MABANGO YENYE ALAMA(DIRECTION)
WALITAKIWA WAWE WASHAWEKA MUDA TU

ova
Vibao vipo vinaonesha kwa kwenda kila round about inakwambia huku wapi huku wapi tatizo madereva wengi wao wanangalia mbele tu ka maroboti...
 
Pale ukikosea kama unatoka mjini, unaenda mpaka kwa Yusufu, unakunja kushoto raund about, inakunja kushoto, utaifuata barabara ya juu, mpaka upande wa pili, hatimae magufuri.

Hiyo niliipita kwa wenge na kupanik sababu nilikuwa Lane ya kulia kuja kustuka nshaipita na siwezi ku reverse.....

Nilienda kugeuza mbele hukooo yaani sina hamu....😔😔
 
Hiyo niliipita kwa wenge na kupanik sababu nilikuwa Lane ya kulia kuja kustuka nshaipita na siwezi ku reverse.....

Nilienda kugeuza mbele hukooo yaani sina hamu....
Pole
 
Well binansi nna tabia ya kuendesha kwa mazoea bila kusoma maelekezo mapya.

Kuna siku nilikuwa namuwahisha mtu stendi ya Magufuli awahi basi la kuondoka saa moja 12 alfajiri. Niko ndani ya muda vizuri tuu nilikuwa natokea Ubungo.

Hapo sijapita maeneo hayo kama miezi 2, niliacha ukitoka Ubungo kwenda stendi ya Magufuli unaweza kuchepuka kushoto ukaingia round about halafu unavuka barabara kisha ukate kushoto kuelekea stendi.

Ila ikiwa mida ambayo sio busy unaweza ukakunjia pale pale kona uingie upande kama unaenda Goba ukitokea Ubungo kitu ambayo ni makosa.

Kwakuwa ilikuwa alfajiri magari si mengi nikajisemea wacha nikatishe nisiende kwenye round about weeehh.....picha likaanzia hapo.... kufika pale pamezibwa nikiwa nashangaa shangaa gari ya nyuma ikanistua kwa honi ikabidi niende mbele....

Sasa nikaanza kupaniki ili niingie stendi upande wa pili navukaje hapo sasa hata maandishi ya kwenye vibao vinavyofuata sioni nikiangalia saa naona muda unakimbia dabodabo, abiria nae anayesafiri akazidi kunipanikisha ntaachwa na gari.....aahahhaaa sitasahau.

Nilienda mbele hadi nakaribia sijui mataa ya wapi kule nshavuka na daraja la mbele huko la waenda kwa miguu yaani sioni pa kugeuzia nikitaka kukata kushoto barabara hairudi yaani sina hamuuu.

Nilipogeuga sasa narudi nna hasiraaa wangu wangu kidogo nikamatwe na askari kwa kupita taa nyekundu....

Ndo kukatisha kushoto kabla ya stendi na kupita round about 2 sijui 3 ndo kukuta basi dereva keshakaa anataka kuamsha safari ianze.

Uzuri msafiri hakuwa na mizigo ya kuweka kwenye buti. Hatukupata hata wasaa wa stori za kuagana... kikubwa kawahi usafiri mie huyooo nikajirudia zangu Mbagala, sina hamuuu....

Pole mtoa mada.... umenikumbusha yaliyonisibu.
Ukichelewa kujua pa kuingilia inakubidi ukageuze kwenye mataa yanayofuatia ambapo ni Mbezi kwa Msuguri au Luguruni.
 
Tatizo ni udereva wa kukariri, hatuangalii vibao, tunaendesha kwa mazoea. Mbezi panajieleza sana. Kwa sisi tunaopita hapo daily hakuna shida, mgeni lazima usome vibao la sivyo utazunguka sana hasa kama unatokea Town unaenda goba, unatokea goba unaenda kinyerezi, unatokea kibaha unaenda kinyerezi, unatokea kinyerezi kuelekea goba au mpigi nk.
Hakuna vibao pale.

Labda waweke leo.
 
Ukichelewa kujua pa kuingilia inakubidi ukageuze kwenye mataa yanayofuatia ambapo ni Mbezi kwa Msuguri au Luguruni.

Yaani mimi hayo yote niliyavuka, nilipaniki kuliko kupaniki kwenyewe....

Nilienda kugeuzia mbele hukooo... hata sijui wapi..
 
Hakuna vibao pale.

Labda waweke leo.
Vibao vipo, hata leo asubuhi nimepita pale ukitoka Goba roundabout ya kwanza ina vibao, roundabout ya pili ina vibao...
 
Hope mko salama

Nina muda mrefu sana sijapita Mbezi Mwisho nikiwa nadrive mwenyewe.

Sasa leo nmetoka Kibaha uelekeo ukiwa ni Tabata na lengo nipite hii njia ya Maramba Kinyerezi kisha Tabata. Nilipofika Mbezi Mwisho pale ile sijui niite ni round about au ni kitu gani.

Nimehangaika sana yani, mwisho wa siku nikafanikiwa baada ya mahangaiko mengi.

Ugeni na ushamba wa barabara hii umechangia lakini pia hapo kuna jambo itabidi lifanyike maana kinachotumika kwa madereva hapa ni uzoefu tu.

Serikali inaweza ona namna ya kuweka interchange hapo hapo
Shida husomi mabango ya maelezo na usomi alama za barabarani. In short wewe sio dereva bali mshika uskani
 
Back
Top Bottom