wakimataifa.
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 1,625
- 558
akina mbatia hamna asili ya uongozi nyumba za osterbay zilipitishwa kihalali
Mheshimiwa Mbatia unaheshimiwa sana tafadhali usijishushe hadhi yako kwa matamko ambayo hayatarajiwi toka kwako.
JPM hakuwahi kuwa na uwezo wa kuuza nyumba au mali yoyote ile ya serikali. Kwenye kuuzwa nyumba za serikali rightly or wrongly ilikuwa uamuzi wa baraza zima la mawaziri chini ya rais. Na hili lilifikiwa baada ya mjadala mrefu kuhusu nyumba hizo. Hivyo basi kumlaumu JPM eti kwa vile ametekeleza wajibu wake kisheria ni kutomtendea haki kabisa.
Kama unatafuta wa kumlaumu mbona Mzee Ben humchokozi? Tatizo la Escrow lilikuwa la kisheria mno na kwa mtu kama wewe unalifahamu vizuri sana.
Hisia zangu, rightly or wrongly ni kuwa huyu JPM anawanyima raha jinsi anavyokubalika na umma na kwa kiasi fulani mnahisi mkiendelea kunyamaza kimya basi mtakuwa hamna ajenda na hili ndiyo maana mara mnafunga midomo yenu, mara naibu spika hamumtaki[taratibu za kumng'oa mnazijua lakini hamfuati hizo].
Ushauri wangu ni kwamba kwa sasa tulieni. JPM yuko honeymoon. wananchi wengi wanamkubali na wanaamini kuwa muelekeo wa serikali yake ni mzuri kwao na honeymoon ikiisha mtapata tu mada za kuzungumzia.
Wakina martin lutter king walipigania Uhuru wao wazungu pamoja na baadhi ya waafrica waliokuwa wananufaika waliwadharau hata Obama alipokuwa anaomba urais kwama mwafrika wakwanza alidharauliwaTatizo ni kwamba ndugu zangu hawa wanadhani wananchi ni mbumbumbu na hawajui kinacho endelea nchini.
Ukweli ni kwamba wananchi wa kawaida wanauelewa mkubwa kuliko wanavyofikiria. Hii inanikumbusha kuhusu mbunge mmoja wa upinzani hivi karibuni aliwekwa kapeti na wananchi wake wakitaka kujua kwa nini ameamua kutohudhuria vikao vya bunge kuwawakilisha kama mkataba wao na yeye. Jamaa alijibu kuwa anafuata maelekezo ya viongozi wake na wakamwambia jee huko mjengoni ulipelekwa na viongozi wake au ni sisi ndiyo tuliokupa kazi hiyo????
Wengi waliosikia kauli hii hawakuipa kipa umbele lakini kwa maoni yangu hiyo ni ishara tosha kuelewea kuwa wananchi hawa tunaowaita wa kawaida wanauelewa mkubwa sana kuliko tunavyofikiria. zile enzi za kuwadanganya zimepita.
Lowassa kaingiaje kwenye uzi huu ?!.JPM sio malaika kama tulivyo binsdamu wengine ila Kazi anayofanya nii nzuri sana. Huyo Lowassa wenu mliyetaka awe Rais ana usafi gani? Acheni kudanganya watu.
JPM sio malaika kama tulivyo binsdamu wengine ila Kazi anayofanya nii nzuri sana. Huyo Lowassa wenu mliyetaka awe Rais ana usafi gani? Acheni kudanganya watu.
