Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,
Brother "G", huu ninaokupa ni ushauri mzuri ambao utakusaidia kukulindia heshima yako nusu uliyobaki nayo sasa hivi.
Kumbuka Jimbo la Kawe ndio Jimbo namba 1 au 2 nchini kuwa na
1. Wasomi wengi.
2. Viongozi wengi wa Serikali, waliopo madarakani na wastaafu.
3. Wakuu wengi wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, waliopo madarakani na wastaafu.
4. Maspika wabunge wastaafu.
5. Baadhi ya wakuu wa vyama vya siasa.
6. Na raia wengine ambao wana uelewa mkubwa wa mambo.
Hivyo basi hayo makundi niliyoyataja hapo juu, hayatokuwa tayari kukurudisha bungeni ukaendelee kupiga pesa kupitia Jimbo hili again.
Ahadi ulizotoa mwaka 2020, mpaka sasa ni miaka mi3 ndani ya ofisi haujatimiza hata 15% ya kile ulichoahidi. Kwa kukusaidia tu, ngoja nikupe baadhi ya maeneo ambayo kama CCM wakikupitisha kugombea basi askofu "G" utaangukia pua mchana kweupe.
A. Mtaa wa SALASALA.
Toka uingie bungeni mwaka 2020, hadi leo hakuna kitu chochote cha maana ambacho ushaifanyia Salasala.
Barabara iliyopo ni moja tu ile inayotoka mbuyuni alafu inakunja pale katika ofisi ya serikali ya mtaa, inapita kwa spika wa bunge na kwenda kuishia mbele kidogo.
Maeneo mengine ni hovyo. Barabara zingine zilizobaki zote mbovu, hazipitiki kwa gari, baskeli wala bodaboda. japo mtaa upo katika eneo zuri kijiografia, hali ya hewa tamu na upepo mwanana kutoka mbezi beach unapanda hadi juu, ardhi safi ambayo haina milima milima ya hovyo nk. Miundo mbinu ya maji, umeme pia bado ni kikwazo kwa baadhi ya maeneo.
B. Mtaa wa MADALE
Huko nako ndo usiseme, yani hata ile barabara ya Madale imekosa wa kuisimamia. Imekuwa kama vile njia ya kupitia ng'ombe kwenda malishoni. Japo eneo lina hadhi ya kishua kama Salasala lkn usimamiaji wa miundo mbinu umekuwa hakuna, hadi kupelekea watu sasa wanajijengea hovyo kama mwananyamala kisiwani au vingunguti.
Maeneo ambayo umeyaacha katika Jimbo ni mengi, haina haja ya kuyataja yote, ila unachotakiwa kujua ni kwamba 2025 hautapita katika ubunge hata ukija na porojo gani.
Kama unataka uendelee na ubunge basi una options mbili.
1. Kufanyia kazi changamoto zote za miundombinu ya Jimbo angalau kwa 60% alaf zilizobaki utamaliza katika kipindi cha pili cha 2025 to 2030.
2. Au ukagombea katika majimbo mengine kama vile Temeke, Mbagala au Ukonga ambayo yana idadi kubwa ya waswahili.
Uchaguzi ujao wana Kawe watamchagua mtu mwenye uwezo wa kweli wa kuleta maendeleo Kawe, bila kujali ni wa chama tawala au upinzani.