Mbege nzuri inatengenezwa vipi

1. Andaa ulezi - anika juani, twanga kwenya kinu, pepeta, osha, loweka maji yaelee mpaka juu, acha kwa siku tatu mpaka tano.
osha tena, suuza maji safi, tengeneza kitu kama kitanda cha majani ya mgomba chini ili mradi ufunike udongo fresh
mwaga hapo huo ulezi. funika vizuri na majani ya mgomba, yaani hewa isiweze kupita. kaa siku tatu hadi nne,
toa ule ulezi utakuta umeota vitu fulani vyeupe, uanike juani, wakati wa kuanika bonda bonda yale mabonge ili kila
punje iwe peke yake. Anika kwa muda wa siku kadhaa hadi ukauke. pepeta tena ili uchafu utoke. Hifazi kwenye gunia
zuri na safi kwa ajili ya kwenda kusaga hapa baada ya maandalizi ya ndizi kukamilika.

Ndizi - Tumia ndizi ng'ombe - siyo bukoba - chagua ndizi zilizo komaa vizuri, vundika, zikiiva vizuri toa maganda, zipike
chombo kigumu, kama sufuria kubwa au chungu kikubwa, tumia kuni ngumu na zilizokauka ili ndizi ziive vizuri
pika hadi ziwe na rangi ya damu ya mzee - ni vizuri usizigeuze geuze sana kwani zinaweza kuungulia chini
epua, ngoja zipoe, hifadhi kwenye chombo kisafi, uchagani wanaweka kwenye pipa maalum lililotengenezwa kwa
miti (sijui kama yapo tena). hakuna haja ya kufunika juu, ngoja muda wa siku tatu hadi saba inategemea na joto
la mahali ulipo. Utaona kama kuna puvu fulani linaanza kutoka kwa mbali, ujui ndizi tayari zimejisindika.

Utengenezaji wa mbege.
  • asubuhi na mapema jaza maji kwenye chombo kama pipa kisha weka huko zile ndizi ulizovundika, ile leya ya juu haifai hivyo unaweza ukawapa mifugo kama ipo. koroga, tulia
  • baada ya kusaga ule ulezi - tuliza tu unga pembeni (saga siku ya kutengeneza mbege)
  • ikifika saa kumi jioni chuja zile ndizi ili kutenganisha uchafu na ile juisi
  • pika uji wa ule ulezi, usiwe mwepesi wala mzito sana hakikisha unaiva vizuri siyo kuungulia lakini.
  • changanya huo uji kwenye ile juisi ya ndizi. koroga. weka msesewe ambao tayari utakuwa umeutwanga vizuri na kuutenganisha na yale makapi yake (ndicho kilevi cha mbege) kipimo kisiwe kikubwa. kama una watoto wanaopenda mbege watolee kabla ya kuweka msesewe.
  • ilale hadi kesho, mbege tayari.
ukitaka maelezo zaidi uliza.
 
1. Andaa ulezi - anika juani, twanga kwenya kinu, pepeta, osha, loweka maji yaelee mpaka juu, acha kwa siku tatu mpaka tano.
Osha tena, suuza maji safi, tengeneza kitu kama kitanda cha majani ya mgomba chini ili mradi ufunike udongo fresh
mwaga hapo huo ulezi. Funika vizuri na majani ya mgomba, yaani hewa isiweze kupita. Kaa siku tatu hadi nne,
toa ule ulezi utakuta umeota vitu fulani vyeupe, uanike juani, wakati wa kuanika bonda bonda yale mabonge ili kila
punje iwe peke yake. Anika kwa muda wa siku kadhaa hadi ukauke. Pepeta tena ili uchafu utoke. Hifazi kwenye gunia
zuri na safi kwa ajili ya kwenda kusaga hapa baada ya maandalizi ya ndizi kukamilika.

Ndizi - tumia ndizi ng'ombe - siyo bukoba - chagua ndizi zilizo komaa vizuri, vundika, zikiiva vizuri toa maganda, zipike
chombo kigumu, kama sufuria kubwa au chungu kikubwa, tumia kuni ngumu na zilizokauka ili ndizi ziive vizuri
pika hadi ziwe na rangi ya damu ya mzee - ni vizuri usizigeuze geuze sana kwani zinaweza kuungulia chini
epua, ngoja zipoe, hifadhi kwenye chombo kisafi, uchagani wanaweka kwenye pipa maalum lililotengenezwa kwa
miti (sijui kama yapo tena). Hakuna haja ya kufunika juu, ngoja muda wa siku tatu hadi saba inategemea na joto
la mahali ulipo. Utaona kama kuna puvu fulani linaanza kutoka kwa mbali, ujui ndizi tayari zimejisindika.

Utengenezaji wa mbege.
  • asubuhi na mapema jaza maji kwenye chombo kama pipa kisha weka huko zile ndizi ulizovundika, ile leya ya juu haifai hivyo unaweza ukawapa mifugo kama ipo. Koroga, tulia
  • baada ya kusaga ule ulezi - tuliza tu unga pembeni (saga siku ya kutengeneza mbege)
  • ikifika saa kumi jioni chuja zile ndizi ili kutenganisha uchafu na ile juisi
  • pika uji wa ule ulezi, usiwe mwepesi wala mzito sana hakikisha unaiva vizuri siyo kuungulia lakini.
  • changanya huo uji kwenye ile juisi ya ndizi. Koroga. Weka msesewe ambao tayari utakuwa umeutwanga vizuri na kuutenganisha na yale makapi yake (ndicho kilevi cha mbege) kipimo kisiwe kikubwa. Kama una watoto wanaopenda mbege watolee kabla ya kuweka msesewe.
  • ilale hadi kesho, mbege tayari.
ukitaka maelezo zaidi uliza.
hapo redi unapika hzo ndizi kwenye moto mkali,unaacha kwa siku tatu ,pia usisahau kuweka na molases na ngunana
 
hapo redi unapika hzo ndizi kwenye moto mkali,unaacha kwa siku tatu ,pia usisahau kuweka na molases na ngunana

smile hongera kwa kulijua hata hili,
kweli kuna wanaoweka hivi vitu,
sijui ni wa wapi, ila kule kwetu marangu
hatuweki hivi vitu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom