KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,772
- 21,489
Issue ya Ngwisa na Polisi ilikuwa hivi, marehemu Mapugilo alikuwa na wake wa Tatu. Mama yake Ngwisa ndio alikuwa Bi mdogo. Ngwisa akamfukuza Stella ambaye ni mtoto wa dada yake ila mama tofauti na Ngwisa. Pia baadae akawatimua na ndugu zake wengine. Wakaenda Polisi. Mamwela wakaja na 110 Lao akawapiga sana, ndipo wakaenda kuleta ma bunduki na mabomu ya machozi. Manjagu walipiga mabomu kuanzia saa tisa Alasiri hadi kesho yake asubuhi, Ngwisa alikuwa akizidiwa na Moshi wa mabomu anatoka na shoka lake anawatimua Polisi ndipo wataanza kumlenga kwa risasi. Kesho yake akaja RPC akambembeleza Ngwisa aende Polisi ndio hicho kisa cha NgwisaNakumbuka enzi hizo Uncle Ngwisa Mapugilo,alikuwa mbabe hasa Mbeya manispaa walikataza kuchunga n'gombe pale makuburi ya Loleza,yeye akapeleka n'gombe,kuchunga akatumiwa polisi hii issue Nilishuhudia live aliwapiga na akaenda kuchukua shoka kufuata mifugo yake siku kadhaa mbele wakamkamata baada ya kupiga bomu la machozi sokomatola hiyo
Bisso Ntepa ni mlokole tena, ana kanisa lake hapo Dar. Nilikuwa naye hapa mbeya last week.Pia kulikuwa na Bisso Ntepa, alisha fungwa mara kadhaa kwa ujambazi baadae akaokoka na kufungua kanisa lake DSM. Baadae akaachana na kanisa na kujiunga na bongo movie. Miaka minne nyuma nilimuona anaendesha daladala kubwaa
Karibu sana Mbeya, Pareto ya Uyole ipo mkuu.Mimi naikumbuka Mbeya ya 1975/1977. Reli ya Tazara inazinduliwa 1976 tulipanda train iliyotoka Kapiri Mposhi tukashuka Makambako tukarudi Mbeya kwa gari VW combi. Nilikuwa na viwanja vya golf kabla ya kugeuzwa matumizi ili ujengwe uwanja mkubwa wa michezo. Tulishiriki katika Ujenzi wa Uwanja wa Mapinduzi ( Sokoine) tukitokea Majengo primary school tukishirikiana na wanafunzi wa Sisimba, Mbaya, Azimio hiyo ilikuwa 1976 etc. Mwalimu Mkuu Malengo alikuwa Mwl Mwangomile na Mbaya alikuwa Mwakang'ata.
Nakumbuka kulikuwa na kikundi cha Sanaa kilichoitwa Chamnambe kikiongozwa na Mzee Ryoba. Kulikuwa na shule inaitwa Muungano ilikuwa msituni njia ya Mwanjelwa sijui kama bado ipo. Pia nakumbuka Pareto ya uyole. Those old good days.
Pia nakumbuka 1976 ilitokea ajali kubwa ya basi likiitwa Mwambipile Bus Service ilipinduka huko Mwakaleli ikaua watu wengi sana.
Sijafika Mbeya Tangu Dec. 1977, nasikia imebadilika mno.
Safi SanaBisso Ntepa ni mlokole tena, ana kanisa lake hapo Dar. Nilikuwa naye hapa mbeya last week.
Nilisoma Sisimba ya Msuya, akahama akaja Mtawa.12 inanihusu direct shule ya katikati ya jiji iliyopo mlimani, wale wa Sisimba wapite tufahamiane
Mkakile, Amini alifarikiAisee. Kuna nyumba ya kina Kajigili pale karibu na Moravian jirani yao. Nakumbuka kuna jamaa yangu alikuwa anaitwa Amini na kina Mwaikakile. Kwenye zile kota kulikuwa kuna mtu anaitwa Mfula Mohamed.
Aisee! Huyo pamoja na Elisha kajigili tulikuwa ni marafiki sana na majirani pia.Mkakile, Amini alifariki
Mkuu! Bila shaka unamaanisha MNASI, pale jirani na AgaKhan!Then Mmasi baadae
Nimekupata ....mdau mzee wa Rockers hizi id zinaficha watu ha ha haaMimi Sajo, hao madogo walikuwa bado wanacheza chandimu wakati mimi nacheza Rockers United.Dogo wangu aliitwa Prince Lugax rapa wa mwanzo mwanzo kampani ya kina Sugu
Mamkwe amenifundisha muungano ....Mwailima pia amenifundisha hesabu ....amenifundisha hesabu za maumbo .....mzingo ....pia kulikuwa na mwalimu flani kilema Yessaya wa yessaya kanifundisha historia .....huyu mwalimu ilikuwa usipoandika notisi zake za darasani lazima uchezee fimbo .....lakini pia alikuwa akipokea hongo ya shilingi ishirini ili asikuchape .....Wale wa Muungano Primary kulikuwa na mwalimu Mwailima,Mecky,John David,Mamkwe etc bila kumsahau Ester David
Mamkwe kanifundisha hesabu na Mwailima kanifundisha Science Kilimo. Mwailima alikuwa anapiga bakora mpaka 20Mamkwe amenifundisha muungano ....Mwailima pia amenifundisha hesabu ....amenifundisha hesabu za maumbo .....mzingo ....pia kulikuwa na mwalimu flani kilema Yessaya wa yessaya kanifundisha historia .....huyu mwalimu ilikuwa usipoandika notisi zake za darasani lazima uchezee fimbo .....lakini pia alikuwa akipokea hongo ya shilingi ishirini ili asikuchape .....
daah kitambo sanaaa!! dr. Kasimbazi saiz kachakaa,kawa kama mwehu,pombe zimeshamuharibuNimemkumbuka mzee remmy wa kule sokomatola alikuwa mwanamziki na mchezaji mzuri sana wa drafti, wakina Devi, mzee wa kuholamaka, mzee ramadhani. Nimemkumbuka pia dr. Kasimbazi, dr. Salehe n.k.