Lowasa hajakanusha hivyo ukikaa kimya maana yake umekubali. Kikwete aliwaambia watanzani kule mwanza tarehe 24 oktoba kuhusu Richmond Lowasa hajajibu. Kama unakubali richmond ya kikwete basi ukubali uuzaji nyumba si wa magufuli maana magufuri kicheo alikua waziri mdogo kwa sumaye. Tafuteni namna nyingine ya kumkashfu Magufuri. Kosa kubwa kina Mbatia limewakumba ni kuwa silaha zote ambazo wangezitumia kumshambulia magufuri ni batili maana makombora yameelekea kwao. Mbatia asingekua ktk muungano wa ukawa angetumia makombora ya cdm kuwapiga ccm na cdm lakini kitendo cha kuwepo kundini kupokea fataki ambaxo zingewasaidia amekosa credibility ya kumshambulia maguRichmond ni ya kikwete
Ungetuambia haya maneno mwaka 2008 ama mwaka jana kabla ya july wengi wetu tungekuelewa lakini kwasasa unajifurahisha na kujidanganya. Ulikaa kimya kina Mbowe walivyotuaminisha Lowasa ni fisadi. Ulimshabikia Slaa aliposema Lowasa ni fisadi lini ulipata ukweli kuwa Lowasa hakua fisadi? Kosa kubwa alulolifanya Lowasa lilikua kukubali kujitoa mhanga kutetea rafiki zake na hilo yeye mwenyewe analijutia hivyo kwangu si shujaa ninachokijua mimi alikaa kimya kwa makusudi maana alitarajia kupata nafasi kubwa ktk nchi ni ubinafsi na uchu wa madaraka aliuweka mbele kuliko maslahi ya nchi. Hili kosa hatasamehewa kamwe. Kama Lowasa angekua mzalendo alitakiwa kuitisha waandishi wa habari na kuueleza umma wa watanzania nini kilitokea kiwaziwazi na baadae ajiuzuru hapo angeonyesha kuwa yupo innocent lakini kwakua hakufanya hivyo anabaki tu kuwa moja wa lile genge la wezi na kikwete akiwemo na ndilo litamfuata huko baada ya mkutano mkuu wa kumkabidhi chief wa kisukuma mgolore wake.Mmemtumia sana Lowassa kuficha udhaifu na ufisadi wa viongozi wengine katika chama na serikali. Kwa kuwa Lowassa mwenyewe ni mkimya mmempatia kila jina baya wakati mafisadi halisi wa mali za nchi na vyeo vyao wanalindwa.Hakuna hatua sahihi zilizochukuliwa kwa mafisadi halisi wa nchi hii.
Hatukubali tena kudanganywa kuwa Lowassa ni fisadi, ila ni shujaa mnyenyekevu anayeweza kuacha cheo na madaraka pale anapoona kuna unafiki mwingi.
Hata mimi nimejiuliza swali hili, huyu Mbatia huyu ninayemfahamu mimi toka mwaka 47? au kuna mwingine?Mbatiaaaaa, nae ni msafi kweli!!!! kweli Nyani..............
Sioni kama kuna ubaya wowote ule kwani nyumba hizo wamenunua watanzania[wafanyakazi] na zingeuzwa soko huria karibu zote zingemilikiwa na waarabu/wahindi. Pia pesa zilizopatakana zimeweza kujenga na zinaendelea kujenga nyumba mpya za seerikali kutokana na mtaji huo [hebu nenda pale TBA utaona]. Mimi nionavyo ni kuwa wivu na ubinafsi ndiyo tatizo hasa wale wa kubwa ambao aidha walikuwa wanaishi kwenye nyumba zao wakati wa mchakato huo au wale ambao wangependa wanufaike bila kuwa watumishi wa umma.Kwahiyo yy alitimiza wajibu wa kitu kibaya
Naomba kwanza amuulize maswala ya nyumba Sumaye....RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.
James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi amemtaka Rais Magufuli kujisafisha kutokana na kashfa ya kuhusika katika kuuza nyumba za serikali kabala ya kusafisha watuhumiwa wengine wa ufisadi.
“Rais Magufuli anapaswa kujisafisha mwenyewe kwanza kutokana na kashfa inayomuhusu ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mbatia amesema “tumeona ni kwa namna gani Rais Magufuli anahangaika kupambana na ufisadi au uhujumu uchumi kwa kutumia nguvu kubwa kwa vidagaa na kuacha mapapa kama wale wa Tegeta ESCROW, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere ‘Terminal III’, makontena bandarini, IPTL, Richmond na Mradi wa Umeme wa Kinyerezi.
“Hivyo rais anapaswa kujisafisha kwanza kwa kuwa na yeye anatajwa kuhusika katika kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.
Mbatia amesema, katika kufanikisha hayo Rais Magufuli anapaswa kuacha kuongoza nchi kwa matamko badala yake aongoze kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za Nchi.
“Demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa. Kutokana na hali hiyo, nchi sasa iko kwenye hali mbaya katika; bunge kuingiliwa, hali ya maisha ya Watanzania kiusalama iko njia panda hususani Zanzibar.
Pia, kuna ukiukwa kwa haki za wananchi kutafuta na kusambaza taarifa na matumizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani.
Aidha, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imebaini athari za kiuchumi zitokanazo na uamuzi wa viongozi kufuatia matamko mbalimbali ya serikali.
Miongoni mwa athari hizo ni kupungua kwa mzigo bandarini ikiwa ni sambamba na watumiaji wa bandari wakihamia nchi jirani.
Chanzo: Mwanahalisi
RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.

Aliishazungumzwa sana, ila yuko kwenye kundi la untouchables.Mkuu Pasco!! ingawa haujagusia angalau moja ya hizo kesi 8, nafikiri na hii hapa chini ni moja wapo, isipokuwepo basi hakutakuwa na kesi bali maigizo.
