MBATIA kufukuzwa Ubunge?

MBATIA kufukuzwa Ubunge?

Mbatia, ajiuzulu? Ili iweje? Kwa era hii ya ufisadi ni Lowasa tu ndiye aliyekubali ujinga huo.
 
Ninachojua ni kwamba mbatia aliomba mtaala wa mwaka 2005 na alisema kwa uhakika haupo, na akasema kama akionyeshwa kwa kipindi kile atajiuzulu ubunge wake! kilichofuatia hapo ni sarakasi, maigizo na ngonjera za serikali kama mlivyosikia mara kachukue kwa fulani mara nakala niliyonayo nimeichorachora and damn things like that, kwa mtu mwenye just average mind ataelewa kuwa kawambwa alikuwa hana mtaala genuine au hakuna kabisa na ikabaki danadana tu! sasa wamechapisha/wametunga mtaala mwingine wa 2005 kwa idadi nyingi kuliko ilivyohitajika bungeni kwa ushahidi ili kuchelewesha wapate muda wa kupika mtaala wao, it was a purposely dillydally to gain time to fabricate their so called mtaala!! hata hivyo kama wanaamini mtaala walioleta bungeni ni genuine kulikuwa kuna haja gani ya kuunda kamati ya kuupokea na kuthibitisha mtaala huo tena waziri akiwa miongoni mwa wanakamati na kumuengua mbatia mhusika mkuu!!? the whole drama is just like a new suitcase with full of stinking garbage in it!!
 
bado Mbatia yuko sahihi; muda aliotaka Mtaala wa Elimu uwasilishwe Bungeni aukuonekana; kwa maana haukuwepo kabisa tangu awali; sasa huu uliowasilishwa juzi kuna uwezekano mkubwa umeandaliwa fastafasta ili kuliondolewa Taifa aibu.

Huu ndo uhakika watu walijifungia wakazima moto, mtaala umeandikwa usiku kucha sasa sijui ni mtaala wa kawambwa au wa elimu ya tanzania! Nimefurahi wabunge wanauita mitaala wa Waziri Kawambwa! hahahahahahahaaa! Mbatia asijiuzulu, hii mitaala ni ya Kawambwa na yeye alitaka mitaala ya elimu ya tanzania, mtaala unaojibu maswali ya elimu aliayouliza kwenye hoja!
 
MBATIA aliapa bungeni kwamba Waziri wa Elimu atakapowakilishwa mtaala wa elimu atajiuzulu ubunge kwani haupo tangu tupate uhuru.

Mtaala wa elimu umewakilishwa na kuundiwa Tume ya wabunge 6 itakayodhibitisha mtaala huo chini ya mama Magreth Sitta.

Tugemee nini kama itathibitishwa kwamba mtaala huo upo???

My Take:

Nilimsikia MBATIA kwa kinywa chake akitoa ahidi na kuapa kupitia TBC live kutoka bungeni kwamba ataachia ngazi.

Mdomo nyumba ya maneno. Huwezi kuisukuma gari ukiwa ndani ya gari.

Mbatia hilo unalo timiza ahadi yako endapo itathibitishwa kwamba ulilidanganya bunge na Watanzania. Kama atagoma kujiuzulu basi bunge litumie busara kumfukuza ubunge ili ahadi yake itimie.

Kule mental hawathamini kiapo wanachoapa kwa jina la Mungu ,itakuwa hicho chake? Kiapo kilikwisha pale alipokwishatamka tu!
 
MBATIA aliapa bungeni kwamba Waziri wa Elimu atakapowakilishwa mtaala wa elimu atajiuzulu ubunge kwani haupo tangu tupate uhuru.

Mtaala wa elimu umewakilishwa na kuundiwa Tume ya wabunge 6 itakayodhibitisha mtaala huo chini ya mama Magreth Sitta.

Tugemee nini kama itathibitishwa kwamba mtaala huo upo???

My Take:

Nilimsikia MBATIA kwa kinywa chake akitoa ahidi na kuapa kupitia TBC live kutoka bungeni kwamba ataachia ngazi.

Mdomo nyumba ya maneno. Huwezi kuisukuma gari ukiwa ndani ya gari.

Mbatia hilo unalo timiza ahadi yako endapo itathibitishwa kwamba ulilidanganya bunge na Watanzania. Kama atagoma kujiuzulu basi bunge litumie busara kumfukuza ubunge ili ahadi yake itimie.

Nani atamuhukumu kwa kutotimiza kiapo cha kinjafiki. Kule mjengoni hata Mungu hawamjui kwani wanaapa kila siku na kufanya kinyume. Mbona hawana laana yoyote? Hata mola anajuwa kuwa hawa ni waongo tu!
 
Mbona shuleni kwetu hakuna au ni mtaala wa mawaziri tu...
 
Angalia kwa makini rangi ya mtaala aliouonesha Dr kawambwa. Una rangi tofauti na ule uliowasilishwa jana.

