View attachment 2719269
Taarifa iliyotolewa na Wakili wa Dr Slaa inasema kwamba , kabla ya kufikishwa Mahakamani leo Polisi walitaka kuchukua Sample ya Sauti ya Dkt Slaa (Haifahamiki walitaka kuifanyia nini) , ambapo Dkt Slaa amekataa jambo hilo kufanyika , kwa vile tayari polisi walishasema wanayo sauti yake ambayo wanadai waliinasa akipanga Uhaini wake , basi ni vema wakiitumia hiyo waliyo nayo ili kufanyia mambo yao .
Vinginevyo Wakili wake amedai kwamba wakitaka sauti ya Dkt Slaa basi wafungue kesi mahakamani kuiomba sauti hiyo , inatajwa kwamba jambo hili ndilo limekwamisha Watuhumiwa hao kufikishwa Mahakamani siku ya leo kutokana na mabishano makali kuhusu Sauti hiyo .
========
Bali wadau wengi wanaona Polisi hawakujipanga na kesi hii wameburuzwa tu na Watawala ili kuwalinda Waarabu wa DP WORLD , na ndio maana wanaokoteza
na kuunga unga sauti ya Dkt Slaa ili kutengeneza ushahidi wa magumashi .
Lakini ni vema tukafahamu kwamba , Hakuna popote pale kwenye dunia hii ambako Shetani aliwahi kumshinda Mungu