Mbeya kuna Daktari anaitwa Danny, serikali imeshindwa kumuwajibisha?

Amefanya OPs ngapi kwa ujumla na ngapi zimekuwa na madhara.? Kwa uwiano na hospital nyingine kwa madhara yatokanayo na pasuaji hizo yeye yuko wapi?. Kwa gharama ukilinganisha na hospitality binafsi nyingine kwa upasuaji ule ule yeye ana nafuu au ni ghali kupindukia?
Yeye binafsi anajiita dr bingwa wa mifupa au Wateja ndio wamwita hivyo? Mbeya hamna dr bingwa wa mifupa aliyeajiriwa na serikali? Kwa nini wagonjwa waende kwake?
Ukienda MOI pasuaji azifanyazo hufanya na specialist Tu au na registrars hufanya?
Na mikoa mingine kuna orhopedicians wangapi? Watu hawavunjiki? Nani huwatibia? Wote waenda MOI na KCMC?.Kabla yake hao Wateja wake walitibiwa wapi?
 
Naunga mkono sehemu ya Maelezo yako kuhusu huyu daktari,kama ni mwenyewe "Danny".
Huyu ni dr mzuri wa mifupa,ni kweli alifukuzwa hosptali ya Peramiho lakini wakati anahamishiwa mbeya alikuwa akifanya kazi hosptali ya Mkoa wa Ruvuma na kuna wakati alikaimu nafasi ya mganga mkuu wa wilaya

Pamoja na mambo mengine shida kubwa ya huyu Dr ni mpenda pesa,bila pesa hawezi kukufanyia upasuaji mzuri,na wakati mwingine yupo tayari akuache uendelee kuteseka kama huna kiwango cha pesa akitakacho.

Wagonjwa wengi wanaokwenda hosptali ya serikali ambapo ni muajiriwa uwaamuru kufanyiwa oparation ki-private vinginevyo anakwambia live kuwa kama huna kiwango cha pesa akitakacho,anakwambia "utakufa bwana,au mgonjwa wako atakufa".

Kuna kipindi wakati akiwatembelea wagonjwa wodini alikuwa maalufu kwa kutaja figure huku akiwa ameshikilia kadi ya mgonjwa,utasikia akisema Wewe laki 7, Akiimanisha oparation yako itakugharimu kiasi hicho na kama huna mguu wako au kiungo chako kitaoza.

Nakumbuka alifanya hivyo kwa jamaa yangu ,ikabidi tutafute laki 7 ndo akafanyiwa upasuaji.
Kiwango chake cha chini ilikuwa ni laki 5.

Kuna kesi nyingi za namna hiyo zilitokea hosptali ya mkoa wa Ruvuma na ilikuwa ni sehemu ya kashfa zilizo mfanya ahamishwe Mbeya.
Nikweli hata Mimi rafiki yangu alivunjika mguu Ruvuma alipo lazwa hospital ya mkoa tukakutana Danny akataka 600000 kesho baada ya siku mbili kutimia ndipo akamfanyia upasuaji

Huyu jamaa ni balaa
 
Hahhahaha, JF bhana.


Dr Danny nimefanya naye kazi kwa muda mrefu tangu akiwa Peramiho mission kabla ya kuhamia Hospitali ya mkoa wa Ruvuma (HOMSO), ni kwamba jamaa priority yake ni pesa na kama hauna pesa anayotaka hawezi kukuhudumia au mgonjwa wako hatomuhudumia.



Akikuhudumia una asilimia kubwa ya kupona kwani wagonjwa wengi wanaokuja kwake wanakuwa wameshindikana kwenye hospitali nyingi hivyo wanaelekezwa kwake, wagonjwa wanatoka mikoa mbalimbali kumfuata popote atakapokuwepo kwani anao uwezo mkubwa usio wa kawaida katika mambo ya mifupa.


Nashauri kama ndugu yangu ana tatizo la mifupa lililoshindikana wamuone huyu jamaa kwani anaweza.



Mkuu mleta mada tatizo alilopata mgonjwa hilo la PULMONARY EMBOLISM ni moja ya complications za operation hivyo usihusishe na habari uliyoleta au usije ukafikiri tatizo hilo anasababisha Danny..



