Mbeya: Afisa Mionzi ahukumiwa kwa kujipatia Fedha kidanganyifu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Novemba 3, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya mbele ya Mhe Mtengeti Sangiwa, imeamuliwa Kesi ya Jinai na 215/2022, Jamuhuri dhidi ya
Lambert Haule ambaye ni Afisa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya.

Mshitakiwa huyo ameshtakiwa kwa kosa la kujipatia fedha kiasi cha sh. 1,000,000 /= kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Bi. Paulina Mbezi akidai kuwa atamsaidia kuongea na Maafisa wa TAKUKURU (M) Mbeya wasiendelee na uchunguzi wa makosa ya Rushwa unaoendelea dhidi yake.

Jambo hili lilikuwa ni la udanganyifu kwani Bi. Paulina Mbezi hakuwa na tuhuma za rushwa zilizokuwa zinachunguzwa na TAKUKURU (M) Mbeya.

Kosa hili ni kinyume na vifungu vya 301 na 302 vya Kanuni ya Adhabu [CAP 16 R.E 2022] pamoja na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Mashtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa hili na amehukumiwa kulipa faini ya sh 500,000/= au kwenda jela miaka 3.
 
alikutwa na vipande nyama ya swala jela miaka 22.

aliyetapeli milioni moja alipe tu faini ya 500,000.

hivi kuna Hakimu au Polisi anatarajia kuiona Pepo ?
 
Ah nchi mnashikilia vikesi vya hela ndogo wakati kuna watu wanakula
Mabilion wa matrilion hawafanywi kitu

Ova
 
Umedhulumu 1,000,000 anaambiwa alipe 500,000/= kweli ?Hakimu hayupo serious
 
Ah nchi mnashikilia vikesi vya hela ndogo wakati kuna watu wanakula
Mabilion wa matrilion hawafanywi kitu

Ova
Mzee wa Kino nimekuwa nikisema mara nyingi sana kwamba watu maskini wajiepushe sana na kuvunja sheria vinginevyo wataozea jela. Kama mtu kaamua kufanya uhalifu iwe ni mamilioni au mabilioni ya hela. Yaani iwe hela ndefu hadi vyombo vyote vya habari vinatangaza. Kuna watu kwenye kesi za uhujumu uchumi waapiga mabilioni halafu faini kama milioni kadhaa na kukaa mahabusu kwa muda.
 
Naomba kuongezewa ufahamu.

Mpokea Rushwa anawezaje kuhukumiwa peke yake Ikiwa ili apokee ni lazima mtoaji alidhie?

Ikiwa mtu mwenye kuhitaji kuhudumiwa atatakiwa kutoa Rushwa kwanza ili ahudumiwe na Ikiwa anajua haki na wajibu wake je ni sahihi kwa mpokea Rushwa kushitakiwa peke yake?

Ikiwa mtu anahitaji huduma na akatengeneza mazingira kwa watoa huduma wamuhudumie kinyume na utaratibu kwa kuwahonga je ni yupi atashitakiwa kati ya mtoa Rushwa na mpokea Rushwa?

Je, TAKUKURU wanawezaje kutokushitakiwa kama watoa Rushwa Ikiwa wataamua kumbaini mpokea Rushwa kwa njia ifuatayo?
Mtu anahitaji huduma lakini ili apewe huduma, watoa huduma wanamwambia atoe kiasi Cha pesa ili ahudumiwe. Sasa mtu anayetakiwa kuhudumiwa anaamua kuwasiliana na TAKUKURU Kisha TAKUKURU wao wanaamua kumpatia kiasi Cha pesa huyo mtu ili aipeleke anakotakiwa kuhudumiwa na baadaye TAKUKURU wanamshitaki mpokea Rushwa.

Je Ikiwa unahitaji kuhudumiwa lakini fursa hiyo ya kuhudumiwa unalazimishwa kuitolea hongo, ni mahali gani unatakiwa kutoa taarifa ili upate utetezi tofauti na TAKUKURU?

Je mtoa Rushwa na mpokea Rushwa hawawezi kushitakiwa kwa pamoja Ikiwa kati Yao mmoja ameshawishi na mwingine kwa akili zake timamu amekubali kushawishika?

Je undugu, mahusiano kama vile mapenzi au urafiki, Uchawi, na umasikini sio mizizi mikuu ya Rushwa?

Je, tunaweza kushindwa kukubali kwamba TAKUKURU hawataweza kuzuia Wala kupambana na Rushwa Ikiwa undugu, mahusiano kama vile mapenzi au urafiki, Uchawi na umasikini ndo mizizi mikuu ya Rushwa?

Nani anaweza kusema kama mimi kwamba "angalau tunaweza kupunguza kwa karibu 96% janga la Rushwa Ikiwa tutaamua kuyafanya makosa ya kupokea na kutoa Rushwa kuwa ni kosa Moja"?
 
Kwamba mtuhumiwa kaamriwa kugawana pasu kwa pasu na serikali hiyo rushwa aliyopewa sio?!
 
Back
Top Bottom