Mbaroni kwa kujaribu kuchoma shule ya kiislamu

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,336
Toka wilayani hai mkoa wa Kilimanjaro Wanafunzi wa 3 wanashikiliwa na Polisi kwa kujaribu kuchoma Bwalo la chakula la shule ya Othman bin Hasani

Source Radionesterio

========
Wanafunzi watatu wanaosoma masomo ya Dini Katika Chuo kinachotoa mafunzo ya Quran na hadithi za Mtume cha Othuman Binhassan kilicho chini ya Msikiti wa Othman Bomang’ombe Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuchoma moto bwalo la chakula linalotumiwa na wanafuzi wa chuo hicho.

Tukio la kuchomwa moto bwalo hilo limetokea Jumapili ya tarehe 11 Octoba 2020 wakati waumini wa msikiti huo wakiendelea na Swala ya adhuhuri ambapo kufuatia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Hai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Lengai Ole Sabaya amefika msikitini hapo kukagua athari na kupata taarifa ya tukio hilo.

Sabaya amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi wilayani humo linawashikilia wanafunzi watatu ambao wamekiri kuhusika na tukio hilo huku akilipongeza jeshi la polisi kwa jitihada walizofanya kwa muda mfupi za kufanikisha kuwakamata na kulitaka jeshi hilo kuendelea na uchunguzi ili kubaini sababu za tukio hilo.

“OCD mimi nakupongeza sana wewe na vijana wako kwa kazi mliyoifanya ya kuhakikisha kwamba angalau tumetatua kitendawili cha nani amechoma, hili ni tukio letu la kwanza kwenye wilaya ya Hai na tulikubaliana kwamba kwenye wilaya hii matukio ya namna hiyo hayatatokea”. Amesema Sabaya.

“Hapa tumepata watu watatu ambao wamethibitika wamechoma moto jengo hilo, kwa hiyo muendelee kuwahoji vizuri wawaambie kama kuna wengine na waseme wanafanya project ya nani na walitaka kuwauwa wangapi ili tufikishe hitimisho hii ajenda mpya yakuchoma maeneo na taasisi mbalimbali”. Ameongeza Sabaya.

Aidha Sabaya ameuomba uongozi wa msikiti na chuo hicho kuhakikisha kuwa unaendeleza uhusiano mzuri baina yao na serikali kwani kwa kupitia ushirikiano wa katibu ni rahisi kubadilishana taarifa na kuweza kuzuia vitendo vya uhalifu kabla havijatokea.

Awali akisimulia tukio hilo Msimamizi Mkuu wa chuo hicho na imamu wa msikiti huo Abdala Juma amesema kuwa kabla ya tukio la moto kulitokea upotevu wa simu za wanafuzi 68 ambazo ziliibiwa na wanafuzi hao watatu na kwenda kuzificha kwenye dari la msikiti ambapo amesema kuwa walipowahoji wanafunzi hao walisema kuwa waliamua kuchoma jengo hilo moto ili chuo kifungiwe na wao wapate fursa yakutoroka na simu hizo.

“Tuna utaratibu wanafunzi wote wakifika simu zao tunazichukua na kuziweka kwenye chumba cha kiongozi, watuhumiwa hao walivizia tukiwa msikitini wakaiba zile simu zote wakazificha na baada ya hapo tukafanya uchunguzi wakahisi tutawakamata.”

“Baada ya tukio tuliwahoji wakasema waliamua kuwasha moto ili chuo kifungwe na kikishafungwa wapate fursa ya kuchukua zile simu waondoke nazo kutoka mahali walipozificha juu ya dari ndani ya msikiti”. Amesema Imamu Abdala Juma.

Kuhusu madhara amesema kuwa moto huo umeteketeza magodoro 8, mabegi sita na nguo chache za wanafuzi huku vitu vingine vikiokolewa.

Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kuungua kwa moto mabweni katika shule mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka hivi sasa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi katika matukio hayo ili kubaini chanzo chake.

1603039678290.png

1603039732344.png
 
Hao nao eti wamewasha moto jengo liungue ili chuo kifungwe waondoke na simu.

