Mbatia: Rais Magufuli si msafi

Mbatia: Rais Magufuli si msafi

Mheshimiwa Mbatia unaheshimiwa sana tafadhali usijishushe hadhi yako kwa matamko ambayo hayatarajiwi toka kwako.

JPM hakuwahi kuwa na uwezo wa kuuza nyumba au mali yoyote ile ya serikali. Kwenye kuuzwa nyumba za serikali rightly or wrongly ilikuwa uamuzi wa baraza zima la mawaziri chini ya rais. Na hili lilifikiwa baada ya mjadala mrefu kuhusu nyumba hizo. Hivyo basi kumlaumu JPM eti kwa vile ametekeleza wajibu wake kisheria ni kutomtendea haki kabisa.

Kama unatafuta wa kumlaumu mbona Mzee Ben humchokozi? Tatizo la Escrow lilikuwa la kisheria mno na kwa mtu kama wewe unalifahamu vizuri sana.

Hisia zangu, rightly or wrongly ni kuwa huyu JPM anawanyima raha jinsi anavyokubalika na umma na kwa kiasi fulani mnahisi mkiendelea kunyamaza kimya basi mtakuwa hamna ajenda na hili ndiyo maana mara mnafunga midomo yenu, mara naibu spika hamumtaki[taratibu za kumng'oa mnazijua lakini hamfuati hizo].

Ushauri wangu ni kwamba kwa sasa tulieni. JPM yuko honeymoon. wananchi wengi wanamkubali na wanaamini kuwa muelekeo wa serikali yake ni mzuri kwao na honeymoon ikiisha mtapata tu mada za kuzungumzia.
Mtu anayekubalika na jamii anaweza kuogopa mikutano ya kisiasa ?
 
Back
Top Bottom