Mbeya: Soko la Mwanjelwa lageuka Parking ya magari

Mwanongwa

JF-Expert Member
Feb 15, 2023
539
531
Hivi Kwa gharama za zaidi ya Bilioni 16 zilizotumika kujenga Soko la Mwanjelwa ndiyo tumeamua kuligeuza Parking ya magari?

Licha ya gharama kubwa zilizotumika kulijenga Soko hilo lakini limeshindwa kabisa kuwavutia wafanyabiashara kuhamia hapo au kuanzisha biashara hapo.

Mwanzo sababu ilikuwa gharama kubwa za kupanga vyumba lakini kwasasa gharama zimepungua lakini Soko bado limedoda kabisa

Leo nilipata Bahati ya kutembelea Soko hilo aiseee ni chafu balaa,hasa Yale maeneo ya ngazi na zile njia za kupandishia kwenda ghalofani.

Zile ngazi na zile korido hasa za ule upande ambako ipo Benki ya Postal zinanuka mikojo hatari utadhani Soko halina choo na wahusika wametulia tu.

Swali ninalojiuliza ni zile gharama zitalipwaje maana mwanzo walitegemea watapata wapangaji lakini kwasasa mambo ni tofauti kabisa,au watakusanya hizi za kupaki magari ndiyo zitalipa deni.

Mimi nawapa ushauri wa bure kabisa,chukuweni wale wamachinga wanaopanga vitu vyao kweye Barabara ya Mfikemo wote wale waingizeni Kwenye Soko hilo naamini itasaidia kuchangamsha Soko.

Ila pia niwapongeze Kwa kujiongeza na kugeuza Soko kuwa Parking,maana wafanyabiashara karibia wote wa Soko la Sido wanapark hapo magari yao toka asubuhi hadi jioni.

DSC_0223.JPG
DSC_0230.JPG
DSC_0231.JPG
DSC_0234.JPG
DSC_0228.JPG
DSC_0227.JPG
DSC_0223.JPG
DSC_0230.JPG
DSC_0231.JPG
DSC_0234.JPG
DSC_0228.JPG
DSC_0227.JPG
 
Back
Top Bottom