Ninachoweza kusema ni kwamba Dr Danny hapendwi na madaktari wengi kwani huwa hana tabia ya kutoa commission kwa madaktari au manesi amabao wanamletea wagonjwa ama wateja hivyo fitna ni kawaida kwake, hata alipokuwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma walimpiga fitna sana pale kitengo cha mifupa kwa sababu alikuwa anapiga sana hela na vifaa vyote vilikuwa vyake hivyo hospitali ilikuwa haifaidi chochote kwani kitengo cha mifupa kilionekana kama cha mtu binafsi na gharama kuwa kubwa.



Labda niseme tu majungu siyo mtaji, hata Danny akizuiwa kutoa huduma bado mleta mada hutofaidika na chochote.



Tufanye kazi!
 
Umesema ana degree moja tuwekee hapa hicho cha degree moja ya udaktari ambacho wewe unadai ili nasi tuthibitishe vinginevyo ni majungu.na hivyo vyeti vya hao ambao unadai amewasababishia vifo unavyo na vinasema hivyo kuwa yeye ndiye msababishaji.
Crap.....
 
Nimeenda Mbeya nikamkuta daktari anaitwa Danny! Anatamba hata kipindi hiki cha daktari Magufuli.

Anajiita Daktari Bingwa wa Mifupa wakati ana degree moja tu.

Alihamishwa toka Peramiho na kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mbeya.

Amesababisha vifo vingi kutokana na kufanya upasuaji asiosomea.

Mwezi wa tatu mwaka huu alisababisha kifo cha mwendesha bodaboda aliyekuwa akiitwa Festo aliyelazwa hospitali ya rufaa Mbeya baada ya kugongwa na gari ya mmiliki wa hotel moja iitwayo Kwetu Pazuri.

Haijulikani Danny alipata wapi taarifa za huyo mgonjwa kulazwa hospitali ya Rufaa Mbeya na kisha mgonjwa akahamishwa na akaishia kufanyiwa operation hospitali ya private ya K's Hospital; hii ni baada ya mgonjwa Festo kuambiwa na madaktari wa hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya kwamba hawatoweza kuokoa mguu wake.

Danny baada ya kwenda kumfanyia operation hapo K's akagundua hawezi okoa mguu huo akiwa anaendelea na operation. Ndugu waliombwa watoe pesa za damu iliyoendwa kufuatwa benki ya damu Mbeya.

Danny ana mambo mengi sana yanayoaibisha madaktari.

Amewaacha watu wengi wakiwa vilema, ikiwamo mke wa mfanyabiashara mashuhuri wa jijini Mbeya (Babito).


Amekuwa na mtandao wa kuhamisha wagonjwa (ukiwahusisha manesi wa wodi hadi mafundi wa mionzi) waliopata ajali toka hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya (ambayo si hospitali yake) na kwenda kuwafanyia operation kwenye hospitali binafsi iitwayo K's Hospital, kwa gharama kubwa huku akiwaacha wagonjwa na vilema vya kudumu au vifo.

Ana ushirikiano na laboratory technician wa NBTS Mbeya (ipo Meta hospitali) katika kuwauzia ndugu damu.

Watu gani wanamlinda Danny? Je, walewale wanaomlinda 'Dr. Nyagori' wa Morogoro.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Update toka Mbeya
Siku tatu zilizopita, Dr. Danny kamfanyia operation ya mifupa mmoja wa madaktari wasaidizi katika hospitali anayofanyia hizi operation zake zisizo na sifa. Taarifa zinasema baada ya kumfanyia operation daktari huyu msaidizi alipata complication ya Pulmonary Embolism, yaani bonge la damu kuziba njia za mapafu na kwamba hii ilisababisha mgonjwa kuwa mahututi na sasa amelazwa hospitali ya kanda ya Mbeya, wodi za Tiba, akiwa mahututi.
Acha uongo ndugu yangu,majungu hayajengi,Dr.Danny ni Dr mzuri sana aliye bobea kwenye mifupa hayo unayo msingizia hayata kufikisha popote,zaidi ya kujipatia laana tu.
 
