Uchaguzi 2020 Mbeya na Iringa bado ngoma ngumu kwa CCM

MBEYA NA IRINGA BADO NGOMA NGUMU

Na, Robert Heriel

Kama kuna majimbo ambayo CCM itahangaika sana ni pamoja na Iringa Mjini, Mbarali, Mbeya Mjini, na Tunduma Mjini.

Kanda ya juu Kusini sasa ndio itakuwa kambi Rasmi ya Upinzani tofauti na sasa ambapo Kanda ya kaskazini mashariki yaani Arusha na Moshi Mjini.

Ni rahisi Kwa CCM kupata jimbo la la Moshi mjini na Arusha Mjini Kuliko Kuyapata Majimbo ya Iringa Mjini na Mbeya Mjini.
Sitashangaa kutokumuona Lema na mbunge atakayepeperusha bendera ya CHADEMA pale moshi mjini,

Tulia Ackson namuona kama Mpambanaji anayejaribu bahati yake, lakini uhakika ni kuwa hawezi kupata ubunge hapo Mbeya Mjini. Jimbo la Mbeya mjini ni gumu mno zaidi ya majimbo mengine. Sitashangaa Sugu akimshinda Tulia kwa kura zaidi ya elfu ishirini, hilo halitanishangaza kabisa.

Kitu pekee ambacho ninakiona katika majimbo hayo ni muitikio wa wanawake kwenye siasa pamoja na wanaume watu wazima. Nafahamu wanawake ndio wapiga kura wakubwa na watu wazima.

Mbeya Mjini na Iringa wakina mama ni wengi wanaoukubali Upinzani, kina baba ni wengi wanaoukubali upinzani. Achilia mbali vijana ambao kimsingi ndio wapinzani wenyewe lakini hawa wengi wao sio wapiga kura. Kina mama na wababa ukiona wanakusapoti basi kuwa na uhakika kwamba utashinda.

Arusha na Moshi Mjini kwa sasa inapoteza sifa yake, ni kama wameishiwa pumzi, nina uhakika jimbo moja kati ya Moshi mjini au Arusha mjini Mwaka huu lazima liende CCM. na kama Upinzani hawatakuwa makini wanaweza kupoteza majimbo yote mawili.

Kwa upande wa Mbowe pale Hai, mwaka huu atashinda lakini kwa Kura chache sana.

Majimbo mengine ambayo CCM itaonja joto la jiwe ni pamoja na Mikumi kwa Profesa Jay, Kigoma mjini, Tunduma, Tarime Vijijini, Bunda huyu atashinda kwa kura chache,

Majimbo ambayo yapo hati hati kuchukuliwa na CCM ni KAWE kwa Halima Mdee, Ubungo hili litachukuliwa asubuhi kabla magari yanayotoka Dar hayajafika morogoro. Kibamba hili nalo litachukuliwa mapema tuu.

CCM mwaka huu itachukua majimbo mengi ya Upinzani, lakini litashindwa kuchukua majimbo ya Iringa mjini na Mbeya mjini.

Kwa upande wa Jimbo la Singida mashariki alipokuwa Tundu Lisu, upinzani utachukua kwa kura chache.

Upande wa Urais, mgombea wa Upinzani, atachukua kura nyingi jimbo la Iringa Mjini, mbeya mjini, Mikumi, Kigoma mjini, kusini na kaskazini, Tarime vijijini, Bunda nusu nusu, Arusha mjini Nusu kwa Nusu, Moshi Mjini nusu kwa Nusu, Karatu mpinzani atashinda, Majimbo mengi ya Singida watagawana na CCM, Zanzibar upinzani utashinda ikiwa watasimamisha mgombea mmoja.

Kama Lisu atapitishwa na NEC atapigwa kwenye majimbo mengi na Magufuli, labda abadilishe mbinu hasa katika utoaji wa hotuba.

Ni ngumu Lisu kumshinda Magufuli lakini kama atabadili hotuba zake Lisu anaweza kushinda hata kwa kura laki moja.

Mambo ambayo Lisu lazima ayaongelee ili apewe kura na kumzidi Magufuli

1. Ajira kwa vijana na namna ya kuondoa umasikini
Lisu lazima awashawishi vijana ambao wengi kwa sasa hawana ajira, Lisu lazima atumie ushawishi mkubwa kuhakikisha anageuza nyoyo za vijana, aseme ataajiri vijana,

Hoja hii Atamzidi Magufuli kwa sababu ni wazi awamu hii Magufuli hajaajiri vijana wengi, hivyo kufanya vijana wengi kubaki mtaani wakiwa wamezubaa.

Magufuli hoja hii hawezi kuitumia kwani ataonekana anaongea uongo, tena ataonekana anawadharau vijana kwa kuongea uongo wa mchana kweupe. Najua hawezi kusema kuwa ataajiri akipewa tena, kwani vijana watamuambia kama ulishindwa kutuajiri awamu ya kwanza basi hata awamu ya pili utashindwa.

2. Nyongeza ya Mishahara, na kupanda madaraja.
Lisu anaweza akashinda, ikiwa atatoa maneno yenye kushawishi wafanyakazi na watumishi wa UMMA kuhusiana na nyongeza ya mishahara na kupanda vyeo.

Wafanyakazi wengi hawajaongezewa mishahara tangu Magufuli aingie madarakani, hakuna mtumishi anayelifurahia hili lakini watafanya nini ikiwa waliambiwa kama mshahara mdogo waache kazi.

Lisu lazima aeleze kuwa serikali isipoongeza mshahara inatengeneza mazingira hata kwa sekta binafsi kupunguza mishahara ya wafanyakazi wao.

Lisu lazima aseme kuwa endapo serikali haiajiri inasababisha thamani ya elimu kushuka, na wataalamu kulipwa ujira mdogo kwenye sekta binafsi.

Lisu lazima atoe mifano kuwa serikali inapogoma kuajiri inasababisha vijana wasomi kuwa cheap labor. Atoe mifano kuwa wapo wasomi wa ngazi ya shahada wanaolipwa laki moja, wengine wakijitolea kwenye sekta binafsi miaka nenda rudi wakisubiri ajira lakini mtoa ajira yupo kimya.

Lisu lazima azungumzie suala la vijana wa viwandani wanaolipwa chini ya laki themanini huku wakifanya kazi masaa kumi na mbili.

Hili magufuli kashindwa kulitolea maelezo, na penginde muda huo hana.

3. Unyonyaji wa wazungu
Lisu lazima azungumzie suala la makampuni ya kigeni yaliyokuja kuwekeza hapa nchini na namna yanavyolinyonya taifa hili.

Lisu hapaswi kukaa kimya kuwakemea wazungu.

Katika hili Magufuli amemzidi kwa mbali kabisa, Magufuli amejipambanua kwa kuwakemea wazungu, hata mimi namsapoti.

4. Uhuru wa Vyombo vya habari
Lisu katika hili namuona akijitahidi kulibeba, na linampa nguvu kubwa kwa watu wengi hasa wenye taaluma.

Magufuli hapa atashindwa kwani amekuwa nyuma katika hili wakati yeye anayomamlaka namba moja hapa nchini

5. Haki za Binadamu
Lisu katika hili kajidhatiti, nafikiri ni kwa vile yeye ni mwanasheria. Lisu lazima apigilie misumari kwa matukio ya kikatili ambayo yametokea nchi hii na vyombo husika havijafuatilia, matukio ya utekaji, mauaji, unyanyasaji, upendeleo miongoni mwa mambo mengine.

