MBATIA kufukuzwa Ubunge?

MBATIA kufukuzwa Ubunge?

Mtaala upo nchi haiwezi kukosa mtaala. Tunapoongelea mtaala wa 2005 ni mabadiliko ya mtaala yaliyofanywa mwaka huo. Mabadiliko hayo yapo na yanadhihirika kwenye Sylabus mpya ya 2005. Kinachowasumbua Mbatia na vilaza wenzake ni uelewa wa nini maana ya mtaala na na vitu gani vinarejelewa mtu anapoongelea juu ya mtaala. my take kabla ya kujadili kwa undani suala hili hakikisha unaelewa kwa kina maana ya MTAALA.

Wewe ndo kilaza na kawa mbwa wako. Kama ipo,nini kilimshinda kuitoa siku ile. Walimu kama watekeleza huo mtaala je wanaujua au kawa mbwa ndo anaujua pekee? Msiwe wepesi kuropoka kwenye msslahi ya kitaifa. Sasa hivi tinatumia mitasari ya 2010 na je hiyo ilitumia mtaala gani kutungwa kama ipo mitaala ya 2005?

MMEM/PEDP iliendeshwa kwa,mtaala upi?

Acha uchama nchi inapotea hii na,kawa mbwa watoto wake wako mbali na hii mitaala feki mnayo shabikia.
 
Mi naona kama waziri angetoa siku ile mheshimiwa tungemruhusu ajiuzuru ila hakupewa siku ile licha ya kumpa taarifa mapema kabisa mheshimiwa waziri wa elimu juu ya uhitaji wa mtaala huo siku inayofuata..
 
Mkuu,
Tunaomba dondoo za alichosema

Amesema iliyoletwa ni mfano wa mitaala lkn sio mitaala halisi, anajua fika nn Kawambwa alichofanya ili kufanikiwa malengo yake na akadai bado hoja yake iko palepale.
 
Wewe umeona wapi mtihani wa hisabati unakuwa na majibu ya kuchagua?a b c d ha ha ha ha
 
hata kama hiyo mitaala imewasilishwa haina tija kwa elimu ya sasa

Niliwahi kumsikia Mbatia akisema amefanya utafiti wa miaka zaidi ya kumi kuhusu elimu. Je ni vipi hakufanikiwa kuona mitaala ya elimu? Kuna uwezekano hii iliyowasilishwa ni mitaala feki. Waziri ni budi alete kumbukumbu za vikao vilivyoidhinisha mitaala hiyo ndio na sisi wengine tumwamini waziri maana waziri mwenyewe ni miongoni mwa mawaziri wababaishaji.
 
Jaman matokeo ya form four bado wadogo zetu acheni uoga yakitoka kila mtu atajua
 
MBATIA aliapa bungeni kwamba Waziri wa Elimu atakapowakilishwa mtaala wa elimu atajiuzulu ubunge kwani haupo tangu tupate uhuru.

Mtaala wa elimu umewakilishwa na kuundiwa Tume ya wabunge 6 itakayodhibitisha mtaala huo chini ya mama Magreth Sitta.

Tugemee nini kama itathibitishwa kwamba mtaala huo upo???

My Take:

Nilimsikia MBATIA kwa kinywa chake akitoa ahidi na kuapa kupitia TBC live kutoka bungeni kwamba ataachia ngazi.

Mdomo nyumba ya maneno. Huwezi kuisukuma gari ukiwa ndani ya gari.

Mbatia hilo unalo timiza ahadi yako endapo itathibitishwa kwamba ulilidanganya bunge na Watanzania. Kama atagoma kujiuzulu basi bunge litumie busara kumfukuza ubunge ili ahadi yake itimie.

Mtu huwa hana haki ya kuongea kitu bila kufanya Utafiti, Mbatia yupo sahihi juu ya hili kinachofanyia hapo na kutaka kuliondolea Taifa (Wizara) aibu, Kama hiyo mtaala ilikuwepo kwa nini isiwasilishwe mapema na je tujiulize hii mitaala huwa inahifadhiwa Wizarani tu maana huku mashuleni hatujawai kuiona na swali lingine la kizushi tujiulize hiyo mitaala iliyowasilishwa ilikuwa katika hali gani imechakaa au mipya kimuonekano?
 
Back
Top Bottom