Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,833
- 155,780
Mbeya ni mkoa mzuri sana kijografia, ukiwa umezungukwa na milima na vilima. Mito na vijito, hali nzuri ya hewa, udongo mzuri wenye rutuba na mambo mengi mazuri.
Watu wa Mbeya ni wakarimu sana, watoaji na wenye upendo, ila ukiwazingua wanakuzingua mara milioni sita zaidi.
Mbeya kuna mandhari ya kuvutia. Kuna vivutio kibao vya utalii, kama kona ya taifa, hii ni bonge ya kona, iko kwenye barabara ya lami itokayo Cape Town Afrika ya Kusini kwenda Cairo Misri kupitia Chunya kwa Masache Kasaka a.k.a Man Kasa mbunge wa Lupa Chunya.
Hii ni picha ya kona ya Taifa, iliyopigwa na Fadhy, Fadhili Mtanga, mpishi anaye andika na kupiga picha.
Kivutio kingine ni ziwa Masoko.
Hili ni ziwa lililoko mlimani, crater lake. Ziwa hili limekaa mithili ya lulu ipatikanayo kwenye samaki aina ya chaza (Oysters). Lulu hiyo kwa Kinyakyusa huitwa pearl.
Mbeya imejaaliwa bwana, pia juna ziwa Kisiba, ziwa la msituni. Ziwa hili liko kwenye msitu asilia, ile misitu inayojulikana kwa jina la rain forest. Hutojuta kabisa kufika mahali hapa.
Kwa wanaopenda kuoanda milima, Mbeya ni mahali sahihi kabisa kwa burudani hiyo. Kuna mlima Loleza, huu ni mlima mzuri sana na rahisi kupanda na wala hauko mbali na mji.
Shule ya sekondari ya wasichana ya Loleza ilipewa jina hili kwababu iko chini ya Mlima Loleza.
Picha hii ilipigwa na Fadhy, Fadhili Mtanga ikionyesha mlima Loleza unavyoonekana ukiwa Mwanjelwa, pale mahali ambapo soko liliungua. Nimepamiss sana home.
Mlima Rungwe, mlima huu una urefu wa meta 2,981. Mlima huu uko wilayani Rungwe. Unakaribishwa sana kutembelea mkoa huu, wenye neema nyingi za kutosha.
Picha mbili zikionesha mandhari tofauti za mlima Rungwe.
Mashamba ya Chai Katumba
Haya ni mashamba yaliyopo Katumba, Tukuyu. Mashamba haya yana muonekano mzuri sana, na jali ya hewa ni nzuri sana. Hakika ukifika Katumba, utabakiwa na kumbukumbu isiyofutika kamwe