Lisu hili linambeba kwa watu wote wenye hofu ya Mungu, waasomi na watu wanaojua dunia ipo wapi.

Lisu atafeli katika hoja hii pale atakaposhindwa kueleza mipaka ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya ushoga, usagaji, umalaya, kutupa picha za uchi mitandaoni, ambapo kimsingi katika Hili Magufuli naye kajipambanua.

Lisu lazima atoke hadharani aseme kuwa tunapenda haki, lakini sio haki zinazovunja utu wa mwanadamu, aseme kuwa hataruhusu ushoga, wasagaji na wahuni kulingana na sheria za nchi yetu.

Lisu amezidiwa hapa na Magufuli kwa sababu Anashindwa kueleza kinagaubaga tena kwa ukali kuwa Ushoga ni kosa. Magufuli katika hili amemshinda. Na hili linambeba.

6. Kukemea na Kutokomeza Rushwa na Ufisadi.
Lisu lazima akemee Rushwa na Ufisadi. Lisu ni mwanasheria hivyo anajua ni kwa namna gani anaweza kulisaidia taifa hili kwa kutokomeza Rushwa na Ufisadi.

Lisu atachaguliwa na Watanzania kwa kukema Rushwa na Ufisadi.

Magufuli katika hoja ya Rushwa na Ufisadi amejidhatiti na kajitahidi kwa kiasi chake. Shida ya Magufuli ni pale ambapo hatuoni Fisadi yeyote aliyefungwa licha ya kuanzishwa kwa mahakama ya Ufisadi. Niliwahi sikia wapo waliwekwa rumande lakini baadaye waliambiwa walipe kisha watolewe. Hiyo binafsi ilinifanya nione kama igizo la kuchekesha.

Wezi wa kuku nao wangeambiwa warudishe kuku watolewe, wezi wa maduka, n.k
Hata hivyo siasa inamambo mengi, kwa umri wangu mengine pengine yakawa sio level yangu. Lakini kwa akili ya kawaida, jambo lile lilikuwa sio zuri.

7. Mahusiano Mazuri ndani ya Nchi na jumuiya za Kimataifa.
Lisu lazima aeleze kwa kina ni mahusiano yapi ayatakayo baina ya nchi yetu na mataifa mengine.

Magufuli katika hili kajidhatiti kikamilifu kuwa, yeye hana shida na taifa lolote, anahitaji uhusiano mzuri na mataifa mengine, lakini mahusiano hayo sharti yawe na maslahi kwa taifa letu. Hiyo nampa Tiki, hata mimi ningekuwa Rais ningefanya kama yeye, nchi kama inataka kukunyonya au kukulalia unaipiga mtama wa mchomvu. Lazima kuwe na mutual relationship.

Kuhusu Kuzikana, ni kweli MAGUFULI anafanya isivyo halali kutokwenda kwenye misiba ya wakubwa wenzake huko nchi za nje, lakini nami nasema sio kila msiba lazima aende, angalau msiba mmoja kwa misiba minne aende. Asipoenda kabisa inaonekana hana upendo, akienda kila msiba ataitwa Rais wa Misiba.

Kwa upande wa ndani ya nchi, Magufuli nimeshawahi kuona kwenye media viongozi kadhaa wa upinzani wakialikwa ikulu au pengine kwenda wao wenyewe. Magufuli anafanya vizuri katika hilo. Kuhusu CHADEMA kutoitwa Ikulu, kama hujaitwa IKULU na unalolote la kuongea na Rais, nini kilikuzuia, viongozi wa CHADEMA kama hamkuitwa Ikulu, mngepaswa muende ninyi. Hapa Magufuli hana makosa, vinginevyo awe aliwahi kufuatwa na viongozi wa CHADEMA akakata, kwa kweli hata mtanzania wa kawaida akisikia ataona Magufuli hajafanya vizuri.

Kuhusu Mikutano ya Kisiasa, ni kweli kabisa kuna muda wa siasa na muda wa kazi. Lakini hatuwezi kusahau kuwa wapo watu wamesomea taaluma ya siasa, yaani siasa kwao ni kazi. Kuwazuia vyama upinzani kufanya siasa kwa miaka karibu mitano wakati CCM tunawaona wakifanya mikutano yao hapa na pale haikuwa vizuri. Lisu katika hili watanzania wenye kupenda haki na wasomi watamuelewa.

8. MAENDELEO
Lisu lazima atuambie ni namna gani atatuletea maendeleo katika miundombinu, huduma za kijamii, kilimo, mawasiliano, viwanda, usafirishaji n.k

Magufuli katika hili kafanikiwa kwa asilimia kubwa. Hapa Magufuli hatatumia nguvu kubwa kwani tayari amefanya kwa kiasi maendeleo,
Magufuli kafanya yafuatayo kwa kipindi chake
1. SEKTA YA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI

1.1. RELI
>Kafufua reli ya kaskazini, DSM, Tanga, Moshi na Arusha. Hii niliipanda mwezi wa pili.
> Kujenga Reli ya Kisasa SGR, HII nami nimeikagua imefikia pazuri
> Kununua na kukarabati mabehewa na miundombinu ya Reli pamoja na Treni

1.2. NDEGE
> Kafufua shirika la ndege kwa kununua ndede za kisasa, Nadhani mpaka sasa Tangu aingie madarakani kanunua ndege 6.
> Kajenge Terminal 3 pale uwanja wa Julius kambarage Nyerere
> Kajenga uwanja wa Ndege Chato. Japo wapinzani wake wanakosoa vikali, lakini Chato pia ni Tanzania.

1.3. Barabara
> Magufuli kajenga barabara na kuzikarabati barabara nyingi hapa Tanzania

2. HUDUMA ZA KIJAMII
> Magufuli kajenga hospitali nyingi za wilaya na kuzikarabati. Japo kuna changamoto ya madaktari na madawa lakini atapongezwa na kila mtu muungwana kwa kufanaya hivyo.

> Magufuli chini ya serikali ya awamu yake, umeme umetambazwa kwa kiasi kikubwa vijijini, pia tatizo la umeme sio sana

> Maji, kwa sehemu kubwa hasa mjini serikali imejitahidi kuwapa wananchi maji. Lakini bado changamoto ni kubwa.

> Serikali imejitahidi kutoa elimu bure kwa ngazi ya msingi mpaka shule ya upili kidato cha nne. Pia madawati kwa sehemu za mjini kwa kiasi kikubwa. Lakini bado miundombinu ya elimu bado haijatengemaa. Lakini angalau amepagusia.

> Huduma za kipolisi, kwa kiasi kikubwa uhalifu wa unyang'anyi umepungua, vikundi vya uhalifu kama panya road, watoto wa Mbwa, vimedhibitiwa, hata changamoto ya kuel kibiti, mapango ya Amboni, Mwanza, kote kumedhibitiwa.
Kasoro kubwa ilikuwa utekaji ambapo kwa sehemu kubwa wapinzani wanaishutumu serikali.
Huduma za ulinzi imejitahidi sana, lakini kasoro ipo kwenye utekaji kwa watu wasiojulikana.