6-waziri%252Bwa%252Belimu%252BShukuru%252Bkawambawa%252Bakionyesha%252Bbaadhi%252Bya%252Bvitabu.JPG

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, akionyesha kimoja kati ya vitabu vinavyotumika mashuleni alipokuwa akijibu hoja mbalimbali zinazohusu elimu baada ya Mbunge wa kuteuliwa wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia, kuwakilisha hoja yake binafsi ya Udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini.
mba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nasari, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana

Huo mtaala umeanza kuandaliwa last week na watumishi wa pale wizarani walilazimishwa wafanye wawezavyo kuhakikisha nakala 300 zinapatikana kabla ya jumatatu week hii. lakini ukweli ni kwamba hakuna mtaala wa elimu tangu tumepata uhuru. Huwa tuna silabasi tu, nimeambiwa na mtu wa karibu sana ambaye ni mtumishi wa ngazi za juu wizara ya elimu
 
Kwa kuwa hoja binafsi zimezuiwa bungeni na kauli ya kuachia ngazi mbatia imezuiwa tehetehe! Kwa kukuwa ilikuwa kauli binafsi.
 
Someni makala ya dr. Mkumbo gazeti la raia mwema la leo muone tanzania ilivyo na viongozi uchwara. Waziri kawambwa ni kilaza,wabunge pia ni vilaza tu. Suala hili kwetu sisi wataalam ni dogo sana lakini limekuzwa na ukilaza na uvivu wa kufikiri wa wabunge na wafanya kazi wa wizara ya elimu. NASISITIZA KWAMBA TANZANIA HAKUNA DOCUMENTS ZINAZOITWA MITAALA. Kama kuna kitu kilichoandikwa juu yake mtaala either wa shule ya msingi au secondary kilichopelekwa bungeni,ninasikitika kuona kwamba wataalam wa mitaala wanalipotosha taifa. mbatia alipaswa kupewa elimu kuhusu maana ya mitaala

Mbatia anaapia vitu ambavyo havifahamu. hakuna nchi yoyote duniani ambayo haina mtaala. Mitaala ipo na kila ngazi ya elimu Tanzania ina mtaala wake sema neno mtaala si kitu kirahisi kueleweka kwa layman.
 
Mtaala upo nchi haiwezi kukosa mtaala. Tunapoongelea mtaala wa 2005 ni mabadiliko ya mtaala yaliyofanywa mwaka huo. Mabadiliko hayo yapo na yanadhihirika kwenye Sylabus mpya ya 2005. Kinachowasumbua Mbatia na vilaza wenzake ni uelewa wa nini maana ya mtaala na na vitu gani vinarejelewa mtu anapoongelea juu ya mtaala. my take kabla ya kujadili kwa undani suala hili hakikisha unaelewa kwa kina maana ya MTAALA.
 
Huo mtaala wameuchakachua
Bunge alinamamlaka ya kumvua ubunge.Pili ni mpaka Mh Mbatia alizike na mtaala uliyowasilishwa.na kama aliziki nao je nani wa kujiuzulu.SWALI kwanini waziri alipouwasilisha bungeni unachunguzwa kwanini wangeuweka wazi kijulikane kilichomo kabla ya usanii unaofanyika sasa.
 
Ajiudhuru kwa lipi? mbona mawaziri wengi hutoa kauli kama hizo lakini huendelea kupeta? wangetaka kumuwajibisha wangewasilisha mitaala hiyo kwa wakati.
 
Hiyo iliwakilishwa ni document to ambayo watu wamefanya kazi 24 hours kuitengeneza haikuwepo. Lakini kwa upande mwingine kama kila mwanasiasa angejiuzulu kwa kushindwa kufanya aliyosema Kikwete angekuwa ameondoka siku nyingi
 
MBATIA aliapa bungeni kwamba Waziri wa Elimu atakapowakilishwa mtaala wa elimu atajiuzulu ubunge kwani haupo tangu tupate uhuru.

Mtaala wa elimu umewakilishwa na kuundiwa Tume ya wabunge 6 itakayodhibitisha mtaala huo chini ya mama Magreth Sitta.

Tugemee nini kama itathibitishwa kwamba mtaala huo upo???

My Take:

Nilimsikia MBATIA kwa kinywa chake akitoa ahidi na kuapa kupitia TBC live kutoka bungeni kwamba ataachia ngazi.

Mdomo nyumba ya maneno. Huwezi kuisukuma gari ukiwa ndani ya gari.

Mbatia hilo unalo timiza ahadi yako endapo itathibitishwa kwamba ulilidanganya bunge na Watanzania. Kama atagoma kujiuzulu basi bunge litumie busara kumfukuza ubunge ili ahadi yake itimie.

Waziri hakuileta kwa wakati. Uchakachuzi tu huo. Hakuna mtu atayejiuzuru
 
Kwa style hiyo wangefukuzwa wengi maana wengi wameahidi ila hadi sasa bado 0. Mbatia go hakuna kualala.
 
Hongera sana mbatia! Umefanya watu watunge mtaala kwa wiki na kufanya uchakachuzi!
 
Kikwete aliahidi kugawa laptop kwa wanafunzi wa. Shule za Msingi....hatuko makini na serikali na bunge dhaifu
 
Back
Top Bottom