Hahhahaha, JF bhana.


Dr Danny nimefanya naye kazi kwa muda mrefu tangu akiwa Peramiho mission kabla ya kuhamia Hospitali ya mkoa wa Ruvuma (HOMSO), ni kwamba jamaa priority yake ni pesa na kama hauna pesa anayotaka hawezi kukuhudumia au mgonjwa wako hatomuhudumia.



Akikuhudumia una asilimia kubwa ya kupona kwani wagonjwa wengi wanaokuja kwake wanakuwa wameshindikana kwenye hospitali nyingi hivyo wanaelekezwa kwake, wagonjwa wanatoka mikoa mbalimbali kumfuata popote atakapokuwepo kwani anao uwezo mkubwa usio wa kawaida katika mambo ya mifupa.


Nashauri kama ndugu yangu ana tatizo la mifupa lililoshindikana wamuone huyu jamaa kwani anaweza.



Mkuu mleta mada tatizo alilopata mgonjwa hilo la PULMONARY EMBOLISM ni moja ya complications za operation hivyo usihusishe na habari uliyoleta au usije ukafikiri tatizo hilo anasababisha Danny..



Ninachoweza kusema ni kwamba Dr Danny hapendwi na madaktari wengi kwani huwa hana tabia ya kutoa commission kwa madaktari au manesi amabao wanamletea wagonjwa ama wateja hivyo fitna ni kawaida kwake, hata alipokuwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma walimpiga fitna sana pale kitengo cha mifupa kwa sababu alikuwa anapiga sana hela na vifaa vyote vilikuwa vyake hivyo hospitali ilikuwa haifaidi chochote kwani kitengo cha mifupa kilionekana kama cha mtu binafsi na gharama kuwa kubwa.



Labda niseme tu majungu siyo mtaji, hata Danny akizuiwa kutoa huduma bado mleta mada hutofaidika na chochote.



Tufanye kazi!
Actually umethibitisha kwamba anapiga hela, and he is corrupt
 
Madaktari ni miongoni mwa binadamu wajinga zaidi duniani, ma engineer ni miongoni mwa binadamu wenye akili zaidi duniani, nikipata mda ntakuja kufafanua
 
Usini quote kwa upuuzi wako, kama hauna pesa tembea mbele waache wenye hela zao watibiwe
You confirmed kwamba jamaa anapiga pesa.... Na kimaadili hilo ni kosa

Umemchoma mwenzako

Mbaya sana

Danny is corrupt
 
Dr Danny kama ni kweli basi kuna shida hapo lakini kama ni majungu basi kuna ugomvi hapo kati ya mtoa mada na Dr.

Kuna Mratibu wa Mkoa na Wilaya ambao hukagua hospitali na vituo vya private vya kutoa Huduma wakiambatana na Timu za uendeshaji za afya ya mkoa ( RHMT ) na Timu ya Wilaya ( CHMT )

Lakini kama kuna tuhuma za Huduma duni na vifo vyenye utata then Mamlaka zingine zipo kwa walalamikaji pelekeni huko ili mpatie haki zenu,Private Hospital zinatoa Huduma kwa niaba ya Serikali na kazi ya Serikali ni kumlinda kila RAIA.
 
Akili ni ya mtu binafsi, sio profession.

Madaktari ni miongoni mwa binadamu wajinga zaidi duniani, ma engineer ni miongoni mwa binadamu wenye akili zaidi duniani, nikipata mda ntakuja kufafanua
 
Inawezekana kakudanganya kabobea kwenye mifupa. Sasa muulize Danny wako kawaambia nini UWT baada ya kukalishwa kitimoto.

Acha uongo ndugu yangu,majungu hayajengi,Dr.Danny ni Dr mzuri sana aliye bobea kwenye mifupa hayo unayo msingizia hayata kufikisha popote,zaidi ya kujipatia laana tu.
 