3. UTALII
3.1 Uanzishwaji wa TANZANIA SAFARI CHANEL
Kupitia chanel hii utalii wa nchi unatangazwa ndani na nje ya Tanzania, tunatangaza nchi yetu, hivyo utalii utakua. Lakini pia wapo watanzania wenzetu wamepata ajira pale.
Changamoto ya Chanel hii ni kuwa Hakuna ubunifu, mambo yanarudiwa yale yale kila siku utadhani hakuna mambo mengine. Nafahamu ubunifu uanenda sambamba na uwekezaji, serikali ihakikishe vijana wanakusanya taarifa za kuvutia ili zirushwe luningani.

3.2 Kuzipandisha hadhi mapori na kuwa hifadhi
> Serikali hii imepandisha hadhi baadhi ya mapori na kuwa hifadhi matahalani mapori ya akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi. Manufaa yatakajikita katika uimarishaji wa utalii pamoja na ulinzi katika mapori hayo.
Pia kupitia upandishaji hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ajira zimezalishwa kwa watakaozihudumia hifadhi hizo.

Lisu hapaswi kuziponda kazi za Magufuli, katika hilo anakosea, na anatukosea watanzania hasa wale ambao hatuna mrengo wowote zaidi ya kuangalia maslahi ya nchi.

Lisu kuziponda kazi za Magufuli unapoteza baadhi ya kura kwa wale wanaoziona.

Lisu unapaswa uponde yale mapungufu aliyonayo Magufuli katika utendaji wake kwa kulitumikia taifa hili. Mimi naunga mkono mtu anayetenda haki, asiye na upendeleo.

Mtu asiye na mawe mawili ya kupimia, mtu asiye mnafiki.

Ninapenda Lisu na Magufuli washirikiane, iwe ni Lisu kashindwa au Magufuli kashindwa. Wote ni Watanzania.

Mbeya na Iringa bado kugumu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
MJITAHIDI KUTUNZA HIZI THREAD ZENU MAANA BAADA YA OCTOBER 30 SIAMINI KAMA MTAKUWA NA UWEZO WA KUCHANGIA MADA KWA JINSI MTAVYOKUWA MMELOWA JASHO LA KUSHINDWA
 
Katika majimbo yote ya upinzani jimbo ambalo labda Chadema wanaweza kupoteza ni Kibamba.

Lakini nayaona majimbo mengine ya wazi yakiangukia Chadema tena asubuhi tu mfano Kyela, Mbarali, Mafinga mjini, Mororgoro mjini, Ilala. Pia majimbo ambayo CCM watashinda basi kutakuwa na uwiano mdogo sana wa kura. Kiukweli nimewasifu watanzania sasa wanaiona siasa kama kazi isiyohitaji masihara!

Kitu kingine Magufuli ana uwanja mdogo sana wa kujinadi ambao ni miundombinu na hilo kila kiongozi analiweza. Magufuli pia hataweza kujinadi kwa hilo maana amekuwa akilizungumza kwa miaka yote mitano! Hawezi kuwaambia watu eti ataajiri au kuongeza mshahara wamuelewe maana tayari alishawadanganya 2015 baada ya kushindwa kutekeleza mengi.

Kiukweli Lissu ana uwanja mpana na atakapokuwa anahutubia kwanza wananchi watakuwa na kumbukumbu ya yeye kupigwa risasi, uminywaji mkubwa wa haki na mengine mengi. Magufuli atakuwa hadi anaona aibu mbele za watu hasa kwa swala la mpinzani wake kupigwa risasi na hajafanya kitu kama kiongozi.

Kitu kingine Magufuli hachelewi kuharibu wakati wa kuhutubia maana wameshaona kila hotuba. Kumbuka kuwa kipindi hiki ana kiburi na amekionyesha waziwazi kwa watanzania. Kitu ambacho ni tofauti kabisa na alipokuwa akihutubia mwaka 2015! Alikuwa anaonyesha upole na unyenyekevu mkubwa.

Kuna maeneo akienda kwanza itamlazimu aanze kuweka hali sawa kama Kusini, Kagera na Kaskazini. Kumbuka kuwa Magufuli Kaskazini hajawahi kufanya ziara ya kimaendeleo na hajapeleka chochote kile zaidi ya hilo treni ambalo kimsingi kwa watu wa Kaskazini ni useless! Magufuli alikosea sana kujitenga na kuikumbatia njia yake ya uelekeo wa Chato! Halafu dhambi ya ubaguzi ameionyesha wazawazi!

Halafu ndani ya CCM kwenyewe mfano mtu kama JK hata anavyoongea unaona kabisa hamkubali hata kidogo Magufuli. Mwisho wa yote mtu ambaye walimtegemea kuwa anaweza kuongea kitu kikaingia masikioni na alikuwa mtetezi mkubwa wa kutegemewa wa Magufuli ameshaaga dunia! Aliyebaki Mwinyi hana point, JK ndo hivyo akiongea hadi kina Hapi kule Iringa wanarusha mawe!

Mwisho kabisa tegemeeni kusikia mtu au watu ndani ya CCM wakiropoka kuhusu matukio ya watu kupotea, Lissu kupigwa risasi na mengine mengi. Kiuhalisia Magufuli amejijengea taswira mbaya sana ya ubinadamu machoni pa watanzania kitu ambacho watanzania wengi wanakithamini kwa nguvu kubwa!
 
Katika majimbo yote ya upinzani jimbo ambalo labda Chadema wanaweza kupoteza ni Kibamba.

Lakini nayaona majimbo mengine ya wazi yakiangukia Chadema tena asubuhi tu mfano Kyela, Mbarali, Mafinga mjini, Mororgoro mjini, Ilala. Pia majimbo ambayo CCM watashinda basi kutakuwa na uwiano mdogo sana wa kura. Kiukweli nimewasifu watanzania sasa wanaiona siasa kama kazi isiyohitaji masihara!

Kitu kingine Magufuli ana uwanja mdogo sana wa kujinadi ambao ni miundombinu na hilo kila kiongozi analiweza. Magufuli pia hataweza kujinadi kwa hilo maana amekuwa akilizungumza kwa miaka yote mitano! Hawezi kuwaambia watu eti ataajiri au kuongeza mshahara wamuelewe maana tayari alishawadanganya 2015 baada ya kushindwa kutekeleza mengi.

Kiukweli Lissu ana uwanja mpana na atakapokuwa anahutubia kwanza wananchi watakuwa na kumbukumbu ya yeye kupigwa risasi, uminywaji mkubwa wa haki na mengine mengi. Magufuli atakuwa hadi anaona aibu mbele za watu hasa kwa swala la mpinzani wake kupigwa risasi na hajafanya kitu kama kiongozi.

Kitu kingine Magufuli hachelewi kuharibu wakati wa kuhutubia maana wameshaona kila hotuba. Kumbuka kuwa kipindi hiki ana kiburi na amekionyesha waziwazi kwa watanzania. Kitu ambacho ni tofauti kabisa na alipokuwa akihutubia mwaka 2015! Alikuwa anaonyesha upole na unyenyekevu mkubwa.

Kuna maeneo akienda kwanza itamlazimu aanze kuweka hali sawa kama Kusini, Kagera na Kaskazini. Kumbuka kuwa Magufuli Kaskazini hajawahi kufanya ziara ya kimaendeleo na hajapeleka chochote kile zaidi ya hilo treni ambalo kimsingi kwa watu wa Kaskazini ni useless! Magufuli alikosea sana kujitenga na kuikumbatia njia yake ya uelekeo wa Chato! Halafu dhambi ya ubaguzi ameionyesha wazawazi!

