Mbezi Mwisho palivyonitoa ushamba

Mbezi Mwisho palivyonitoa ushamba

Ni kweli pale pamekaa complicated sana, mimi kuna siku nilikuwa naenda huku Mbezi Maramba Mawili kwenye msiba natokea njia ya Goba, nilishazoea ukifika pale Mbezi mwisho baada ya round about unanyoosha moja kwa moja unavuka unaendelea na safari.

Nilivyofika pale kucheki pamezibwa kabisa, ikabidi nizunguke ile round about nielekee kama naenda stand ya Magufuli, shida nikaja nikaingia kwenye hili daraja la kwanza pale ambalo linaelekea stand ya daladala. Baada ya kuvuka tu kuna round about nyingine pale nikazunguka kama mara 3 hivi najaribu kutafuta exit ya kuelekea maramba mawili sioni, nikaona kuna entry moja inakuja toka uelekeo huo na haishuki, nyingine inaenda stand ya daladala, na moja inarudi barabara kubwa.

Ikabidi tu nirudi hadi barabara kubwa alafu ninyooke mpk kwa Yusuph ndiyo nikunje kushoto nitembee. Kifupi pale hapana maelekezo ya kutosha na yanachanganya kinoma, na traffic wamejaa pale wanasubiri ujichanganye wale kichwa. Nilivyofika kuwauliza wenyeji wangu wakanielekeza vizuri ambapo kimsingi nilitakiwa kuvuka kwenye daraja la pili baada ya kupita stand ya Magufuli ukiwa unatokea uelekeo wa Goba.
Pole sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbona vibao vipi pale 100Meter kabla hujaingia kwenye barabara zinazoachana vikielekeza uelekeo? Wewe sema hukuzingatia vibao, ukatumia uzoefu kumbe njia za kuchepuka ukawa umeshazipita
Kuendesha kwa uzoefu mkuu,na presha kukosea vikazidi kunichanganyw

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hope mko salama

Nina muda mrefu sana sijapita Mbezi Mwisho nikiwa nadrive mwenyewe.

Sasa leo nmetoka Kibaha uelekeo ukiwa ni Tabata na lengo nipite hii njia ya Maramba Kinyerezi kisha Tabata. Nilipofika Mbezi Mwisho pale ile sijui niite ni round about au ni kitu gani.

Nimehangaika sana yani, mwisho wa siku nikafanikiwa baada ya mahangaiko mengi.

Ugeni na ushamba wa barabara hii umechangia lakini pia hapo kuna jambo itabidi lifanyike maana kinachotumika kwa madereva hapa ni uzoefu tu.

Serikali inaweza ona namna ya kuweka interchange hapo hapo
Ni ugeni tu lakini madaraja yaliyowekwa yanatosha kabisa na infact hakuna jam kabisa.

Na uwepo wa madaraja mawili imesaidia maana ukikuta sehemu ya kwanza imejaa unaenda sihemu ya pili na hii ilipaswa kuwepo kwenye design ya ujenzi tangu mwanzo.

Kwa upande wa pale kibaha na mlandizi na miji mingine wapange kuwa na miundombinu hiyo wanapoendelea na ujenzi wa njia hiyo
 
Ni ugeni tu lakini madaraja yaliyowekwa yanatosha kabisa na infact hakuna jam kabisa.

Na uwepo wa madaraja mawili imesaidia maana ukikuta sehemu ya kwanza imejaa unaenda sihemu ya pili na hii ilipaswa kuwepo kwenye design ya ujenzi tangu mwanzo.

Kwa upande wa pale kibaha na mlandizi na miji mingine wapange kuwa na miundombinu hiyo wanapoendelea na ujenzi wa njia hiyo
Kilichonitesa ni kuendesha kwa mazoea bila kuchungulia vibao,japo navyo sio vikubwa sana,pia ugeni na barabara hasa kutokujua huko mbele pakoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaaaaaaaaa, daaaah, umenichekesha sana aisee,

Anyway ndo njia yangu everyday, na nimebahatika kushuhudia mabadiliko yooooote yanavyotokea, ila kuna siku nilijisemea Hizi njia kama mtu hajapita loooong time lazima aipate fresh !

Pole aisee
Daraja la kwanza kama unatokea goba ukifika kwenye round about wengi ujichanganya wanakata kulia,kulia atatokea stendi ya daladala kule ukiingia kutoka ni jero au atokee njia kutokea malamba mawili ambayo inaenda tu airudi,wazee wa fursa uwa wanajificha chini ya daraja pale na vest zao 🦺 😃,ukijichanganya wanasema na wewe
 
Well binansi nna tabia ya kuendesha kwa mazoea bila kusoma maelekezo mapya.

