Mbatia: Rais Magufuli si msafi

Mbatia: Rais Magufuli si msafi

RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi amemtaka Rais Magufuli kujisafisha kutokana na kashfa ya kuhusika katika kuuza nyumba za serikali kabala ya kusafisha watuhumiwa wengine wa ufisadi.

“Rais Magufuli anapaswa kujisafisha mwenyewe kwanza kutokana na kashfa inayomuhusu ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mbatia amesema “tumeona ni kwa namna gani Rais Magufuli anahangaika kupambana na ufisadi au uhujumu uchumi kwa kutumia nguvu kubwa kwa vidagaa na kuacha mapapa kama wale wa Tegeta ESCROW, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere ‘Terminal III’, makontena bandarini, IPTL, Richmond na Mradi wa Umeme wa Kinyerezi.

“Hivyo rais anapaswa kujisafisha kwanza kwa kuwa na yeye anatajwa kuhusika katika kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Mbatia amesema, katika kufanikisha hayo Rais Magufuli anapaswa kuacha kuongoza nchi kwa matamko badala yake aongoze kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za Nchi.

“Demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa. Kutokana na hali hiyo, nchi sasa iko kwenye hali mbaya katika; bunge kuingiliwa, hali ya maisha ya Watanzania kiusalama iko njia panda hususani Zanzibar.

Pia, kuna ukiukwa kwa haki za wananchi kutafuta na kusambaza taarifa na matumizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani.

Aidha, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imebaini athari za kiuchumi zitokanazo na uamuzi wa viongozi kufuatia matamko mbalimbali ya serikali.

Miongoni mwa athari hizo ni kupungua kwa mzigo bandarini ikiwa ni sambamba na watumiaji wa bandari wakihamia nchi jirani.

Chanzo:
Mwanahalisi
Mbatia aombe kazi ya uchungaji kkkt. anajua kuimbisha nyimbo za kanisani hadi anaimbisha kwenye mikuno ya siasa nyimbo za kanisani. uongozi wa siasa umemshinda hadi chama chake nccr kimekufa. amebaki kazi kujipendekeza chadema na kwa sasa yeye ni nyumbu mfuata malisho. jpm ndio champion.. hayo mapapa anayodai mbona mengi yashatumbuliwa. mbatia anafikiri watu hawayajui mafisadi papa. inaelekea jinsi jpm anavyotumbua majipu ndio mbatia et al wanashikwa na kiwewe.
 
Kiwewe kipi ? Zipo wapi zile bilion 252 zilizopotea wizara ya ujenzi Kwa kuwalipa makandarasi Hewa? Kivuko cha Azam kipya kilinunuliwa bilion 5 tu, lakini kivuko chakavu cha Dar Bagamoyo kikanunuliwa Kwa bilion 8, huku nyumba za serikali baba yako alijiuzia kibao mpaka akagawa zingine bure , unatakiwa Mbatia akae kimya Kwa hili ?
 
Siasa inamaana nyingi kutokana na muktadha Fulani, hapa naweza sema siasa ni kuongea. Na rafiki yangu kaonelea kukaa kimya atasahaulika katika uwanja wa siasa hivyo ni bora aongee kitu.
Tusimlaum mbatia naye kajarib kuongea. Mpigien makofi tafadhar
 
Mwana alisi tena! Wakati mwingine Mh.Mbatia upenda sana cheap publicity na kukosa busara - masuala ya kuuza nyumbaza Serikali na mashirika ya UMMA kwa nini amuulizi Waziri mkuu mstaafu Mh.Sumaye ambaye wako pamoja UKAWA - Sumaye aliwahi kufafanua kiundani nini kilijili katika uuzaji nyumba - alisema Dk.Nagufuli alitejeleza yaliyo amuliwa na Baraza la mawaziri na Rais - kwa nini Mbatia na kundi lake wakiishiwa sera wanakimbilia masuala ya nyumba za Serikali as if hakuna kitu kingine cha kujadili.
 
RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi amemtaka Rais Magufuli kujisafisha kutokana na kashfa ya kuhusika katika kuuza nyumba za serikali kabala ya kusafisha watuhumiwa wengine wa ufisadi.

“Rais Magufuli anapaswa kujisafisha mwenyewe kwanza kutokana na kashfa inayomuhusu ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mbatia amesema “tumeona ni kwa namna gani Rais Magufuli anahangaika kupambana na ufisadi au uhujumu uchumi kwa kutumia nguvu kubwa kwa vidagaa na kuacha mapapa kama wale wa Tegeta ESCROW, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere ‘Terminal III’, makontena bandarini, IPTL, Richmond na Mradi wa Umeme wa Kinyerezi.

“Hivyo rais anapaswa kujisafisha kwanza kwa kuwa na yeye anatajwa kuhusika katika kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Mbatia amesema, katika kufanikisha hayo Rais Magufuli anapaswa kuacha kuongoza nchi kwa matamko badala yake aongoze kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za Nchi.

“Demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa. Kutokana na hali hiyo, nchi sasa iko kwenye hali mbaya katika; bunge kuingiliwa, hali ya maisha ya Watanzania kiusalama iko njia panda hususani Zanzibar.

Pia, kuna ukiukwa kwa haki za wananchi kutafuta na kusambaza taarifa na matumizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani.

Aidha, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imebaini athari za kiuchumi zitokanazo na uamuzi wa viongozi kufuatia matamko mbalimbali ya serikali.

Miongoni mwa athari hizo ni kupungua kwa mzigo bandarini ikiwa ni sambamba na watumiaji wa bandari wakihamia nchi jirani.

Chanzo:
Mwanahalisi
Kwanini yeye msafi?!
 
Chadema mpaka Leo hawajapeleka gharama walizotumia kwenye uchaguzi mkuu
 
uuzwaji hovyo Wa Nyumba za serikali!!!! hoja ya kijinga kabisaaaa!!!ebu mh mbatia muulize mh sumaye akupe Maelezo vizuri!!yawezekana wakati mchakato unaendelea wewe ulikuwa darasani ukibukuwa!!!kama ziliuzwa kiholela basi wakulaumu ni mh sumaye kwa kushindwa kusimamia vizuri mawaziri na Mali za serikali/umma!!vinginevo Mzee ikujiabisha unapoleta hoja kama hii wakati wakukupa jibu umekaa naye mezani na anagombea uenyekiti huko chadema
 
MAGUFULI nae aache mzaha, kutumbua Magesa Mlongo kisa CV nakuacha RADA/Chenge hewani, Kitwanga hewani, IPTL, Richmond, Meremeta, EPA, Bomba la Mtwara, hata Kigamboni (Daraja na mradi wa nyumba) ni Jipu BoT kila dili wamo, Uuzwaji wa Nyumba na mali za serikali kiholela, pia Magufuli asidhani sisi wa Tz ni wajinga eti Wizara yake ya Ujenzi haina MAJIPU wakati barabara za awamu yake zote ni mahandaki ya Alshabab hakuna michoro mipya ya barabara ktk Majiji.

Kwanza nina wasiwasi sana na Kampuni ya NYANZA Road kama si yake!! Kazi zake ni za hovyo ila kwa kupewa tenda haijambo!!!
 
uuzwaji hovyo Wa Nyumba za serikali!!!! hoja ya kijinga kabisaaaa!!!ebu mh mbatia muulize mh sumaye akupe Maelezo vizuri!!yawezekana wakati mchakato unaendelea wewe ulikuwa darasani ukibukuwa!!!kama ziliuzwa kiholela basi wakulaumu ni mh sumaye kwa kushindwa kusimamia vizuri mawaziri na Mali za serikali/umma!!vinginevo Mzee ikujiabisha unapoleta hoja kama hii wakati wakukupa jibu umekaa naye mezani na anagombea uenyekiti huko chadema
Acha kusapoti maovu kwa hoja dhaifu eti SUMAYE!! SUMAYE ni nani hapa Tz? Tz kwanza SUMAYE au MAGUFULI baadae awe SUMAYE au LOWASSA au JK au CHENGE YOYOTE alie tupiga hela awajibike.
 
Ndani ya UKAWA msafi nani???? Mbowe, Lowasa, Sumaye, Mbatia, nani ajitokezeeee, Na wewe malisa utatumika baadae utatemwa kama Big G
 
Mheshimiwa Mbatia unaheshimiwa sana tafadhali usijishushe hadhi yako kwa matamko ambayo hayatarajiwi toka kwako.

JPM hakuwahi kuwa na uwezo wa kuuza nyumba au mali yoyote ile ya serikali. Kwenye kuuzwa nyumba za serikali rightly or wrongly ilikuwa uamuzi wa baraza zima la mawaziri chini ya rais. Na hili lilifikiwa baada ya mjadala mrefu kuhusu nyumba hizo. Hivyo basi kumlaumu JPM eti kwa vile ametekeleza wajibu wake kisheria ni kutomtendea haki kabisa.

Kama unatafuta wa kumlaumu mbona Mzee Ben humchokozi? Tatizo la Escrow lilikuwa la kisheria mno na kwa mtu kama wewe unalifahamu vizuri sana.

Hisia zangu, rightly or wrongly ni kuwa huyu JPM anawanyima raha jinsi anavyokubalika na umma na kwa kiasi fulani mnahisi mkiendelea kunyamaza kimya basi mtakuwa hamna ajenda na hili ndiyo maana mara mnafunga midomo yenu, mara naibu spika hamumtaki[taratibu za kumng'oa mnazijua lakini hamfuati hizo].

Ushauri wangu ni kwamba kwa sasa tulieni. JPM yuko honeymoon. wananchi wengi wanamkubali na wanaamini kuwa muelekeo wa serikali yake ni mzuri kwao na honeymoon ikiisha mtapata tu mada za kuzungumzia.
Anatafuta kiongozi msafi? kweli hoja naona zimefika mwisho......
 
Back
Top Bottom