Halafu ndani ya CCM kwenyewe mfano mtu kama JK hata anavyoongea unaona kabisa hamkubali hata kidogo Magufuli. Mwisho wa yote mtu ambaye walimtegemea kuwa anaweza kuongea kitu kikaingia masikioni na alikuwa mtetezi mkubwa wa kutegemewa wa Magufuli ameshaaga dunia! Aliyebaki Mwinyi hana point, JK ndo hivyo akiongea hadi kina Hapi kule Iringa wanarusha mawe!

Best Morogoro mjini itoe hapo umejimix
 
Akipiga Kura kila kitu akachukue ofisi za CCM asitegemee kitu au support yyt kutoka kwangu! Yaani namaanisha!

Usifanye hivyo,
kipimo umpimiacho mtu ndicho utakachopimiwa.

Kwa vile sio kosa kisheria kuwa na tofauti za kimtazamo, usimfanyie hivyo. Kama ameshindwa kukuelewa achana naye
 
Chadema wakiungana na ACT watapata viti vya ubunge 60 percent na Urais Lissu anashinnda kwa 70 percent ili halina mjadala.
LISU hapati zaidi ya 20%

Hili suala watu wanaona kama napiga propaganda ila ndio ukweli
 
Nadhani ni wkt wa Pascal Mayala kujifunza kutoka kwenye huu uchambuzi..asiegemee upande wwte

Kaka Pascal alitegemea hisani kwenye uchaguzi huu. Huoni aligombea?

Ukishakuwa mshabiki wa chama iwe CCM, CHADEMA, au chama chochote unakuwa mtumwa wa vyama hivyo. Lazima uwe mnafiki. Huwezi kukosoa mapungufu ya chama chako kwa kuhofia kutopewa cheo
 
Kweli kbsaa
 
Umejitahidi kueleza ila pale pa kusema huoni mafisadi wakifungwa jela Hapo umekosea kumshugulikia fisadi sio kumfunga tu ni kushughulika na Mali alizochuma kifisadi

Wengi wanalia biashara zao Magufuli kahakikisha zinakufa kifo Cha uhakika kwa kutumia mbinu za kisayansi

Wewe shahidi mafisadi mingi iliiba pesa serikalini ikajenga mihoteli na mi apartment Mbeya,Arusha, Morogoro,Dar nk ikitegemea tenda za serikali Sasa hivi mingi imefilisika na mingine kufariki dunia kwa pressure sababu serikali ilikata tenda zote

Mifisadi mingi ndio ilichangia Chadema 2015 uchaguzi huu haina pesa imeshughulikiwa barabara . Chadema waliipokea mifisadi Magufuli akaishughulikia barabara ikiwa huko huko Chadema ikarudi mingine mbio CCM ikitegemea labda atalegeza akakaza Uzi
Chadema mwaka huu haina pesa Baada ya Magufuli kuishughulikia mifisadi iliyoenda kujificha Chadema.Huko Kuna fisadi mmojatu kabaki ambaye naye analiwa timing saaa yeyote atakiona Cha mtema kuni katulia akidhani kumetulia
C😀😀😀😀
 
MBEYA NA IRINGA BADO NGOMA NGUMU

Na, Robert Heriel

Kama kuna majimbo ambayo CCM itahangaika sana ni pamoja na Iringa Mjini, Mbarali, Mbeya Mjini, na Tunduma Mjini.

Kanda ya juu Kusini sasa ndio itakuwa kambi Rasmi ya Upinzani tofauti na sasa ambapo Kanda ya kaskazini mashariki yaani Arusha na Moshi Mjini.

Ni rahisi Kwa CCM kupata jimbo la la Moshi mjini na Arusha Mjini Kuliko Kuyapata Majimbo ya Iringa Mjini na Mbeya Mjini.
Sitashangaa kutokumuona Lema na mbunge atakayepeperusha bendera ya CHADEMA pale moshi mjini,

Tulia Ackson namuona kama Mpambanaji anayejaribu bahati yake, lakini uhakika ni kuwa hawezi kupata ubunge hapo Mbeya Mjini. Jimbo la Mbeya mjini ni gumu mno zaidi ya majimbo mengine. Sitashangaa Sugu akimshinda Tulia kwa kura zaidi ya elfu ishirini, hilo halitanishangaza kabisa.

Kitu pekee ambacho ninakiona katika majimbo hayo ni muitikio wa wanawake kwenye siasa pamoja na wanaume watu wazima. Nafahamu wanawake ndio wapiga kura wakubwa na watu wazima.

Mbeya Mjini na Iringa wakina mama ni wengi wanaoukubali Upinzani, kina baba ni wengi wanaoukubali upinzani. Achilia mbali vijana ambao kimsingi ndio wapinzani wenyewe lakini hawa wengi wao sio wapiga kura. Kina mama na wababa ukiona wanakusapoti basi kuwa na uhakika kwamba utashinda.

Arusha na Moshi Mjini kwa sasa inapoteza sifa yake, ni kama wameishiwa pumzi, nina uhakika jimbo moja kati ya Moshi mjini au Arusha mjini Mwaka huu lazima liende CCM. na kama Upinzani hawatakuwa makini wanaweza kupoteza majimbo yote mawili.

Kwa upande wa Mbowe pale Hai, mwaka huu atashinda lakini kwa Kura chache sana.

Majimbo mengine ambayo CCM itaonja joto la jiwe ni pamoja na Mikumi kwa Profesa Jay, Kigoma mjini, Tunduma, Tarime Vijijini, Bunda huyu atashinda kwa kura chache,

Majimbo ambayo yapo hati hati kuchukuliwa na CCM ni KAWE kwa Halima Mdee, Ubungo hili litachukuliwa asubuhi kabla magari yanayotoka Dar hayajafika morogoro. Kibamba hili nalo litachukuliwa mapema tuu.

CCM mwaka huu itachukua majimbo mengi ya Upinzani, lakini litashindwa kuchukua majimbo ya Iringa mjini na Mbeya mjini.

Kwa upande wa Jimbo la Singida mashariki alipokuwa Tundu Lisu, upinzani utachukua kwa kura chache.

Upande wa Urais, mgombea wa Upinzani, atachukua kura nyingi jimbo la Iringa Mjini, mbeya mjini, Mikumi, Kigoma mjini, kusini na kaskazini, Tarime vijijini, Bunda nusu nusu, Arusha mjini Nusu kwa Nusu, Moshi Mjini nusu kwa Nusu, Karatu mpinzani atashinda, Majimbo mengi ya Singida watagawana na CCM, Zanzibar upinzani utashinda ikiwa watasimamisha mgombea mmoja.

Kama Lisu atapitishwa na NEC atapigwa kwenye majimbo mengi na Magufuli, labda abadilishe mbinu hasa katika utoaji wa hotuba.

Ni ngumu Lisu kumshinda Magufuli lakini kama atabadili hotuba zake Lisu anaweza kushinda hata kwa kura laki moja.

Mambo ambayo Lisu lazima ayaongelee ili apewe kura na kumzidi Magufuli

1. Ajira kwa vijana na namna ya kuondoa umasikini
Lisu lazima awashawishi vijana ambao wengi kwa sasa hawana ajira, Lisu lazima atumie ushawishi mkubwa kuhakikisha anageuza nyoyo za vijana, aseme ataajiri vijana,

Hoja hii Atamzidi Magufuli kwa sababu ni wazi awamu hii Magufuli hajaajiri vijana wengi, hivyo kufanya vijana wengi kubaki mtaani wakiwa wamezubaa.

