Mbeya kuna Daktari anaitwa Danny, serikali imeshindwa kumuwajibisha?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,466
Nimeenda Mbeya nikamkuta daktari anaitwa Danny! Anatamba hata kipindi hiki cha daktari Magufuli.

Anajiita Daktari Bingwa wa Mifupa wakati ana degree moja tu.

Alihamishwa toka Peramiho na kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mbeya.

Amesababisha vifo vingi kutokana na kufanya upasuaji asiosomea.

Mwezi wa tatu mwaka huu alisababisha kifo cha mwendesha bodaboda aliyekuwa akiitwa Festo aliyelazwa hospitali ya rufaa Mbeya baada ya kugongwa na gari ya mmiliki wa hotel moja iitwayo Kwetu Pazuri.

Haijulikani Danny alipata wapi taarifa za huyo mgonjwa kulazwa hospitali ya Rufaa Mbeya na kisha mgonjwa akahamishwa na akaishia kufanyiwa operation hospitali ya private ya K's Hospital; hii ni baada ya mgonjwa Festo kuambiwa na madaktari wa hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya kwamba hawatoweza kuokoa mguu wake.

Danny baada ya kwenda kumfanyia operation hapo K's akagundua hawezi okoa mguu huo akiwa anaendelea na operation. Ndugu waliombwa watoe pesa za damu iliyoendwa kufuatwa benki ya damu Mbeya.

Danny ana mambo mengi sana yanayoaibisha madaktari.

Amewaacha watu wengi wakiwa vilema, ikiwamo mke wa mfanyabiashara mashuhuri wa jijini Mbeya (Babito).


Amekuwa na mtandao wa kuhamisha wagonjwa (ukiwahusisha manesi wa wodi hadi mafundi wa mionzi) waliopata ajali toka hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya (ambayo si hospitali yake) na kwenda kuwafanyia operation kwenye hospitali binafsi iitwayo K's Hospital, kwa gharama kubwa huku akiwaacha wagonjwa na vilema vya kudumu au vifo.

Ana ushirikiano na laboratory technician wa NBTS Mbeya (ipo Meta hospitali) katika kuwauzia ndugu damu.

Watu gani wanamlinda Danny? Je, walewale wanaomlinda 'Dr. Nyagori' wa Morogoro.

Huyu Jamaa Bora tuwe naye Makini, Nshawahi kupata habari pia kuhusu huyu jamaa. Alifukuzwa Peramiho kwa Kashifa ya Rushwa kwani bila Rushwa alikuwa hafanyi kazi na akipewa rushwa hafanyi kazi ipaswavyo. Mganga Mkuu ahojiwe kwanini hadi sasa hachukuliwi hatua hadi ahamishwe mara Songea, Kesho Tabora na Sasa yupo Mbeya. Usishangae kesho Kusikia yupo Lindi au Nanyamba. Tusubiri

Hakika wew ni msema kweli mimi alishawahi nitibu na nilipo vizuri nilipata ajali nikavunjika mguu kwenye paja yani mfupa mkubwa ulivunjika mwaka 2013 ni akanitibu kwenye Hospital ya mkoa wa Ruvuma kipindi hicho alikuwa ameshafukuzwa peramiho kuhusu garama tulipeana mikononi sh 400,000 badada ya miezi mitatu nilienda cheki mguu umeunga nikaambiwa nitoe sh 80,000 ya kutolea chuma, chuma sikutolewa akanipiga chenga nikaja kusikia amehamiahiwa Tabora ikanibidi nitoe tena 100,000 ya kutowa chuma mpaka sasa natembea vizur ila sio sana kama zaman

>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Update toka Mbeya 1
Siku tatu zilizopita, Dr. Danny kamfanyia operation ya mifupa mmoja wa madaktari wasaidizi katika hospitali anayofanyia hizi operation zake zisizo na sifa. Taarifa zinasema baada ya kumfanyia operation daktari huyu msaidizi alipata complication ya Pulmonary Embolism, yaani bonge la damu kuziba njia za mapafu na kwamba hii ilisababisha mgonjwa kuwa mahututi na sasa amelazwa hospitali ya kanda ya Mbeya, wodi za Tiba, akiwa mahututi.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Update 2
Taarifa za ndani zinadai Danny kuhojiwa na UWT na kudai yeye si daktari bingwa wa Mifupa, bali wagonjwa wenyewe humfuata. Lakini bado swali linakuja, inakuwaje Danny afanye operation kubwa ambazo hana uzoefu nazo wala kusomea?

