Miaka 22? Huyu so Binti mdogo kabisa? Ya kuua Mumeo yanatokea wapi? Bila shaka waliisha zoeshana kutwangana ndani ya nyumba! Leo Binti kamuwahi TU Mwenzie!Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja, Riziki Henry (22), mkazi wa Nditu wilaya ya Rungwe mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua mume wake, Ayub Aron (33) baada ya kumpiga na kitu kizito kichwani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema leo Jumatatu Aprili 4, 2022 kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya alfajiri baada ya marehemu kupigwa na kitu kizito kichwani baada ya kutokea ugomvi.
Matei amesema kuwa baada marehemu kujeruhiwa na kukimbiza katika hosptali ya Wilaya ya Makandana, wilaya ya Rungwe alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu kutokana na kumwagika damu nyingi.
Amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni baada ya kutokea ugomvi kutokana na marehemu kumtuhumu mkewe kuchelewa kurejea nyumbani na alipohojiwa ndipo ulipozuka ugomvi.
Amesema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na polisi huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa hosptali ya wilaya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kufuatia tukio hilo Kamanda Matei ameonya jamii kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi hususan kwa wanandoa ili kuepukana na migogoro isiyokuwa na tija inayosababisha vifo
Chanzo: Mwananchi
zile harakati za kuachana tu,nazo ni mtihani mkuu,hususani muwe na hazina yakutosha,ni balaa. mnaanza kuviziana nani anatangulia kukata kauli ya kumwacha mwenzie. Soln ni kuvumiliana pale inapostahili .ikishindikana ,ondoka kaa mbali nae!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Wapi HukoNgapi ngapi?
kweli mkuu.kumalizia maisha yako yote jela kwa Jambo unaloweza kuliepuka ni Ujinga.
Mali zinatafutwa.
Mimi wanawake wangu uwa nawaambia ukiona umenichoka wewe niambie tu tuachane.
Kuliko kufanyiana vituko.
Na kosa ambalo uwa sisamehi ni usaliti.simpigi ila kuachana tu.
we unadhani ni rahisi nyumba ambayo umejenga kwa kujitolea maisha yako yote kuibomoa na kuanza upya ?Mkishindwana muachane kwa wema
Viumbe dhaifu!Ingekuwa ni mume ameua mke ndio pangekuwa na kesi.
Wanawake wengi sana wanaua waume zao na kujitetea then kwishney.
Ole wao wanywao mvinyo mpaka usiku mwigi, vitu vizito vimechukua nafasi ya Covid!Naona wanawake mwaka huu mmedhamiria kweli kweli! Ni kutupiga tu wanaume na vitu vizito kichwani! Alianza kupigwa Nduguway, wakaja Mataga na Sukumagang!
Na sasa wanawake wengine wameamua kurithi! Ukizubaa tu, unakuta 'kitu kizito' kimesha dondoshwa kichwani. Sijui tukimbilie wapi! Yaani mnaupiga mwingi kweli kweli.
we unadhani ni rahisi nyumba ambayo umejenga kwa kujitolea maisha yako yote kuibomoa na kuanza upya ?
hivi unajua wanaume tunasota sana kwa ajili ya familia zetu halafu mtu analeta mambo ya ajabu ajabu .
kama umeoa/umeolewa omba Mungu majaribu hayo yasikukute
Sisi wala hatutafikia huko usihofuMmmmh
Ukiendelea kimasikhara ujiandae kisaikolojiaSisi wala hatutafikia huko usihofu