Magufuli hoja hii hawezi kuitumia kwani ataonekana anaongea uongo, tena ataonekana anawadharau vijana kwa kuongea uongo wa mchana kweupe. Najua hawezi kusema kuwa ataajiri akipewa tena, kwani vijana watamuambia kama ulishindwa kutuajiri awamu ya kwanza basi hata awamu ya pili utashindwa.

2. Nyongeza ya Mishahara, na kupanda madaraja.
Lisu anaweza akashinda, ikiwa atatoa maneno yenye kushawishi wafanyakazi na watumishi wa UMMA kuhusiana na nyongeza ya mishahara na kupanda vyeo.

Wafanyakazi wengi hawajaongezewa mishahara tangu Magufuli aingie madarakani, hakuna mtumishi anayelifurahia hili lakini watafanya nini ikiwa waliambiwa kama mshahara mdogo waache kazi.

Lisu lazima aeleze kuwa serikali isipoongeza mshahara inatengeneza mazingira hata kwa sekta binafsi kupunguza mishahara ya wafanyakazi wao.

Lisu lazima aseme kuwa endapo serikali haiajiri inasababisha thamani ya elimu kushuka, na wataalamu kulipwa ujira mdogo kwenye sekta binafsi.

Lisu lazima atoe mifano kuwa serikali inapogoma kuajiri inasababisha vijana wasomi kuwa cheap labor. Atoe mifano kuwa wapo wasomi wa ngazi ya shahada wanaolipwa laki moja, wengine wakijitolea kwenye sekta binafsi miaka nenda rudi wakisubiri ajira lakini mtoa ajira yupo kimya.

Lisu lazima azungumzie suala la vijana wa viwandani wanaolipwa chini ya laki themanini huku wakifanya kazi masaa kumi na mbili.

Hili magufuli kashindwa kulitolea maelezo, na penginde muda huo hana.

3. Unyonyaji wa wazungu
Lisu lazima azungumzie suala la makampuni ya kigeni yaliyokuja kuwekeza hapa nchini na namna yanavyolinyonya taifa hili.

Lisu hapaswi kukaa kimya kuwakemea wazungu.

Katika hili Magufuli amemzidi kwa mbali kabisa, Magufuli amejipambanua kwa kuwakemea wazungu, hata mimi namsapoti.

4. Uhuru wa Vyombo vya habari
Lisu katika hili namuona akijitahidi kulibeba, na linampa nguvu kubwa kwa watu wengi hasa wenye taaluma.

Magufuli hapa atashindwa kwani amekuwa nyuma katika hili wakati yeye anayomamlaka namba moja hapa nchini

5. Haki za Binadamu
Lisu katika hili kajidhatiti, nafikiri ni kwa vile yeye ni mwanasheria. Lisu lazima apigilie misumari kwa matukio ya kikatili ambayo yametokea nchi hii na vyombo husika havijafuatilia, matukio ya utekaji, mauaji, unyanyasaji, upendeleo miongoni mwa mambo mengine.

Lisu hili linambeba kwa watu wote wenye hofu ya Mungu, waasomi na watu wanaojua dunia ipo wapi.

Lisu atafeli katika hoja hii pale atakaposhindwa kueleza mipaka ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya ushoga, usagaji, umalaya, kutupa picha za uchi mitandaoni, ambapo kimsingi katika Hili Magufuli naye kajipambanua.

Lisu lazima atoke hadharani aseme kuwa tunapenda haki, lakini sio haki zinazovunja utu wa mwanadamu, aseme kuwa hataruhusu ushoga, wasagaji na wahuni kulingana na sheria za nchi yetu.

Lisu amezidiwa hapa na Magufuli kwa sababu Anashindwa kueleza kinagaubaga tena kwa ukali kuwa Ushoga ni kosa. Magufuli katika hili amemshinda. Na hili linambeba.

6. Kukemea na Kutokomeza Rushwa na Ufisadi.
Lisu lazima akemee Rushwa na Ufisadi. Lisu ni mwanasheria hivyo anajua ni kwa namna gani anaweza kulisaidia taifa hili kwa kutokomeza Rushwa na Ufisadi.

Lisu atachaguliwa na Watanzania kwa kukema Rushwa na Ufisadi.

Magufuli katika hoja ya Rushwa na Ufisadi amejidhatiti na kajitahidi kwa kiasi chake. Shida ya Magufuli ni pale ambapo hatuoni Fisadi yeyote aliyefungwa licha ya kuanzishwa kwa mahakama ya Ufisadi. Niliwahi sikia wapo waliwekwa rumande lakini baadaye waliambiwa walipe kisha watolewe. Hiyo binafsi ilinifanya nione kama igizo la kuchekesha.

Wezi wa kuku nao wangeambiwa warudishe kuku watolewe, wezi wa maduka, n.k
Hata hivyo siasa inamambo mengi, kwa umri wangu mengine pengine yakawa sio level yangu. Lakini kwa akili ya kawaida, jambo lile lilikuwa sio zuri.

7. Mahusiano Mazuri ndani ya Nchi na jumuiya za Kimataifa.
Lisu lazima aeleze kwa kina ni mahusiano yapi ayatakayo baina ya nchi yetu na mataifa mengine.

Magufuli katika hili kajidhatiti kikamilifu kuwa, yeye hana shida na taifa lolote, anahitaji uhusiano mzuri na mataifa mengine, lakini mahusiano hayo sharti yawe na maslahi kwa taifa letu. Hiyo nampa Tiki, hata mimi ningekuwa Rais ningefanya kama yeye, nchi kama inataka kukunyonya au kukulalia unaipiga mtama wa mchomvu. Lazima kuwe na mutual relationship.

Kuhusu Kuzikana, ni kweli MAGUFULI anafanya isivyo halali kutokwenda kwenye misiba ya wakubwa wenzake huko nchi za nje, lakini nami nasema sio kila msiba lazima aende, angalau msiba mmoja kwa misiba minne aende. Asipoenda kabisa inaonekana hana upendo, akienda kila msiba ataitwa Rais wa Misiba.

Kwa upande wa ndani ya nchi, Magufuli nimeshawahi kuona kwenye media viongozi kadhaa wa upinzani wakialikwa ikulu au pengine kwenda wao wenyewe. Magufuli anafanya vizuri katika hilo. Kuhusu CHADEMA kutoitwa Ikulu, kama hujaitwa IKULU na unalolote la kuongea na Rais, nini kilikuzuia, viongozi wa CHADEMA kama hamkuitwa Ikulu, mngepaswa muende ninyi. Hapa Magufuli hana makosa, vinginevyo awe aliwahi kufuatwa na viongozi wa CHADEMA akakata, kwa kweli hata mtanzania wa kawaida akisikia ataona Magufuli hajafanya vizuri.

Kuhusu Mikutano ya Kisiasa, ni kweli kabisa kuna muda wa siasa na muda wa kazi. Lakini hatuwezi kusahau kuwa wapo watu wamesomea taaluma ya siasa, yaani siasa kwao ni kazi. Kuwazuia vyama upinzani kufanya siasa kwa miaka karibu mitano wakati CCM tunawaona wakifanya mikutano yao hapa na pale haikuwa vizuri. Lisu katika hili watanzania wenye kupenda haki na wasomi watamuelewa.

