Bikirembwe
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 250
- 7
Familia moja ilishangazwa pale walipopokea jeneza la marehemu mama yao
aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.
Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana ndani ya jeneza kiasi
kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza!
Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna
hii:
"Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya
mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Machame, katika nyumba ya ukoo. Samahani sikuweza kuja na mwili kwani
nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi
huu.
Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa
makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe. Mgawane
hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi.
Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili
ya mtoto mkubwa wa Mushi. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya
watoto wa Urassa na Kwayu, natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu.
Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya
Manka, na zinazobaki ni za watoto wake. Hizo jeans mpya 2 ambazo mama
amezivaa ni za wavulana. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni
zawadi ya Koku kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti
Rebeka, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.
Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama
nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani
hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana.
Dada yenu mpenzi,
Mama Manka