Hawa sasa ndio walioenda kusomea ujinga kama FF anavyodai.
Sweetie mzima wewe..? Nimekuhamu Kama upepo mwanana uvumao kwenye vilindi vya mto swafi!.. Ni wewe unurishae mapafu yangu kwa kuyajaza hewa Safi huku ukiniimbia ule ushairi pendwa kwa sauti yako nyororo isiyo kasoro!.. niite nami nitaitika laazizi na tena nitakuenzi kwa utenzi..😉
 
Movie la kihindi hili! Kumbe ni wenyewe kwa wenyewe? Hapa Kuna mwanzisha tukio ili apate platform ya kusema na kuonekana Kama mpigakazi asiyechoka na mwenye mbinu Kali za kiitelejinsia! Ocd na mkuu wa wilaya wanajisafisha Kiana huku wakibakiwa na mabaka ya uchafu! Watafute Kiki nyingine kwani hii imebuma na Kama huamini fuatilia mlaka mwisho Kama Kuna mtu atakwenda jela kwa hili!
 
Hapa mimi sijaelewa
Jengo lililochomwa ni bwalo la chakula
"Kuhusu madhara amesema kuwa moto huo umeteketeza magodoro 8, mabegi sita na nguo chache za wanafuzi huku vitu vingine vikiokolewa"
Inamaana wanafunzi walikua wanalala kwenye hilo bwalo la chakula?
 
Sweetie mzima wewe..? Nimekuhamu Kama upepo mwanana uvumao kwenye vilindi vya mto swafi!.. Ni wewe unurishae mapafu yangu kwa kuyajaza hewa Safi huku ukiniimbia ule ushairi pendwa kwa sauti yako nyororo isiyo kasoro!.. niite nami nitaitika laazizi na tena nitakuenzi kwa utenzi..😉
😍😍😍😍😍

Karibu Hai.
 
Kama kwenda kusoma chuo cha dini ni ujinga basi watafutie shule ya mashoga ambao nyie wa upande wa wazungu mumeuuunga mkono na kudiriki makanisa kufungisha kuhalalisha na kufungisha hizo ndoa za jinsia moja
Hao nao eti wamewasha moto jengo liungue ili chuo kifungwe waondoke na simu.

Hawa sasa ndio walioenda kusomea ujinga kama FF anavyodai.
Ujinga
 
😍😍😍😍😍

Karibu Hai.
sawima kwako nimetulia kama maji ya mtungini!.. ukoko kwenye sufuria nitakwangu sirini.. nifanye niwe wako unipe joto lako!,nipe na moyo wako nikufikishe kunako.

Weye ndo wangu malkia sifa zote nakumwagia! Achana na wabeba sufuria vinyeramumo watavalia.
Niyasemayo yatoka moyoni na niyafanyanyo yatoka rohoni.. wewe ni Kama sumaku kwangu hakika siwezi kukimbia! Uzuri wako ni bahari kwangu samaki wote wanipatia!.. nisitie maneno mengi ukajaniona mi mshenzi! Njoo kwangu mpenzi kivyovyote hutokosa mapenzi..😉
 
Hapa mimi sijaelewa
Jengo lililochomwa ni bwalo la chakula
"Kuhusu madhara amesema kuwa moto huo umeteketeza magodoro 8, mabegi sita na nguo chache za wanafuzi huku vitu vingine vikiokolewa"
Inamaana wanafunzi walikua wanalala kwenye hilo bwalo la chakula?
Twendelee kula mtori nyama tutazikuta chini.

Wanamtafuta Mwenyekiti
 
sawima kwako nimetulia kama maji ya mtungini!.. ukoko kwenye sufuria nitakwangu sirini.. nifanye niwe wako unipe joto lako!,nipe na moyo wako nikufikishe kunako.

Weye ndo wangu malkia sifa zote nakumwagia! Achana na wabeba sufuria vinyeramumo watavalia.
Niyasemayo yatoka moyoni na niyafanyanyo yatoka rohoni.. wewe ni Kama sumaku kwangu hakika siwezi kukimbia! Uzuri wako ni bahari kwangu samaki wote wanipatia!.. nisitie maneno mengi ukajaniona mi mshenzi! Njoo kwangu mpenzi kivyovyote hutokosa mapenzi..

Hizi porojo zitakutoa kamasi tu mdogo wangu, toa hela unakwarua kirahisi tu.

Kuna wazee wa migodi, hawagongagi hodi... we jifanye unafuga unachunga ila wao ndo wanalipa kodi.

I moved your cheese, so what!
 
Back
Top Bottom