8. MAENDELEO
Lisu lazima atuambie ni namna gani atatuletea maendeleo katika miundombinu, huduma za kijamii, kilimo, mawasiliano, viwanda, usafirishaji n.k

Magufuli katika hili kafanikiwa kwa asilimia kubwa. Hapa Magufuli hatatumia nguvu kubwa kwani tayari amefanya kwa kiasi maendeleo,
Magufuli kafanya yafuatayo kwa kipindi chake
1. SEKTA YA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI

1.1. RELI
>Kafufua reli ya kaskazini, DSM, Tanga, Moshi na Arusha. Hii niliipanda mwezi wa pili.
> Kujenga Reli ya Kisasa SGR, HII nami nimeikagua imefikia pazuri
> Kununua na kukarabati mabehewa na miundombinu ya Reli pamoja na Treni

1.2. NDEGE
> Kafufua shirika la ndege kwa kununua ndede za kisasa, Nadhani mpaka sasa Tangu aingie madarakani kanunua ndege 6.
> Kajenge Terminal 3 pale uwanja wa Julius kambarage Nyerere
> Kajenga uwanja wa Ndege Chato. Japo wapinzani wake wanakosoa vikali, lakini Chato pia ni Tanzania.

1.3. Barabara
> Magufuli kajenga barabara na kuzikarabati barabara nyingi hapa Tanzania

2. HUDUMA ZA KIJAMII
> Magufuli kajenga hospitali nyingi za wilaya na kuzikarabati. Japo kuna changamoto ya madaktari na madawa lakini atapongezwa na kila mtu muungwana kwa kufanaya hivyo.

> Magufuli chini ya serikali ya awamu yake, umeme umetambazwa kwa kiasi kikubwa vijijini, pia tatizo la umeme sio sana

> Maji, kwa sehemu kubwa hasa mjini serikali imejitahidi kuwapa wananchi maji. Lakini bado changamoto ni kubwa.

> Serikali imejitahidi kutoa elimu bure kwa ngazi ya msingi mpaka shule ya upili kidato cha nne. Pia madawati kwa sehemu za mjini kwa kiasi kikubwa. Lakini bado miundombinu ya elimu bado haijatengemaa. Lakini angalau amepagusia.

> Huduma za kipolisi, kwa kiasi kikubwa uhalifu wa unyang'anyi umepungua, vikundi vya uhalifu kama panya road, watoto wa Mbwa, vimedhibitiwa, hata changamoto ya kuel kibiti, mapango ya Amboni, Mwanza, kote kumedhibitiwa.
Kasoro kubwa ilikuwa utekaji ambapo kwa sehemu kubwa wapinzani wanaishutumu serikali.
Huduma za ulinzi imejitahidi sana, lakini kasoro ipo kwenye utekaji kwa watu wasiojulikana.

3. UTALII
3.1 Uanzishwaji wa TANZANIA SAFARI CHANEL
Kupitia chanel hii utalii wa nchi unatangazwa ndani na nje ya Tanzania, tunatangaza nchi yetu, hivyo utalii utakua. Lakini pia wapo watanzania wenzetu wamepata ajira pale.
Changamoto ya Chanel hii ni kuwa Hakuna ubunifu, mambo yanarudiwa yale yale kila siku utadhani hakuna mambo mengine. Nafahamu ubunifu uanenda sambamba na uwekezaji, serikali ihakikishe vijana wanakusanya taarifa za kuvutia ili zirushwe luningani.

3.2 Kuzipandisha hadhi mapori na kuwa hifadhi
> Serikali hii imepandisha hadhi baadhi ya mapori na kuwa hifadhi matahalani mapori ya akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi. Manufaa yatakajikita katika uimarishaji wa utalii pamoja na ulinzi katika mapori hayo.
Pia kupitia upandishaji hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ajira zimezalishwa kwa watakaozihudumia hifadhi hizo.

Lisu hapaswi kuziponda kazi za Magufuli, katika hilo anakosea, na anatukosea watanzania hasa wale ambao hatuna mrengo wowote zaidi ya kuangalia maslahi ya nchi.

Lisu kuziponda kazi za Magufuli unapoteza baadhi ya kura kwa wale wanaoziona.

Lisu unapaswa uponde yale mapungufu aliyonayo Magufuli katika utendaji wake kwa kulitumikia taifa hili. Mimi naunga mkono mtu anayetenda haki, asiye na upendeleo.

Mtu asiye na mawe mawili ya kupimia, mtu asiye mnafiki.

Ninapenda Lisu na Magufuli washirikiane, iwe ni Lisu kashindwa au Magufuli kashindwa. Wote ni Watanzania.

Mbeya na Iringa bado kugumu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Ahsante Robert, uandishi wa hali ya juuuuuuu, Great Thinker,
 
CCM inawateja wake wa kwenye nyumba za tembe(Simiyu, Singida, Dodoma, Pwani, Tabora, Shinyanga, Geita, Kigoma, Rukwa, Katavi, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Songwe na Njombe).
 
MBEYA NA IRINGA BADO NGOMA NGUMU

Na, Robert Heriel

Kama kuna majimbo ambayo CCM itahangaika sana ni pamoja na Iringa Mjini, Mbarali, Mbeya Mjini, na Tunduma Mjini.

Kanda ya juu Kusini sasa ndio itakuwa kambi Rasmi ya Upinzani tofauti na sasa ambapo Kanda ya kaskazini mashariki yaani Arusha na Moshi Mjini.

Ni rahisi Kwa CCM kupata jimbo la la Moshi mjini na Arusha Mjini Kuliko Kuyapata Majimbo ya Iringa Mjini na Mbeya Mjini.
Sitashangaa kutokumuona Lema na mbunge atakayepeperusha bendera ya CHADEMA pale moshi mjini,

Tulia Ackson namuona kama Mpambanaji anayejaribu bahati yake, lakini uhakika ni kuwa hawezi kupata ubunge hapo Mbeya Mjini. Jimbo la Mbeya mjini ni gumu mno zaidi ya majimbo mengine. Sitashangaa Sugu akimshinda Tulia kwa kura zaidi ya elfu ishirini, hilo halitanishangaza kabisa.

Kitu pekee ambacho ninakiona katika majimbo hayo ni muitikio wa wanawake kwenye siasa pamoja na wanaume watu wazima. Nafahamu wanawake ndio wapiga kura wakubwa na watu wazima.

Mbeya Mjini na Iringa wakina mama ni wengi wanaoukubali Upinzani, kina baba ni wengi wanaoukubali upinzani. Achilia mbali vijana ambao kimsingi ndio wapinzani wenyewe lakini hawa wengi wao sio wapiga kura. Kina mama na wababa ukiona wanakusapoti basi kuwa na uhakika kwamba utashinda.

Arusha na Moshi Mjini kwa sasa inapoteza sifa yake, ni kama wameishiwa pumzi, nina uhakika jimbo moja kati ya Moshi mjini au Arusha mjini Mwaka huu lazima liende CCM. na kama Upinzani hawatakuwa makini wanaweza kupoteza majimbo yote mawili.

Kwa upande wa Mbowe pale Hai, mwaka huu atashinda lakini kwa Kura chache sana.

Majimbo mengine ambayo CCM itaonja joto la jiwe ni pamoja na Mikumi kwa Profesa Jay, Kigoma mjini, Tunduma, Tarime Vijijini, Bunda huyu atashinda kwa kura chache,

Majimbo ambayo yapo hati hati kuchukuliwa na CCM ni KAWE kwa Halima Mdee, Ubungo hili litachukuliwa asubuhi kabla magari yanayotoka Dar hayajafika morogoro. Kibamba hili nalo litachukuliwa mapema tuu.

