Mbeya: Madiwani wapiga marufuku Usajili mpya wa Bajaji, wadai zimekuwa nyingi kuliko mahitaji

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,997
142,017
Baraza la Madiwani Jijini Mbeya limepiga marufuku Usajili mpya wa Bajaj kwa sababu zimekuwa nyingi kupitiliza mahitaji.

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya amesema Usajili utakaofanywa ni ule wa replacement baada ya Bajaj kuchakaa hivyo mmiliki ataruhusiwa kununua mpya.

Chanzo: ITV habari

===============

Baraza la Madiwani Jijini Mbeya limesitisha usajili mpya wa usafiri wa Bajaj kwa sababu zimekuwa nyingi kuliko mahitaji huku barabara ikiwa finyu pamoja na kusababisha ajali mara kwa mara.

Mfumo wa usajili umefungwa hadi wakati ambapo miundombinu itakapokuwa rafiki kwa matumizi. Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Triphonia Kisiga amesema Bajaj zilizosajiliwa Mkoani hapo ni 3000.

Naye, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mohamed Issa amesema “Mbeya imekuwa kama dampo la Bajaj, imefika hatua tunasema Hapana.”
 
Baraza la Madiwani Jijini Mbeya limepiga marufuku Usajili mpya wa Bajaj kwa sababu zimekuwa nyingi kupitiliza mahitaji

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya amesema Usajili utakaofanywa ni ule wa replacement baada ya Bajaj kuchakaa hivyo mmiliki ataruhusiwa kununua mpya

Source ITV habari
Mbeya michosho sna eti biashra kubwa wanazomiliki Ni bajaji hkn pesa pale Ni uzushi tu na ndio maan Ni maish Ni marais
 
Iringa napo bajaj ni kama manzi yale ya chooni makubwa! Bado dar Kunanzia Mbezi Luis aisee ni kero haijapata konekana zinasimama katikati ya barabara wakigombeana abiria! Kwa dar, kwanini bajaji zisihudumie njia za ndani tu, na sio barabara kubwa kama hiyo ya kimataifa MOROGORO ROAD! Bora hata zile kero za vi hiaceVIPANYA kipindi ile
 
Baraza la Madiwani Jijini Mbeya limepiga marufuku Usajili mpya wa Bajaj kwa sababu zimekuwa nyingi kupitiliza mahitaji

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya amesema Usajili utakaofanywa ni ule wa replacement baada ya Bajaj kuchakaa hivyo mmiliki ataruhusiwa kununua mpya

Chanzo: ITV habari
Hongera Mbeya kwa kuchukua hatua,angalau mmefanya mmeona tatizo na kufanya maamuzi,kwamba maamuzi yatapokelewaje ni jambo jingine.

Nilisema hapa nyumba Bajaji na Bodaboda ni Bomu linalosubiriwa kulipuka,hatua mbalimbali kama hizi zinahitajika kuchukuliwa kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom