Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,870
- 155,832
Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyowahi kutokea huko Mbeya.
- Eneo la Forest kulikuwa na msitu mkubwa ambako mauji yalikuwa yakifanyika kila uchao.
- Eneo la soweto kulikuwa na wachinjaji, kila mara miili ya watu waliochinjwa ilikuwa ikukutwa eneo hilo.
- Nonde ni kitongoji kilichopo Mbeya mjini, ila kimekaa kama kiko maili elfu tatu kutoka mjini. Bangi inavutwa hadharani kuanzia kwenye ngazi ya familia. Huko kazi yao kubwa, kinababa ni kuchinja ng'ombe na wanawake kufanya biashara ndogondogo soko la Mabatini. Kiongozi asiye rasmi aliyewahi kusimika bendera na kudai kuwa Nonde ni nchi yake alikuwa ni Baunsa mchinja ng'ombe maarufu akiitwa Mwasimba.
- Jombi alikuwa ni jambazi maarufu zambia na tanzania akiteka magari, kupora magari na mali za watu.Alikuwa akitoa taarifa kabla hajafanya uhalifu wake. Wazungu wa Denmark waliokuwa wakifadhili mradi wa maji danida walikatisha msaada wao baada ya Jombi kuua na kubaka mke wa mkurugenzi wa mradi huo. Mkapa akatoa amri kuwa jombi akamatwe. Vikosi maalum ndio vilivyoenda kumkamata jombi.
- Mbeya kuna makanisa mengi sana yenye majina ya Kiingereza, Kiswahili, Kinyiha, Kisafwa, Kimalila na Kikimbu. Makanisa mengi na uovu mwingi vyaenda sambamba.
- Waimbaji wa nyimbo za injili wanaovuma wengi wao wana asili ya Mbeya.
- Pombe ya kadansana ilikuwa maarufu sana mwaka 2000, haijuulikani ilikokuwa ikitokea. Ilikuwa ikiua sana watu, na watu waliendelea kuishabikia hadi ilipogundulika kuwa inatoka Malawi, ikapigwa marufuku kabisa.
- Mauaji na uchunaji wa ngozi uliwatisha sana watu waishio nje ya mkoa wa Mbeya, Mbeya hali ilikuwa shwari kabisa.
- matukio ya kupigana na nondo ilikuwa gumzo sana mwaka juzi na mwaka jana, wengi walijeruhiwa.
- Leo Mbeya kuku na nguruwe wananenepeshwa kwa dawa za kuzuia makali ya ugonjwa wa ukimwi.
- Pombe inayoitwa kiduchu ndio sasa iko kwenye midomo ya watu. lmeacha gumzo kwa kuwa ukiiweka kwenye chupa inavimbisha chupa hadi inapasuka. pombe hiyo inahifadhiwa kwenye vyungu.Ni ya hatari lakini wana Mbeya wanaendelea tu kuinywa.
- Kuna vivutio kibao vya utalii lakini havitangazwi, sijui ni kwanini.
- Pichani ni kijana Peter muongoza watalii akijipumzisha baada ya kazi ngumu ya kutwa nzima.
-