Zitto amuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni
Zitto amuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni
- May 14, 2013
Ndugai amekuwa mtetezi wa ufisadi bungeni. Ni baada ya kamanda Zitto Kabwe kumuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni. Baada ya Zito kutoa hoja ya kutoa shilingi ya mshahara wa Magufuli, Ndugai akakurupuka kufunika hoja, eti kisa Zito ni Mwenyekit wa PAC. Safari bado ngumu.
"Mwaka 2011 tulipohoji kifungu chenye Fedha tshs 252bn kwenye Wizara ya Ujenzi, Naibu Waziri Harrison Mwakyembe alijibu "hizi Ni Fedha za miradi maalumu ya barabara ambapo tukipata misaada ya wafadhili hizi ndio michango yetu Kwa miradi". Bunge likapitisha. Hazina ikatoa pesa zote kwenda Wizara ya Ujenzi.
Mwaka huu tumehoji, hizi Fedha zilitumika namna gani? Waziri John Magufuli akasema "tulilipa Madeni".
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema kwenye taarifa yake "ilitengenezwa miradi hewa ya barabara yenye namba ya mradi hewa. Pia hakuna uthibitisho kuwa Madeni yalilipwa kwani hakuna nyaraka za kuonyesha malipo". Tumehoji kutaka majibu, tumepigwa chenga.
Kweli? Tshs 252 bilioni hazina maelezo? Tutahakikisha Uwajibikaji katika hili"
Agosti 24, 2013 - Mwananchi
Tuhuma nzito: Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012.
Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.
Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa kiasi cha Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo, alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema).
Alisema katika majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Mwakyembe wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha.
Alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.
Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara, Zitto alisema akikariri maneno ya Dk Magufuli wakati anawasilisha bajeti.
Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili, haya yalikuwa maneno ya Dk Mwakyembe wakati akifanya majumuisho.
Hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund, alimkariri Lukuvi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Zitto alisema CAG alihoji mwaka huu kuhusu matumizi ya fedha hizo na alitoa taarifa akidai kuwa fedha hizo zilikuwa miradi hewa na kasma kivuli.
Zitto alisema kuwa Dk Magufuli na Katibu Mkuu wake walipohojiwa walidai kutumia fedha hizo kulipa madeni.
Kwa nini mlidanganya Bunge? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za madeni. Kwa nini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa? Zitto alimhoji Balozi Mrango.
Katika majibu yake, Balozi Mrango alisema kwa nia njema, fedha hizo zilitumika kuwalipa makandarasi waliokuwa wamechachamaa, huku baadhi yao wakisisitiza kusitisha kuendelea na miradi. Hivyo wakalazimika kuomba fedha kwa njia hiyo ili miradi kuendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Zitto hakuridhishwa na majibu hayo akisema hapakuwa na haja ya kutumia fedha hizo kuwalipa makandarasi wakati kulikuwa na kasma yao ya awali. Alisema kama kulikuwa na haja hiyo, wizara isingeita mradi rasmi.
Jambo hili siyo sahihi hata kidogo kulidanganya Bunge na hadi sasa wewe na waziri wako hamuonyeshi kukubali kosa hili, hata Waziri Lukuvi naye alisisitiza bungeni kwamba fedha hizo zinaombwa ili kutekeleza mradi maalumu lakini sasa imebainika sivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge tutawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe nao wajieleze kwa kulidanganya, alisema Zitto.
Pia kamati hiyo imeitaka wizara hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi ya Sh100 bilioni zilizotumika kinyume na maombi yaliyowasilishwa kwenye Bajeti ya mwaka huo wa fedha.
CAG ameshauri madeni yote ambayo Wizara ya Ujenzi inadaiwa yaorodheshwe ili yawe wazi kuepuka migongano katika matumizi ya fedha.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Lukuvi alisema haelewi chochote na kusisitiza kuwa akipata taarifa rasmi za Kamati ya PAC, atatoa ufafanuzi.
Halmashauri zinavyotafuna mabilioni
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAACc), imeeleza namna mamilioni ya fedha za Serikali zinavyoibwa kutoka Hazina kupitia halmashauri za wilaya huku Ilala ikitajwa kuongoza kwa ufisadi huo.
Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohammed aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Hazina imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri zikiwa zimezidi na kwamba kiasi kinachozidi hakirudishwi badala yake huliwa.
Alisema kamati hiyo imefanya uchunguzi kwenye halmashauri 43 na kubaini kwamba mtindo huo ndiyo unaotumika kuiba fedha za Serikali.
Mwaka 2011/12 kiasi cha Sh1.5 bilioni zilipelekwa zikiwa zimezidi kwenye halmashauri hizo lakini hazikurudishwa Hazina kama inavyoonyesha kwenye ripoti ya CAG.