Kama ni kweli basi huyu danny achukuliwe hatua madhubuti
Nimefuatilia sana huyu Dr. Danny, kuanzia peramiho mpaka alipo hapo mbeya, nimembiwa peramiho alikuwa anafanya kazi vizuri sana kiasi kwamba hata wafanyabiashara wakubwa wa mbeya kama vile tugimbe amewafanyia upasuaji na wapo safi. Alipotoka peramiho akawa kaimu mganga mkuu wa wilaya ya songea kwa miaka miwili, swali kama peramiho alifukuzwa kwa rushwa ikawaje awe mganga mkuu wa wilaya? Anyway akiwa peramiho hospitali ya kanda ya rufaa ya mbeya walikuwa wanamwomba kuja kufanya upasuaji huo huo wa mifupa, wakati huo huo rufaa mbeya kulikuwa na specialist watatu (ben, masandika na shuma) lakini wagonjwa walirundikana huyo Dr Dan alikuwa anakuja kufanya pamoja na kuwa na hiyo degree moja kulipwa vizuri tuu.Sasa kama hosp ya kanda ya rufaa ilikuwa inamwazima je unadhani uwezo wake kikazi ni wa kubabaisha?
Akiwa mganga mkuu wa wilaya pamoja na majukumu wa wilaya alikuwa anapasua pale mkoani songea, bila tatizo lolote kwa makubaliano kuwa atatumia vifaa vya upasuaji na vitalipiwa na wagonjwa walikuwa wanapata huduma vema. Kuhamishwa kwake ni kutoelewana yeye na mkurugenzi wa halmashauri wakati huo (sixbert) kutokana na.yeye kutumia pesa za idara ya afya ndivyo sivyo, na Danny alimwandikia barua za kuomba pesa za idara arudishe idarani ndo chanzo cha uhamisho.

Tangu amekuja mbeya ametibu wagonjwa wengi sana. Tukumbuke walikuwa wanatoka mbeya kumfuata songea sasa yupo mbeya. Wagonjwa wanafuata kazi nzuri na siyo majengo au vyeti vya watu kwa.sasa pia wagonjwa wanatoka malawi, zambia na kongo, jamani si kipaji alichopewa na Mungu?

Mmesema hafanyi upasuaji bila pesa ndo afanye, nimeenda pale ks hospital aliowafanyia jana, kiujanja nikaulizia waliofanyiwa kama wote wamelipa asilimia kubwa hawajalipa na tayari wamepata huduma bila tatizo.

Maswali ninayojiuliza,
1. Kama degree moja huruhusiwi kufanya upasuaji je Amo anaruhisiwa, mbona ifisi hakuna specialist lakini fuatilia upasuaji anafanya nani, nenda ikonda upasuaji huo huo wa mifupa anafanya specialist?
2. Kama hosp ya.rufaa ya kanda ipo na inafanya vema kwa nini wagonjwa watoroke kwenda kwa Danny kama anatengeneza vilema? Je rufaa kuna vifaa vya upasuaji? Je wanaokwenda private ya huyo Danny ni vichaa?
3.Kwa kazi mbaya na sifa mlizotoa kwa huyo Dany, Mbeya si ingeanza kuandamana kama walivyoandamana kwa Dr Ben(specialist) kutokana na kazi mbaya.
4 kuhusu kuiba au kuhamisha wagonjwa toka rufaa, je wanaokwenda peramiho, ikonda, ifisi wanahamishwa au ni utendaji mbovu wa mbeya rufaa kanda?

Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza. Tafadhali sana heshimuni kazi za watu na kama inawauma kuhusu uwezo wake fanyeni kwa bidii kujenga heshima kama ya huyo Dr Danny. Kwa ujumla mbeya tunampenda sana na anaokoa wagonjwa kila siku.

Na Mungu amnusuru na maneno ya wasiopenda mafanikio ya kazi yake.
 
Kazi kweli kweli, huu muda wa kuangaika na watu ungeutumia kujitafutia competency Zaidi ili ukapata nafasi nzuri pia. Simfahamu muhisika lkn through maelezo yenu tu mnaonesha mna fitina.
Haya mambo yapo ofisi nyingi, nina wasi wasi huyu jamaa ni competent na hataki ujinga.
 
Back
Top Bottom