Mbege nzuri inatengenezwa vipi

Unanunua makunduu, unaroweka kwa siku kadhaa kwenye kihondi (3 days), kisha unayapika mpaka yaive kabisa!
na kubadilika rangi kuwa dark brown! Unaacha Makundu yapoe kisha nayo unayaweka kwenye kihondi chake mpaka kesho yake
(1 DAY),
Baada ya hapo unachukua mfuko wa mahindi maarufu kama SAFLET, Unauosha vizuri uhakikishe ni msafi kabisa na haujatoboka mahali, Kifuatacho unajaza yale makunduu kidogo kidogo kwenye ule mfuko wa saflet kisha unaanza kukamua! ili kutenganisha majimaji yanayotoka kwenye makunduu na ile hard material yaani makundu yenyewe(at this stage hatuhitaji ile hard material ila yale maji maji yake tu..yanayoitwa "olea") kwahiyo unaikamua kistadi mpaka iishe na unakuta tayari yameshakaa mkao wa kumixiwa na bidhaa ingine ili upate mbege!
Bidhaa hiyo ni zao la mbege liitwalo unga wa ulezi. Huu unaupika kama uji wa ulezi hivyo hivyo halafu ukishapoa unaenda kuumix kwenye ile "OLEA"..kumbuka ili mbege iwe kali na yenye ladha nzuri mixture yote ifanyike kwenye Kihondi! , ukishamix unaiache ilale usiku kucha kabla ya kuanza kutumiwa, ..Ile waste products inayopatikana baada ya kukamua makunduu usiitupe ni chakula nzuri sana ya Nguruwe.

NB:
1)Makunduu - ni ndizi aina mbalimbali zilizowiva amabazo hutumika kupikia pombe.
zinapatikana sana masoko ya moshi sijui huko dar!
2)Kihondi - Ni chombo maalum cha kuwekea pombe kimetengenezwa na gogo kubwa la mti na kinaweza kuweka litre 80 na kuendelea za pombe.
3)Olea - Ni Juice inayotoka kwenye makunduu kwenye mchakato wa kutengeneza pombe..hii haileweshi!
Utaalamu huu niliuona kwa bibi yangu(R.i.p) kule old Moshi sango karibu na mjororoni!

Mkuu Mchaka Mchakani,
Aisee wewe kiboko haya maujuzi sio mchezo! Nimejifunza maujuzi, hivi unaweza kuisafirisha kuipeleka mikoa mbali mbali bila kualibika?
 
Mkuu Mchaka Mchakani,
Aisee wewe kiboko haya maujuzi sio mchezo! Nimejifunza maujuzi, hivi unaweza kuisafirisha kuipeleka mikoa mbali mbali bila kualibika?
Hapana ikitingishwa sana umbali mrefu inaharibika..ila huwa wanasafirisha ..kutoka Kibosho mpaka Arusha kwa kutumia Toyota Stout!
 
Pasaka ntakununulia usijali.
Hehehee labda ukinywa kata/chubuka kadhaa, tena zile kubwa.
Hiyo ofa uliyonipa siiachii! Nitakukubusha siku moja kabla ya pasaka!!
December nilikunywa zaidi ya chubuku but asubuhi yake nikawa pouwa kabisa,.....nataka kupata experience kwa wengine kama huwa zinawachosha!! Wewe unaweza maliza kitochi kizima? au kisichana(sijui kama hiki unakifahamu)
 
Basi andaa nauli ya watu wawili kwenda Moshi na kirudi, malazi na chakula utapata.

Ngoja niandae nikiwa tayari takustua Lizzy! Nianze kazi mie nataka niboreshe zaidi niwe nafunga kama juice za Azzam.
 
Hiyo ofa uliyonipa siiachii! Nitakukubusha siku moja kabla ya pasaka!!
December nilikunywa zaidi ya chubuku but asubuhi yake nikawa pouwa kabisa,.....nataka kupata experience kwa wengine kama huwa zinawachosha!! Wewe unaweza maliza kitochi kizima? au kisichana(sijui kama hiki unakifahamu)
Nikumbushe. . . I'll deliver.

Aisee mimi kikombe kimoja tu cha chai au ile chibuku ndogo nikijitahidi sana.
 
Rej hii sio fresh kabisa. Ndio nini kunifanya nitamani kulamba screen ya hiki kitochi changu?

hahahah mkwe acha kuchafua screen nakuandali visichana viwili lol!!! ile fresh haina msesewi inaitwa kifue nzuri balaa
 
Nikumbushe. . . I'll deliver.

Aisee mimi kikombe kimoja tu cha chai au ile chibuku ndogo nikijitahidi sana.
Hamna cha kudeliver hapa...nakufuata huko huko tunaria wote!! raha ya mbege ni kuinywa pamoja!!
 
Back
Top Bottom