CCM mwaka huu itachukua majimbo mengi ya Upinzani, lakini litashindwa kuchukua majimbo ya Iringa mjini na Mbeya mjini.

Kwa upande wa Jimbo la Singida mashariki alipokuwa Tundu Lisu, upinzani utachukua kwa kura chache.

Upande wa Urais, mgombea wa Upinzani, atachukua kura nyingi jimbo la Iringa Mjini, mbeya mjini, Mikumi, Kigoma mjini, kusini na kaskazini, Tarime vijijini, Bunda nusu nusu, Arusha mjini Nusu kwa Nusu, Moshi Mjini nusu kwa Nusu, Karatu mpinzani atashinda, Majimbo mengi ya Singida watagawana na CCM, Zanzibar upinzani utashinda ikiwa watasimamisha mgombea mmoja.

Kama Lisu atapitishwa na NEC atapigwa kwenye majimbo mengi na Magufuli, labda abadilishe mbinu hasa katika utoaji wa hotuba.

Ni ngumu Lisu kumshinda Magufuli lakini kama atabadili hotuba zake Lisu anaweza kushinda hata kwa kura laki moja.

Mambo ambayo Lisu lazima ayaongelee ili apewe kura na kumzidi Magufuli

1. Ajira kwa vijana na namna ya kuondoa umasikini
Lisu lazima awashawishi vijana ambao wengi kwa sasa hawana ajira, Lisu lazima atumie ushawishi mkubwa kuhakikisha anageuza nyoyo za vijana, aseme ataajiri vijana,

Hoja hii Atamzidi Magufuli kwa sababu ni wazi awamu hii Magufuli hajaajiri vijana wengi, hivyo kufanya vijana wengi kubaki mtaani wakiwa wamezubaa.

Magufuli hoja hii hawezi kuitumia kwani ataonekana anaongea uongo, tena ataonekana anawadharau vijana kwa kuongea uongo wa mchana kweupe. Najua hawezi kusema kuwa ataajiri akipewa tena, kwani vijana watamuambia kama ulishindwa kutuajiri awamu ya kwanza basi hata awamu ya pili utashindwa.

2. Nyongeza ya Mishahara, na kupanda madaraja.
Lisu anaweza akashinda, ikiwa atatoa maneno yenye kushawishi wafanyakazi na watumishi wa UMMA kuhusiana na nyongeza ya mishahara na kupanda vyeo.

Wafanyakazi wengi hawajaongezewa mishahara tangu Magufuli aingie madarakani, hakuna mtumishi anayelifurahia hili lakini watafanya nini ikiwa waliambiwa kama mshahara mdogo waache kazi.

Lisu lazima aeleze kuwa serikali isipoongeza mshahara inatengeneza mazingira hata kwa sekta binafsi kupunguza mishahara ya wafanyakazi wao.

Lisu lazima aseme kuwa endapo serikali haiajiri inasababisha thamani ya elimu kushuka, na wataalamu kulipwa ujira mdogo kwenye sekta binafsi.

Lisu lazima atoe mifano kuwa serikali inapogoma kuajiri inasababisha vijana wasomi kuwa cheap labor. Atoe mifano kuwa wapo wasomi wa ngazi ya shahada wanaolipwa laki moja, wengine wakijitolea kwenye sekta binafsi miaka nenda rudi wakisubiri ajira lakini mtoa ajira yupo kimya.

Lisu lazima azungumzie suala la vijana wa viwandani wanaolipwa chini ya laki themanini huku wakifanya kazi masaa kumi na mbili.

Hili magufuli kashindwa kulitolea maelezo, na penginde muda huo hana.

3. Unyonyaji wa wazungu
Lisu lazima azungumzie suala la makampuni ya kigeni yaliyokuja kuwekeza hapa nchini na namna yanavyolinyonya taifa hili.

Lisu hapaswi kukaa kimya kuwakemea wazungu.

Katika hili Magufuli amemzidi kwa mbali kabisa, Magufuli amejipambanua kwa kuwakemea wazungu, hata mimi namsapoti.

4. Uhuru wa Vyombo vya habari
Lisu katika hili namuona akijitahidi kulibeba, na linampa nguvu kubwa kwa watu wengi hasa wenye taaluma.

Magufuli hapa atashindwa kwani amekuwa nyuma katika hili wakati yeye anayomamlaka namba moja hapa nchini

5. Haki za Binadamu
Lisu katika hili kajidhatiti, nafikiri ni kwa vile yeye ni mwanasheria. Lisu lazima apigilie misumari kwa matukio ya kikatili ambayo yametokea nchi hii na vyombo husika havijafuatilia, matukio ya utekaji, mauaji, unyanyasaji, upendeleo miongoni mwa mambo mengine.

Lisu hili linambeba kwa watu wote wenye hofu ya Mungu, waasomi na watu wanaojua dunia ipo wapi.

Lisu atafeli katika hoja hii pale atakaposhindwa kueleza mipaka ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya ushoga, usagaji, umalaya, kutupa picha za uchi mitandaoni, ambapo kimsingi katika Hili Magufuli naye kajipambanua.

Lisu lazima atoke hadharani aseme kuwa tunapenda haki, lakini sio haki zinazovunja utu wa mwanadamu, aseme kuwa hataruhusu ushoga, wasagaji na wahuni kulingana na sheria za nchi yetu.

Lisu amezidiwa hapa na Magufuli kwa sababu Anashindwa kueleza kinagaubaga tena kwa ukali kuwa Ushoga ni kosa. Magufuli katika hili amemshinda. Na hili linambeba.

6. Kukemea na Kutokomeza Rushwa na Ufisadi.
Lisu lazima akemee Rushwa na Ufisadi. Lisu ni mwanasheria hivyo anajua ni kwa namna gani anaweza kulisaidia taifa hili kwa kutokomeza Rushwa na Ufisadi.

Lisu atachaguliwa na Watanzania kwa kukema Rushwa na Ufisadi.

Magufuli katika hoja ya Rushwa na Ufisadi amejidhatiti na kajitahidi kwa kiasi chake. Shida ya Magufuli ni pale ambapo hatuoni Fisadi yeyote aliyefungwa licha ya kuanzishwa kwa mahakama ya Ufisadi. Niliwahi sikia wapo waliwekwa rumande lakini baadaye waliambiwa walipe kisha watolewe. Hiyo binafsi ilinifanya nione kama igizo la kuchekesha.

Wezi wa kuku nao wangeambiwa warudishe kuku watolewe, wezi wa maduka, n.k
Hata hivyo siasa inamambo mengi, kwa umri wangu mengine pengine yakawa sio level yangu. Lakini kwa akili ya kawaida, jambo lile lilikuwa sio zuri.

7. Mahusiano Mazuri ndani ya Nchi na jumuiya za Kimataifa.
Lisu lazima aeleze kwa kina ni mahusiano yapi ayatakayo baina ya nchi yetu na mataifa mengine.

Magufuli katika hili kajidhatiti kikamilifu kuwa, yeye hana shida na taifa lolote, anahitaji uhusiano mzuri na mataifa mengine, lakini mahusiano hayo sharti yawe na maslahi kwa taifa letu. Hiyo nampa Tiki, hata mimi ningekuwa Rais ningefanya kama yeye, nchi kama inataka kukunyonya au kukulalia unaipiga mtama wa mchomvu. Lazima kuwe na mutual relationship.