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Update 3 (Danny akiwa shuleni UDOM akifanya mafunzo Hospitali ya Mkoa wa Iringa


Wauza shamba kumpa rushwa daktari
Picha

FAMILIA ya Boniface Kimbe wa kijiji cha Maragosi wilayani Iringa imelazimika kuuza ekari mbili za shamba lao na kupata Sh 400,000 walizoombwa kama rushwa na Dk Daniel Masawe, ili amfanyie tiba ya upasuaji mwanafamilia mwenzao, Fadhili Kimbe.

Masawe ni daktari wa binadamu, mwajiriwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayefanya mafunzo ya vitendo kwa kufundisha na kufanya kazi kama daktari katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa.

Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Iringa imemkamata daktari huyo Mei 27 katika jaribio lake hilo la kushawishi na kuomba rushwa.

Akizungumza na wanahabari jana, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali alisema daktari huyo amefanya kosa hilo kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Kilimali alisema katika tukio hilo, uchunguzi wao ulibaini kwamba Mei 22, 2019; mtuhumiwa akiwa wodi namba tano akisikiliza wagonjwa wanaohitaji tiba ya upasuaji na kuwapangia siku ya upasuaji alishawishi na kuomba rushwa ya Sh 400,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa, Fadhili Kimbe.

“Mgonjwa huyo alikuwa akisubiri kuwekwa kwenye orodha ya wagonjwa wa kufanyiwa upasuaji Mei 27, 2019,” alisema.

Baada ya kuombwa rushwa hiyo, ndugu wa mgonjwa huyo; Egidi Kimbe, Imani Mleleu, Petro Kimbe, Yosefa Kimbe na Stella Kimbe waliokuwa hawana fedha hiyo walilazimika kukaa kikao na kukubaliana wakauze ekari mbili za shamba la mzee wao, Boniface Kimbe.

Kilimali alisema baada ya makubaliano hayo, shamba hilo liliuzwa Mei 26 na wakiwa katika mchakato wa kuziwasilisha fedha hizo kwa daktari huyo Mei 27, ndipo Takukuru ilipopata taarifa hiyo na kuingilia kati na kumkamata mtuhumiwa huyo.

“Mtuhumiwa aliomba kiasi hicho cha fedha akidai ili apate vifaa ambavyo havipo hospitalini kwa ajili ya kumfanyia tiba ya upasuaji mgonjwa huyo aliyepata ajali,”alisema.

Alisema uchunguzi wa Takukuru ulibaini vifaa vilivyoahidiwa kutafutwa na daktari huyo kwa ajili ya matibabu ya mgonjwa huyo vilikuwepo hospitalini hapo.

“Baada ya daktari huyo kukamatwa, uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa ya Iringa ulifanya taratibu za kumpata daktari mwingine kutoka mkoa jirani wa Dodoma aliyemfanyia tiba ya upasuaji mgonjwa huyo kwa malipo halali ya Sh 80,000,” alisema. Alisema mtuhumiwa huyo aliyetarajiwa kusomewa mashtaka yake hayo juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa na mwendesha mashtaka wa Takukuru, Elisante Fundisha, atapandishwa kizimbani hapo Juni 19 kesi hiyo namba 1/2019 itakapotajwa.
 
Huyu Jamaa Bora tuwe naye Makini, Nshawahi kupata habari pia kuhusu huyu jamaa. Alifukuzwa Peramiho kwa Kashifa ya Rushwa kwani bila Rushwa alikuwa hafanyi kazi na akipewa rushwa hafanyi kazi ipaswavyo. Mganga Mkuu ahojiwe kwanini hadi sasa hachukuliwi hatua hadi ahamishwe mara Songea, Kesho Tabora na Sasa yupo Mbeya. Usishangae kesho Kusikia yupo Lindi au Nanyamba. Tusubiri
 
mkuu nna wasiwsi na hizi doctor za kupewa pewa, yani ukishapewa udoctor. (sio wa kusomea),yani we unajiona kila mkate kwako ukija kwako ni chai lazima uliwe, mi nna wasiwasi na huj udoctor labda ndo walewale , ukienda kuanzisha mradi sehemu flan na u doctor unapataa, then unaenda kufanya upasuaji wa miguu badala ya kichwaa
 
Mimi namshukuru huyu ndugu,aliokoa maisha ya Dereva wangu. Rufaa walichemka nikampeleka pale K's akahudumiwa Na huyo Dany mpaka akapona. Dr huyo yuko vizuri and is very aggressive pamoja Na kwamba sina uwezo wa kudhibitisha taaluma yake ,but he is capable
 
Back
Top Bottom