Kuna siku nilikuwa namuwahisha mtu stendi ya Magufuli awahi basi la kuondoka saa moja 12 alfajiri. Niko ndani ya muda vizuri tuu nilikuwa natokea Ubungo.

Hapo sijapita maeneo hayo kama miezi 2, niliacha ukitoka Ubungo kwenda stendi ya Magufuli unaweza kuchepuka kushoto ukaingia round about halafu unavuka barabara kisha ukate kushoto kuelekea stendi.

Ila ikiwa mida ambayo sio busy unaweza ukakunjia pale pale kona uingie upande kama unaenda Goba ukitokea Ubungo kitu ambayo ni makosa.

Kwakuwa ilikuwa alfajiri magari si mengi nikajisemea wacha nikatishe nisiende kwenye round about weeehh.....picha likaanzia hapo.... kufika pale pamezibwa nikiwa nashangaa shangaa gari ya nyuma ikanistua kwa honi ikabidi niende mbele....

Sasa nikaanza kupaniki ili niingie stendi upande wa pili navukaje hapo sasa hata maandishi ya kwenye vibao vinavyofuata sioni nikiangalia saa naona muda unakimbia dabodabo, abiria nae anayesafiri akazidi kunipanikisha ntaachwa na gari.....aahahhaaa sitasahau.

Nilienda mbele hadi nakaribia sijui mataa ya wapi kule nshavuka na daraja la mbele huko la waenda kwa miguu yaani sioni pa kugeuzia nikitaka kukata kushoto barabara hairudi yaani sina hamuuu.

Nilipogeuga sasa narudi nna hasiraaa wangu wangu kidogo nikamatwe na askari kwa kupita taa nyekundu....

Ndo kukatisha kushoto kabla ya stendi na kupita round about 2 sijui 3 ndo kukuta basi dereva keshakaa anataka kuamsha safari ianze.

Uzuri msafiri hakuwa na mizigo ya kuweka kwenye buti. Hatukupata hata wasaa wa stori za kuagana... kikubwa kawahi usafiri mie huyooo nikajirudia zangu Mbagala, sina hamuuu....

Pole mtoa mada.... umenikumbusha yaliyonisibu.
Ha ha ha pole sana
 
Itabidi nijaribu tena siku nyingine, maana Hadi sasa nilibadilisha njia, nikienda Tabata napita Mwenge via Ubungo.
Rahisi sana, ukitoka Goba kuelekea Tabata nenda hadi upite stand ya Magufuli, baada ya stand kuna round about, kata kushoto uvuke daraja, then utakuta roundabout nyingine, izunguke na endelea mbele hadi roundabout nyingine(ile ya kwa Yusufu) ndio njia ya morogoro ya zamani. Then rudi kama unaenda mbezi stand ya malamba, utakutana na njia ya kuelekea huko unakoenda.
 
Unajua ni nini tunapata changamoto kwakuwa hatujazoea kusoma alama za barabarani ila ukiwa makini tu kitizama alama wala huwezi kusumbuka hata ukiendq New York
Watu wa mikoani bana, hiyo barabara haina alama, bado hawajaweka.
 
Rahisi sana, ukitoka Goba kuelekea Tabata nenda hadi upite stand ya Magufuli, baada ya stand kuna round about, kata kushoto uvuke daraja, then utakuta roundabout nyingine, izunguke na endelea mbele hadi roundabout nyingine(ile ya kwa Yusufu) ndio njia ya morogoro ya zamani. Then rudi kama unaenda mbezi stand ya malamba, utakutana na njia ya kuelekea huko unakoenda.
Aisee ahsante...kumbe ina Ka process!!
 
Serikali inaweza ona namna ya kuweka interchange hapo hapo
Ipo, ukitoka Kibaha ingia kama unakwenda stand kuu, kisha kazunguke round about ya pili uvuke highway, utaona kibao kinaelekeza iliko Kinyerezi yako fuata uelekeo utafika, nilichojifunza ...wengi wavivu kusoma vibao njiani
 
Maelezo marefu tu ila sio parefu wala, kwani hujawahi fika Magu stand?
Nimefika mara mbili tatu, Ila hizo stand za Yusufu ndio sizijui, maelezo lakini yamejitosheleza. Nitajaribu siku moja.
 
Back
Top Bottom