Kuhusu Kuzikana, ni kweli MAGUFULI anafanya isivyo halali kutokwenda kwenye misiba ya wakubwa wenzake huko nchi za nje, lakini nami nasema sio kila msiba lazima aende, angalau msiba mmoja kwa misiba minne aende. Asipoenda kabisa inaonekana hana upendo, akienda kila msiba ataitwa Rais wa Misiba.

Kwa upande wa ndani ya nchi, Magufuli nimeshawahi kuona kwenye media viongozi kadhaa wa upinzani wakialikwa ikulu au pengine kwenda wao wenyewe. Magufuli anafanya vizuri katika hilo. Kuhusu CHADEMA kutoitwa Ikulu, kama hujaitwa IKULU na unalolote la kuongea na Rais, nini kilikuzuia, viongozi wa CHADEMA kama hamkuitwa Ikulu, mngepaswa muende ninyi. Hapa Magufuli hana makosa, vinginevyo awe aliwahi kufuatwa na viongozi wa CHADEMA akakata, kwa kweli hata mtanzania wa kawaida akisikia ataona Magufuli hajafanya vizuri.

Kuhusu Mikutano ya Kisiasa, ni kweli kabisa kuna muda wa siasa na muda wa kazi. Lakini hatuwezi kusahau kuwa wapo watu wamesomea taaluma ya siasa, yaani siasa kwao ni kazi. Kuwazuia vyama upinzani kufanya siasa kwa miaka karibu mitano wakati CCM tunawaona wakifanya mikutano yao hapa na pale haikuwa vizuri. Lisu katika hili watanzania wenye kupenda haki na wasomi watamuelewa.

8. MAENDELEO
Lisu lazima atuambie ni namna gani atatuletea maendeleo katika miundombinu, huduma za kijamii, kilimo, mawasiliano, viwanda, usafirishaji n.k

Magufuli katika hili kafanikiwa kwa asilimia kubwa. Hapa Magufuli hatatumia nguvu kubwa kwani tayari amefanya kwa kiasi maendeleo,
Magufuli kafanya yafuatayo kwa kipindi chake
1. SEKTA YA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI

1.1. RELI
Kafufua reli ya kaskazini, DSM, Tanga, Moshi na Arusha. Hii niliipanda mwezi wa pili.
Kujenga Reli ya Kisasa SGR, HII nami nimeikagua imefikia pazuri
Kununua na kukarabati mabehewa na miundombinu ya Reli pamoja na Treni

1.2. NDEGE
Kafufua shirika la ndege kwa kununua ndede za kisasa, Nadhani mpaka sasa Tangu aingie madarakani kanunua ndege 6.
Kajenge Terminal 3 pale uwanja wa Julius kambarage Nyerere
Kajenga uwanja wa Ndege Chato. Japo wapinzani wake wanakosoa vikali, lakini Chato pia ni Tanzania.

1.3. Barabara
Magufuli kajenga barabara na kuzikarabati barabara nyingi hapa Tanzania

2. HUDUMA ZA KIJAMII
Magufuli kajenga hospitali nyingi za wilaya na kuzikarabati. Japo kuna changamoto ya madaktari na madawa lakini atapongezwa na kila mtu muungwana kwa kufanaya hivyo.

Magufuli chini ya serikali ya awamu yake, umeme umetambazwa kwa kiasi kikubwa vijijini, pia tatizo la umeme sio sana

Maji, kwa sehemu kubwa hasa mjini serikali imejitahidi kuwapa wananchi maji. Lakini bado changamoto ni kubwa.

Serikali imejitahidi kutoa elimu bure kwa ngazi ya msingi mpaka shule ya upili kidato cha nne. Pia madawati kwa sehemu za mjini kwa kiasi kikubwa. Lakini bado miundombinu ya elimu bado haijatengemaa. Lakini angalau amepagusia.

Huduma za kipolisi, kwa kiasi kikubwa uhalifu wa unyang'anyi umepungua, vikundi vya uhalifu kama panya road, watoto wa Mbwa, vimedhibitiwa, hata changamoto ya kuel kibiti, mapango ya Amboni, Mwanza, kote kumedhibitiwa.
Kasoro kubwa ilikuwa utekaji ambapo kwa sehemu kubwa wapinzani wanaishutumu serikali.
Huduma za ulinzi imejitahidi sana, lakini kasoro ipo kwenye utekaji kwa watu wasiojulikana.

3. UTALII
3.1 Uanzishwaji wa TANZANIA SAFARI CHANEL
Kupitia chanel hii utalii wa nchi unatangazwa ndani na nje ya Tanzania, tunatangaza nchi yetu, hivyo utalii utakua. Lakini pia wapo watanzania wenzetu wamepata ajira pale.
Changamoto ya Chanel hii ni kuwa Hakuna ubunifu, mambo yanarudiwa yale yale kila siku utadhani hakuna mambo mengine. Nafahamu ubunifu uanenda sambamba na uwekezaji, serikali ihakikishe vijana wanakusanya taarifa za kuvutia ili zirushwe luningani.

3.2 Kuzipandisha hadhi mapori na kuwa hifadhi
Serikali hii imepandisha hadhi baadhi ya mapori na kuwa hifadhi matahalani mapori ya akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi. Manufaa yatakajikita katika uimarishaji wa utalii pamoja na ulinzi katika mapori hayo.
Pia kupitia upandishaji hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ajira zimezalishwa kwa watakaozihudumia hifadhi hizo.

Lisu hapaswi kuziponda kazi za Magufuli, katika hilo anakosea, na anatukosea watanzania hasa wale ambao hatuna mrengo wowote zaidi ya kuangalia maslahi ya nchi.

Lisu kuziponda kazi za Magufuli unapoteza baadhi ya kura kwa wale wanaoziona.

Lisu unapaswa uponde yale mapungufu aliyonayo Magufuli katika utendaji wake kwa kulitumikia taifa hili. Mimi naunga mkono mtu anayetenda haki, asiye na upendeleo.

Mtu asiye na mawe mawili ya kupimia, mtu asiye mnafiki.

Ninapenda Lisu na Magufuli washirikiane, iwe ni Lisu kashindwa au Magufuli kashindwa. Wote ni Watanzania.

Mbeya na Iringa bado kugumu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

Bandiko lako lina ubora wa 80%+. Hii ndio aina ya uchambuzi, sio yale mabandiko ya kina Paskali ya kujiita wazalendo na kujifanya hawaegemei popote. Tena huko kujiita wazalendo wanaanza kwenye paragraph ya mwanzo, badala ya kutuacha tupime wenyewe. Huu ndio uandishi wa kizalendo, na sio huu uzalendo academia wa kina Paskali kuvutia watawala kwa maslahi binafsi.

Cc: Paskali Mayalla
 
Utaanzaje kuingia geti la Ikulu bila ukaribisho wa mwenye kukalia Ikulu?
Kuhusu CHADEMA kutoitwa Ikulu, kama hujaitwa IKULU na unalolote la kuongea na Rais, nini kilikuzuia, viongozi wa CHADEMA kama hamkuitwa Ikulu, mngepaswa muende ninyi. Hapa Magufuli hana makosa, vinginevyo awe aliwahi kufuatwa na viongozi wa CHADEMA akakata, kwa kweli hata mtanzania wa kawaida akisikia ataona Magufuli hajafanya vizuri.
 
Back
Top Bottom