Alisema kati ya kiasi hicho, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipewa ziada ya Sh213 milioni ikifuatiwa na Geita iliyopewa Sh129 milioni.
Fedha hizo za mishahara zilipelekwa kwenye halmashauri hizo na Hazina kimakosa zikiwa zimezidi lakini watendaji wa hawakuzirudisha kama wanavyotakiwa kisheria badala yake zikayeyuka, alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa uchunguzi huo pia ulibaini kwamba katika halmashauri hizo 43 kiasi cha Sh693 milioni hulipwa mishahara hewa ambayo wafanyakazi wake walishakufa na wengine kustaafu.
Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ililipa mishahara hewa yenye thamani ya Sh79.4 milioni ikifuatiwa na Ukerewe iliyolipa Sh57.5 milioni.
Kwa upande wa fedha za miradi ya maendeleo, mwaka 2011/12, Hazina ilipeleka katika Halmashauri ya Mbarali, Mbeya Sh724 milioni kwa ajili ya Mradi wa Maendeleo ya Elimu Sekondari wakati mradi huo ulikuwa ukihitaji Sh70 milioni tu.
Kiasi cha Sh654 milioni zilipelekwa kimakosa na Hazina lakini badala ya kurudishwa zilitumiwa katika mazingira ya kutatanisha, alisema.
Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilipelekewa ziada ya Sh500 milioni na Mvomero ilipewa Sh85 milioni. Kuna mtandao mkubwa wa Hazina na halmashauri ambao ukiachwa utaendelea kupoteza fedha nyingi za walipakodi, alisema.
pSoma mkasa wa kifisadi na kitapeli uliowahi kufanywa na mgombea wa CCM bwana Magufuli kama unavyosimuliwa na mwandishi wa Raia Mwema:
- See more at: Raia Mwema - Lowassa vs Magufuli:Yupi ni â&[HASHTAG]#8364[/HASHTAG];&[HASHTAG]#732[/HASHTAG];shetani nafuuâ&[HASHTAG]#8364[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8482[/HASHTAG]; tumpe kura?
kweli huyu ni mama Tanzania katika UBORA WAKE...... mtu anayetoa haya maoni ni mmoja kati ya genge la watu wanaowakumbatia lOWASSA na SUMAI...... kama JPM si Msafi!! status za hao waandamizi wawili wa CHADEMA zitakuwaje? kwani hao wote walikuwa ni MABOSS wakubwa wa JPM....RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.
James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi amemtaka Rais Magufuli kujisafisha kutokana na kashfa ya kuhusika katika kuuza nyumba za serikali kabala ya kusafisha watuhumiwa wengine wa ufisadi.
“Rais Magufuli anapaswa kujisafisha mwenyewe kwanza kutokana na kashfa inayomuhusu ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mbatia amesema “tumeona ni kwa namna gani Rais Magufuli anahangaika kupambana na ufisadi au uhujumu uchumi kwa kutumia nguvu kubwa kwa vidagaa na kuacha mapapa kama wale wa Tegeta ESCROW, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere ‘Terminal III’, makontena bandarini, IPTL, Richmond na Mradi wa Umeme wa Kinyerezi.
“Hivyo rais anapaswa kujisafisha kwanza kwa kuwa na yeye anatajwa kuhusika katika kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.
Mbatia amesema, katika kufanikisha hayo Rais Magufuli anapaswa kuacha kuongoza nchi kwa matamko badala yake aongoze kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za Nchi.
“Demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa. Kutokana na hali hiyo, nchi sasa iko kwenye hali mbaya katika; bunge kuingiliwa, hali ya maisha ya Watanzania kiusalama iko njia panda hususani Zanzibar.
Pia, kuna ukiukwa kwa haki za wananchi kutafuta na kusambaza taarifa na matumizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani.
Aidha, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imebaini athari za kiuchumi zitokanazo na uamuzi wa viongozi kufuatia matamko mbalimbali ya serikali.
Miongoni mwa athari hizo ni kupungua kwa mzigo bandarini ikiwa ni sambamba na watumiaji wa bandari wakihamia nchi jirani.
Chanzo: Mwanahalisi
Hiyo meli si ndio imekabidhiwa geshi,,,,eti isizungumzwe tena?JPM anahusika na kashfa nyingi tu, ikiwemo Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kinyume na Mamlaka ya Bunge na kukandamiza Demokrasia ya Vyama vingi na Uhuru wa kupata Habari, kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.
Hiyo meli imeishakabidhiwa jeshini , tafadhari vijana msiendelee kujadili .JPM anahusika na kashfa nyingi tu, ikiwemo Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kinyume na Mamlaka ya Bunge na kukandamiza Demokrasia ya Vyama vingi na Uhuru wa kupata Habari, kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.