Japokua naishi Dar es Salaam, binafsi nakupenda Mbeya kwasababu zifuatazo.
1. Mbeya kuna hali ya hewa nzuri ambayo hata mgeni kutoka Ulaya lazima aipende.
2. Mbeya kuna vyakula vingi vitamu na vya kila aina na vya bei ndogo.
3. Mbeya kuna mazingira mazuri ya kusomea
4. Mbeya unakunywa maji ya kisima😋😋😋😋😋😋😋😋Mbeya unafulia maji ya kisima.
5. Mbeya ukiagiza chakula hotelini maji ya kunywa unamiminiwa kutoka kwenye majagi maalumu. Na hayo maji yanachotwa kwenye ndoo tu. Kitu kimetulia cha baridiii
6. Mbeya kuna AC za asili, ukilala ukijifunika blanket unaweza sahau kwenda kazini. Usingizi mtamuuuu. Hii Christmas nataka nikale Mbeya, maeneo ya Soweto.
Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.
Hii ndio imenipa akili ya kuanza mkakati wa kufungua kiwanda cha Kuchukua maji ya bahari ya Hindi na kuondoa chumvi, ili kupata maji safi na salama.
Lakini pia kuna vimashine nitawauzia wakazi wa Dar es salaam waliochimba visima vyenye maji ya chumvi, vitakua vinatumia solar kutoa chumvi kwenye maji ya kisima. Sasa wakazi wataweza kupata maji ya kunywa, kufulia na kuoga majumbani mwao.
1. Mbeya anayosema Mwandishi Maji yake hayafai yana vijidudu hatari ukinywa basi jiandae na Magonjwa yoe ya tumbo yatakuhusu uliza takwimu za Magonjwa yanayoongoza Mbeya.
2. Jiulize kwa nini Wazungu wamejazana Iringa na sio Mbeya hali ya hewa ya Mbeya haifai kwa kuishi binadamu ni kali mno na hapo ni mbeya Mjini na Mbarali kwingine unaweza anika nguo wiki nzima isikauke.
3. Bora vibaka wa Dar mnaweza hata kuburgain wakati amekutaiti ila Mbeya unapigwa nondo ufilie mbali na hapo wanampekua jamaa wanamkuta ana jero.
4. Uchawi na Ushirikina mbeya umekithiri kiasi hata paka akilia mtu anajua karogwa.
5. Ubaguzi na Ukabila Wasafwa na Wanyakyusa , Wamalila, Wasangu, Wabungu, Wandali hadi Wanyiha hawapendani yaani hata ukifungua Biashara utapata tabu kuuza. Wajanja wao ni Wakinga maana wamewazidi uchawi.
6.Mji una vipindi vibaya kama Taleban yaani vumbi tupu yaani vumbi hata dodoma kuna afadhali
7.Miundombinu ni hovyo kabisa yaani wana barabara moja muhimu kama chupa ya chai, nyingine zote ni utopolo
8.Halafu ushamba kwao sifa
9.Vitongoji kama Isanga, Iganzo, Igodima, Ilemi, kagera ,soko matola, ghana, mbata, iyunga ,nzovwe,mabatini, isyesye ,igawilo kote huko ni utopolo tu kidogo Iwambi, new forest na forest ya zamani
10.Vyakula vya aina ya Samaki hadi wa ziwa nyasa bado ni gharama sana au utakula kande kila siku.