Mbeya: Ashikiliwa na polisi kwa mauaji ya Mumewe

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,614
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja, Riziki Henry (22), mkazi wa Nditu wilaya ya Rungwe mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua mume wake, Ayub Aron (33) baada ya kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema leo Jumatatu Aprili 4, 2022 kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya alfajiri baada ya marehemu kupigwa na kitu kizito kichwani baada ya kutokea ugomvi.

Matei amesema kuwa baada marehemu kujeruhiwa na kukimbiza katika hosptali ya Wilaya ya Makandana, wilaya ya Rungwe alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu kutokana na kumwagika damu nyingi.

Amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni baada ya kutokea ugomvi kutokana na marehemu kumtuhumu mkewe kuchelewa kurejea nyumbani na alipohojiwa ndipo ulipozuka ugomvi.

Amesema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na polisi huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa hosptali ya wilaya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Matei ameonya jamii kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi hususan kwa wanandoa ili kuepukana na migogoro isiyokuwa na tija inayosababisha vifo


Chanzo: Mwananchi
 
Ingekuwa ni mume ameua mke ndio pangekuwa na kesi.
Wanawake wengi sana wanaua waume zao na kujitetea then kwishney.
Na huwezi kuona wale wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu au haki za wanawake wanaongelea chochote.

Cha zaidi hapa watahamia upande wa mwanamke na kusema kuwa jamaa atakuwa alimkosea akavumilia au jamaa ndie alisababisha.

Tumefikia point kwa sasa jamii inambrand mwanamke kama innocent popote pale bila kung'amua dosari zake anapokosea. Na mwanaume anaonekana ana hatia hata pale ambapo hana uhusiano na hali inayotokea kuleta shida.
 
Hii ndio inaitwa kugawana majengo ya Serikali. Kuna kipande cha video niliona mwanamke anabutuliwa anang'olewa nywele kabisa nikajiuliza hivi huyu hawezi kujitetea kabisa? Hata jiwe karibu hakuna ampasue nalo usoni?

Kwenye kujitetea huishia pabaya ila poa tu.
 
Mmmh ., Ngoja nikomae na mzanzibari wangu mie ,
yeye ukimuudhi atajiliza humo ndani sio hawa wengine maswala ya kupiga na vitu kichwani
 
Back
Top Bottom